Kipimajoto ITV miaka 18 bila Baba wa Taifa; Je, misingi ya utaifa aliyosimamia inaenziwa na kuendelezwa

tatzo lako moja una tafiti ,,maprofesa wenye akili wapo wengi tu tatzo mfumo ndio kikwazo? ,,,naweza kukutajia maprofesa ambao waliondka nchni kwasababu ya mambo mbalimbali,

Kama wapo basi ndiyo hao waliopo katika hiyo 10% yangu niliyoisema hapo juu ila wengi wao 90% ni wa ' hovyo hovyo ' watupu. Nina uhakika na ninachokisema na ndiyo maana katika Wanataaluma ambao naongoza kwa ' kuwadharau ' ni hawa wenye ' Titles ' za Uprofesa kutokana na kwamba wameshindwa kuisaidia Tanzania Kitaaluma na kuelekeza mawazo yao katika kusaidia kuijenga nchi na wamebaki tu kujisifia kumiliki huo ' Uprofesa ' wao. Kuna tofauti kubwa mno ya Maprofesa wa Ulaya, Asia, Middle East na America dhidi ya Maprofesa wa Afrika hasa hawa wa Sub Saharan Africa ( Tanzania ) ikiwemo.
 
VIzuri tu,na hapo ndipo anapo stahili kukaa siku zote..afyate mdomo wake aongee ya msingi sio pumba.
 
Inasikitisha sana. Pole pole anavyoongea vile ni kwamba kweli anaamini hivyo ama ni kulinda tu tumbo lake. Na kweli ameanza kupata mashavu hivyo ni lazima atetee uozo.
 
Kama wapo basi ndiyo hao waliopo katika hiyo 10% yangu niliyoisema hapo juu ila wengi wao 90% ni wa ' hovyo hovyo ' watupu. Nina uhakika na ninachokisema na ndiyo maana katika Wanataaluma ambao naongoza kwa ' kuwadharau ' ni hawa wenye ' Titles ' za Uprofesa kutokana na kwamba wameshindwa kuisaidia Tanzania Kitaaluma na kuelekeza mawazo yao katika kusaidia kuijenga nchi na wamebaki tu kujisifia kumiliki huo ' Uprofesa ' wao. Kuna tofauti kubwa mno ya Maprofesa wa Ulaya, Asia, Middle East na America dhidi ya Maprofesa wa Afrika hasa hawa wa Sub Saharan Africa ( Tanzania ) ikiwemo.
Swali dogo tu kama polepole angekuwa profesa kwa kipndi kile na polepole wa sasa wewe ungemwka katika % ipi kati ya 10% na 90%
 
Naangalia kipima joto hapa, Ndg. Pole Pole kawekwa katikati ya Proffesa Baregu na Proffesa mwingine hapa kuongelea miaka kumi na nane bila Baba wa Taifa, je misingi ya utaifa aliyoasisi inaenziwa!?

Ndg Pole Pole hapa anayoongea ki uhalisia hayaendani na Mada na amepwaya mbele ya wachangia Mada wengine.

Hili linaweza lisiwe kosa lake maana watu alionao sio level yake! Ni kosa la muandaa kipindi! Huwezi kumuweka Pole Pole katikati ya wazee tena maprofesa kujadili jambo! Huyu alitakiwa kukaa pembeni na kuwasikiliza kujifunza kutoka kwao

Lakini Humphrey mbona ni mzee pia?
 
Tatizo la vijana wa tanzania ni kuoneana wivu na.mambo yasiyo ya msingi,

Si kwamba pole pole kaenda nje ya mada kabisa kuna mazuri pia kachangia ,

Ila.kwakuwa.tumezoea kuja na ID fake na kupinga kila.kitu basi mnadhani mnajenga kumbe tunadumaza akili zetu,

Jamii yetu imemzunguka majungu na pointi pembeni,

Humphrey si ndo huyu mlikuwa mnamshangilia akiwa na warioba?

Tuwe fair

Hebu fanya mpango wa kurudisha pesa za watu kwanza ulizotapeli kupitia uzi wako kule julwaa la biashara kisha baadaye uje kwenye huu uzi please.
 
Je,hao wezi wameiba wakiwa wapi?

Je,Wakati wanaiba hapakuwa na Vyombo vya dola?

Je, wakati hao wezi wanaiba polepole hakuwa kwenye chama tawala ili ashiriki kuwakamata?

Je, wakati hao wezi wanaiba palikua hakuna serikali iliyoapa kulinda rasilimali za nchi?

Huo unaoitwa wizi ni propaganda za kuwapumbaza na kuwaliwaza wajinga ili waaminishwe kuwa mali zao sasa watazipata matokeo yake ni kuzidi kuwarudisha nyuma watanzania ambao walikua wameshaanza kuingia kwenye biashara za kimataifa bila hofu.

Kwa nini viongozi waliotangulia wakiwemo Mawaziri hawajitokezi wakasema ukweli kuwa ni kwa nini busara iliwaongoza kufanya hayo yanayodharauliwa na kupuuzwa leo wakati kiuhalisia ndiyo yaliyoleta maendeleo Makubwa ya kiuchumi na kuweka misingi na dira za maendeleo kwa watanzania?
Mbona Summaye alijitokeza akasema ukweli kuwa nyumba za serikali ziliuzwa baada ya serikali kujadili kwa kina na kuona ni busara ziuzwe!?
Sasa kama kuna makosa machache yalifanyika hatuwezi kuona kuwa nchi hii ilikua na wezi watupu!!
Hii sio sawa wanachafua watangulizi wao kwa faida za kisiasa lakini pia wanatuonyesha kuwa CCM haina viongozi safi walioandaliwa kitaasisi mpaka atokee mtu mmoja tu kwa bahati nasibu.

Haiwezekani waliopita wato walikua ni wezi tu!
Kama ni hivyo Hao wazuri wamezaliwa lini mana naona hakuna kizazi kilichozaliwa leo zaidi ya watu wale wale tofauti ni madaraka alikua pale jana leo hapa.

Lazima pia tukumbuke kwa mfano kuwa kuna busara iliyokuwa inatumika kuongoza. Mfano kwa nini tusiangalie busara ya kumfanyia wepesi mtu kama Dangote aliyewekeza kiwanda chenye mtaji wa zaidi ya tri.1.3. Ule wepesi au baadhi ya vimisamaha ndiyo iliyomvutia kuja na kutumia tril. of money kuwekeza TZ. Sasa kusimama na kiwaita watu waliokaa na kuja na busara zao kulingana na wakati huo na changamoto zake ni kutowatendea haki wengine waliowahi kuongoza nchi hiyo.
 
Back
Top Bottom