Kipindi cha bibi bomba kinadhalilisha bibi zetu

asau

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
14
Reaction score
4
Kipindi kinaendeshwa na clouds TV.

Nimebahatika kuangalia japo kidogo kipindi hiki na kuona hakina maudhui mazuri vilevile wale vijana au sijui ni majaji wanawauliza bibi zetu maswali ya kuwadhalilisha.

Mfano:
Swali: Yule jirani yako snacks hajambo na bibi mmoja aliyeulizwa akajibu hamfahamu na akataja kuwa yeye kabila lake ni Fulani.

Kilichofuata hapo ni vicheko kwa maana ya bibi huyo kutofaamu maana ya snacks,na maswali mengine ya kipuuzi ambayo si ya kuangalia kweli bibi zetu wana uelewa gani.

Cha kusikitisha zaidi kuna watu kama Regina Mwalekwa ambaye zamani alipokuwa redio one alikuwa ni mtu wa kuuliza maswali yenye ufahamu nay a kiudadisi lakini tangu ajiunge huku nay eye amepoteza heshima yake, pole sana dada.

Tafadhali tusiwaruhusu bibi zetu kwenda kwenye shindano kama hili la kuwadhalilisha na kuendeshwa na wahuni.
 
wenyewe wapenda pesa za bure wacha wadhalilike
 
Kweli kabisa na mimi nimeliona hilo. Yani kuna udhalilishaji wa hali ya juu kwa kweli. Maswali wanayowailiza yamejaa kejeli halafu wakishindwa kujibu wanawacheka. Kipindi kinakera badilikeni.
 
poor tackling of the questions plus irrelevant hosts of bibi bomba.according to the nature of bibi bomba it supposes to have an adult hosts.
 
Kipindi kinaendeshwa na clouds TV
Nimebahatika kuangalia japo kidogo kipindi hiki na kuona hakina maudhui mazuri vilevile wale vijana au sijui ni majaji wanawauliza bibi zetu maswali ya kuwadhalilisha
Mfano:
Swali: Yule jirani yako snacks hajambo na bibi mmoja aliyeulizwa akajibu hamfahamu na akataja kuwa yeye kabila lake ni Fulani.
Kilichofuata hapo ni vicheko kwa maana ya bibi huyo kutofaamu maana ya snacks,na maswali mengine ya kipuuzi ambayo si ya kuangalia kweli bibi zetu wana uelewa gani.
Cha kusikitisha zaidi kuna watu kama Regina Mwalekwa ambaye zamani alipokuwa redio one alikuwa ni mtu wa kuuliza maswali yenye ufahamu nay a kiudadisi lakini tangu ajiunge huku nay eye amepoteza heshima yake, pole sana dada.
Tafadhali tusiwaruhusu bibi zetu kwenda kwenye shindano kama hili la kuwadhalilisha na kuendeshwa na wahuni.
Kwani nawewe BIBI yako bomba?
 
wenzako(prime time promo)wana kamsemo kao!TWENDE ZETU,TUMIA FURSA,acha wazaririke c njao zao,we bibi mzima una ambiwa kata mauno na wa2 ambao ni kama wajukuu zako!
 
Hivi hiki kipindi kinalenga kuifundisha nini Jamii? Ni udhalilishaji tu wa Wazee wale, lugha, ukaaje wao havina maadili kabisa. Huyu kijana nae hana maadili kabisa ya uongozaji wa kipindi hiki, nashauri kipindi hiki kifutwe au kibadilishwe maudhui

Sorry ni Maadili sio hicho nilichokiandika
 
Yan kuliko nikiangalie aheri nitafute kazi ya kufanya its so stupid hakifundishi chochote 😡😡😡
 
Ni upuuzi mtupu, wanaacha kubuni vipindi vyenye tija badala yake wanaonyesha ujinga. Harafu pia kuna kila kipindi cha ijumaa nadhani ni weekend chat show kama sikosei kuna yule dada anaboa sana too much show off, harafu ni mbaya lakini analeta maringo ya kijinga. Au huwa anapata stimu kwanza maana anajishebedua kama nn I hate the session coz of her.
 
