Kipindi cha bibi bomba kinadhalilisha bibi zetu

Kipindi cha bibi bomba kinadhalilisha bibi zetu

Ni kweli, wengi wa TZ ndivyo tulivyo, vipindi vya kuelimisha wengi wanavikwepa ila hivi vya ujinga ujinga hata kiwe saa tano usiku watu watakisubiri na kuangalia.

Na utashangaa hata Kikwete anaangalia au mtu mwenye akili timamu kabisa anajipangia asikose kipindi, then asubuhi utamsikia anasimulia kwa mbwembwe kabisa huku akinywa supu. Yaani basi tu....huku kupata television ukubwani kuna madhara yake haki ya nani.
 
Samahani kwa atakayeumia, ila ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya watanzania inapenda vitu vya kijinga na visivyo na maadili ndani ya jamii, mfano angalie jinsi watu wanavyoshupalia kipindi cha big brother africa. Jiulizeni kile kipindi kina maadili gani hapa TANZANIA?

Kwa kweli kipindi kimejaa udharirishaji kwa bibi zetu. Kuna kijana mmoja anakera na kuchefua. Mfano anamuuliza bibi wa watu eti umeisha wahi kula facebook? Au eti burger ni mshikaji wako? Jamani what a silly question? Tena unamuuliza bibi toka Kimanzichana. Huyo kijana sijui hana wazazi? Au ndio wale waliozaliwa Ulaya?
Nafikiri kuna haja ya maboss wa tv zetu kufuatilia program zao.
 
kipindi kinaitwa bibi bomba, anatafutwa bibi anayeyajua mambo ya dot.com, i.e facebook, twiter, instagram, whasapp, misos ya kileo burger, pizza etc mizik ya kisasa i.e kucheza viduku, ku'bang hiphop etc kubana ------ kwa pamba za kileo eg. Pedo, skin jeans, tights etc na maushenz mengine ya sheitwan! HUYO NDO BIBI BOMBA WA CLOUDS TV.
 
Mimi sikuanzisha mada kwa ajili ya Clouds TV, jaribu kuwa mwelewa nilichokisema ni kipindi, kutokupenda kipindi it has nothing to do with Clouds Tv.....usikuirupuke Mpwa
wanao diss bib bomba ni wale ambao hawana mda na mabibi zao...hata hawatanian na mabib zao...aliyeanzisha hiki kipind nampa salut kubwa sana...haterz wa clouds mkae tu mkidis wenzenu wanafanya yao...hahaha hatari sana...
 
hakuna udhalilishaji wowote wanaofanyiwa pale...kwanza kabsa wanafundisha jinsi ya kuishi na mabib..kwamba unatakiwa umpende na kumsikiliza + utenge muda wa kuongea na mabibi zako....pili wanawafanya mabibi wajihisi kumbe jamii nayo inawakumbuka na kuwajali uwepo wao...vijana wa siku izi hawajui umuhim wa mabib wala hawawajali mabibi zao...wanawaona ni wazee na kuwaacha wawe na msononeko....

Haya namababu nao wanawekwa kundi gani?mi kinaniboa tuuuuuu yan sikipendiii
 
Baba mwanaasha anakipenda hicho kipindi,si mnajua aliandaliwa kipunga cha birthday cellebration 2010.
Mwanahalisi limepigwa ban,utumbo huu unaachwa
 
Sasa tuandamane basi kupinga kudhalilishwa bibi zetu.yule kijana anayejiita mme wao bado kidogo ''atawananihi''stupid
 
Hivi hiki kipindi kinalenga kuifundisha nini Jamii? Ni udhalilishaji tu wa Wazee wale, lugha, ukaaje wao havina maadili kabisa. Huyu kijana nae hana maadili kabisa ya uongozaji wa kipindi hiki, nashauri kipindi hiki kifutwe au kibadilishwe maudhui

Sorry ni Maadili sio hicho nilichokiandika

kusema kweli hata sielewi dhumuni la kipindi hiki. Kwanza hata muendesha kipende mwenyewe hajatulia. Mabibi wenyewe hawajielewi, yaani uelewa wao ni mdogo sana wakati mwingine huwa naona kama wanadhalilishwa tu.
 
Sasa tuandamane basi kupinga kudhalilishwa bibi zetu.yule kijana anayejiita mme wao bado kidogo ''atawananihi''stupid
masiala masiala mwisho kweli atawananihiii, huwa simuelewi kabisa...ni aibu kubwa sana kwa jamiii kuacha utumbo huu unaendelea
 
nadhani tatizo lipo kwa mtangazaji wa kile kipindi analeta usela sana kwa wale mabibi ambayo inaonekana kuwadharirisha sababu tu umaskini....kwetu Afrika umri ni kitu kikubwa sana.
 
Ukweli uko wazi. Kipindi kinadhalilisha wazee wetu na anasema hakifanyi hivyo ampeleke bibi yake. I hate that show for real
 
kusema kweli hata sielewi dhumuni la kipindi hiki. Kwanza hata muendesha kipende mwenyewe hajatulia. Mabibi wenyewe hawajielewi, yaani uelewa wao ni mdogo sana wakati mwingine huwa naona kama wanadhalilishwa tu.

Mabibi wako kwenye revolution age!akili imeishaanza kurudi kwenye utoto!ndo maana kila wanachoambiwa wanafanya hakuna ubunifu wala matakwa yao binafsi!
 
kusema kweli hata sielewi dhumuni la kipindi hiki. Kwanza hata muendesha kipende mwenyewe hajatulia. Mabibi wenyewe hawajielewi, yaani uelewa wao ni mdogo sana wakati mwingine huwa naona kama wanadhalilishwa tu.

Mabibi wako kwenye revolution age!akili imeishaanza kurudi kwenye utoto!ndo maana kila wanachoambiwa wanafanya hakuna ubunifu wala matakwa yao binafsi!
 
Kwa kweli kipindi kimejaa udharirishaji kwa bibi zetu. Kuna kijana mmoja anakera na kuchefua. Mfano anamuuliza bibi wa watu eti umeisha wahi kula facebook? Au eti burger ni mshikaji wako? Jamani what a silly question? Tena unamuuliza bibi toka Kimanzichana. Huyo kijana sijui hana wazazi? Au ndio wale waliozaliwa Ulaya?
Nafikiri kuna haja ya maboss wa tv zetu kufuatilia program zao.

Sasa utashangaa watu wanachekelea hayo maswali. Sijuwi nani waratibu wa hivi vipindi, yaani utashangaa jitu zima linashupalia upuuzi kama huu. Hawa watu wamekuwa worse than Ze Comedy for their lame jokes ambazo badala ya kucheka unabaki unajiuliza what's the hell huku ukilia.
 
nadhani tatizo lipo kwa mtangazaji wa kile kipindi analeta usela sana kwa wale mabibi ambayo inaonekana kuwadharirisha sababu tu umaskini....kwetu Afrika umri ni kitu kikubwa sana.

Ni kweli kwetu afrika umri ni kitu kikubwa ila tatizo liko kwa wale vijana kijifanya wamarekani weusi na kupotosha maadili ya taifa letu. They are so silly na inabidi kipindi kifutwe.
 
Its too bad,eti bibi anafanya promo na anatamka 'nahitaji huo mtonyo'sasa ujiuliza bibi na neno mtonyo wapi na wapi.

Sasa ukijiuliza theme ya hicho kipindi,hupati jibu,ni ujanja ujanja wa kupiga hela.
 
Upumbavu mtupu kuwakosea heshima bibi zetu.Wanawa valisha nguo za kubana makalio. wanawaambia eti wakate viuno kisa eti umasikini wao kama wanataka kuwasaidia wawape hiyo hela sio kuwadharirisha.

Fursa hizo si unajua radio na TV husika ina uwezo wa kuonesha fursa?????????
 
wangekuwa wabunifu wangeuliza maswali ya maana ili akina bibi hao waweze kuifunza jamii ya leo.....kazi tunayo
Its too bad,eti bibi anafanya promo na anatamka 'nahitaji huo mtonyo'sasa ujiuliza bibi na neno mtonyo wapi na wapi.

Sasa ukijiuliza theme ya hicho kipindi,hupati jibu,ni ujanja ujanja wa kupiga hela.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom