Mi mpaka naona aibu kuangalia maana udhalilishaji ule
unachosema ni sahihi lakini kumbuka huwa wanakwenda pasi na kujua aina ya maswali watakayiokumbana nayoMi siwapendi clouds ila naomba kuuliza,hivi wale wa bibi si wana toto?wanalazimishwa na watoto zao au wajukuu zao kwa nini wasiwazuie?
Ni upotovu wa maadili, na udhalilishaji... ni jukumu la serikali kupitia vyombo husika kuhakikisha watu hawadhalilishi kwa sababu ya njaa zao, au kitu chochote kile. Tena kuwatumia wazee ambao huenda they are of unsound mind ili kujipatia faida ni kosa kisheria.Je
kwenye hili shindano la bibi bomba tuwalaumu waendeshaji kwa
ku2dhalilishia bibi zetu, au 2walaumu awa mabibi kwa kukubali
kudhalilishwa, je tatizo ni njaa ndio iliowapeleka au kutokuona aibu,
ebu jifkirie yule bibi anaeambiwa amtongoze yule mvulana mpaka akubali
au yule aliepo kwenye tangazo anaesema yoyoyoyo your sup niga ingalikua
weze wako ungalijiskiaje? ama kwa upand wangu ingalikua wazee wangu nafkiri mulizaji na mtayarishaji vitu vizito vyenye ncha kali vingaliwahalalikia.
Wanasheria wetu siyo wajasiriamali, vinginevyo hiyo kesi mtu unainunua na unashinda. Umdhalilishe bibi yangu kiasi kile halafu nikuache, thubutu.!nachukia hicho kipindi with all ma heart ... kuna vitu wangeweza wakaprogram wabibi wakawa wanafundisha jamii kwa vitendo lakini kwa hili ni upuuzi tu
Na uyu anaewahoji na mipanki yake ya kishamba bora uyo kinyozi angalimchinja, kuna uyu bibi ati amempa maik ili arapu duh c juwi wajukuu zake wanajiskiaje? Wakimuona bibi yao anazinguliwa vile.
Wanasheria wetu siyo wajasiriamali, vinginevyo hiyo kesi mtu unainunua na unashinda. Umdhalilishe bibi yangu kiasi kile halafu nikuache, thubutu.!
hakuna kipindi cha kipuuzi kama hicho nchini au tuseme africa nzima.
Hamna tatizo pale, mida fulani watu wanajiinjoi kwa kuwa 'vikatuni'. Pia huwa hawatekwi kwamba lazima waenda kushiriki. Endapo m'bibi hajisikii basi aache kwenda na pia kuukosa mkwanja. Ni sehemu ya burudani tu.