Ukiendelea tazama clouds utakua mwehu hio ni channel ya wahuni
 
Hivi hiki kipindi kinalenga kuifundisha nini Jamii? Ni udhalilishaji tu wa Wazee wale, lugha, ukaaje wao havina maadili kabisa. Huyu kijana nae hana maadili kabisa ya uongozaji wa kipindi hiki, nashauri kipindi hiki kifutwe au kibadilishwe maudhui

Sorry ni Maadili sio hicho nilichokiandika

Mie nadhani katika organization yoyote ile uongozi ukiwa mbovu, automatically kila kinachofanyika huwa ni kibovu!!!

Titizo la vipindi vyao linaanzia kwenye uongozi husika. Katika hali ya kawaida kwa uongozi makini hauwezi kuruhusu kipindi kisichokuwa na tija kama kipindi kile cha bibi bomba kurushwa hewani!!!

TAFADHARI KAMA KUNA MWANA CLOUDS TV HUMU NDANI; FUNGUKA UTUELEZE NINI JAMII INACHOJIFUNZA TOKA KWA VIKONGWE WALE NA NAMNA KWA UJUMLA KIPINDI KINAVYOENDESHWA!!!!
 
Mleta mada hicho kpindi ni watanzania wangapi wana habari na hicho kpnd mana walio wengi hatujawahi wala hatujui ni tv ipi inayokirusha. Think national wize (tv za mitaa)
 
nashukuru mleta uzi nahisi bibi zetu wanapigishwa pombe kabla hawajanza kuingia kufanya mambo yao maana wanaonekana kabisa wameacha akili zao kwa mda.ule wa shooting
 
Ni upuuzi mtupu, wanaacha kubuni vipindi vyenye tija badala yake wanaonyesha ujinga. Harafu pia kuna kila kipindi cha ijumaa nadhani ni weekend chat show kama sikosei kuna yule dada anaboa sana too much show off, harafu ni mbaya lakini analeta maringo ya kijinga. Au huwa anapata stimu kwanza maana anajishebedua kama nn I hate the session coz of her.

copy and paste (nikikuta kwang wanatazama nabadili channel na boreka sana)
 
hakuna udhalilishaji wowote wanaofanyiwa pale...kwanza kabsa wanafundisha jinsi ya kuishi na mabib..kwamba unatakiwa umpende na kumsikiliza + utenge muda wa kuongea na mabibi zako....pili wanawafanya mabibi wajihisi kumbe jamii nayo inawakumbuka na kuwajali uwepo wao...vijana wa siku izi hawajui umuhim wa mabib wala hawawajali mabibi zao...wanawaona ni wazee na kuwaacha wawe na msononeko....
 
Duh kweli tuko tofauti nimeamini

Upumbavu mtupu kuwakosea heshima bibi zetu.Wanawa valisha nguo za kubana makalio. wanawaambia eti wakate viuno kisa eti umasikini wao kama wanataka kuwasaidia wawape hiyo hela sio kuwadharirisha.
 
hakuna udhalilishaji wowote wanaofanyiwa pale...kwanza kabsa wanafundisha jinsi ya kuishi na mabib..kwamba unatakiwa umpende na kumsikiliza + utenge muda wa kuongea na mabibi zako....pili wanawafanya mabibi wajihisi kumbe jamii nayo inawakumbuka na kuwajali uwepo wao...vijana wa siku izi hawajui umuhim wa mabib wala hawawajali mabibi zao...wanawaona ni wazee na kuwaacha wawe na msononeko....

Tatizo la hiki kipindi nafikiri management imekosea kuacha hiki kipindi cha bibi zetu kuendeshwa na kitukuu.unafikiri kuna maadili yatapatikana hapo?...unaacha bibi anasema ..hey! Hey! Whatssap ma nigga!???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom