Kipimajoto ITV miaka 18 bila Baba wa Taifa; Je, misingi ya utaifa aliyosimamia inaenziwa na kuendelezwa

cyrustheruler

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
2,044
1,867
Tazama Bwana Humphrey Polepole, Prof. Baregu na Prof. Mbwiliza wanachangia hoja kuhusu miaka 18 bila baba wa Taifa; Je, misingi ya utaifaa aaliyoisimamia inaenziwa na kuendelezwa?
 
hapana haienziwi japo kuna viongozi wanajitahidi kuienzi lakini inashindikana kwa sababu ya tamaaa ya madaraka na mali mwalim aliifanya tanzania kama ya kwake ndo maana alijitoa kwa dhati kutumikia taifa na kama angekuja leo angetamani arudi alipo kuwepo maana mambo ni shaghala bhaghala yaani vululu vululu
 
Tazama Bwa.H.Polepole anatabaruku
Prof. BAREGU yupo na Mchangiaji mwingine ni Prof Mbwiliza!
Polepole leo, ndipo anapotezwa vibaya..! Afu prof. Baregu na huyo gwiji mwingine prof. Bwiliza wanamwona HP km kidudu mtu..!

Maana mijamaa inaporomoka point kipolepole kinaongea kissm ujinga ukiwa na wasomi argue kisomi siyo kiitikadi..! Love these profs..!
 
Bw. Polepole anacompromise mjadala wakati wazee wanakaza nondo anaruka huku mara kule kifupi analeta ukatibu uenezi Wake
 
Naangalia kipima joto hapa, Ndg. Pole Pole kawekwa katikati ya Proffesa Baregu na Proffesa mwingine hapa kuongelea miaka kumi na nane bila Baba wa Taifa, je misingi ya utaifa aliyoasisi inaenziwa!?

Ndg Pole Pole hapa anayoongea ki uhalisia hayaendani na Mada na amepwaya mbele ya wachangia Mada wengine.

Hili linaweza lisiwe kosa lake maana watu alionao sio level yake! Ni kosa la muandaa kipindi! Huwezi kumuweka Pole Pole katikati ya wazee tena maprofesa kujadili jambo! Huyu alitakiwa kukaa pembeni na kuwasikiliza kujifunza kutoka kwao
 
Mbona kwenye Tume ya Warioba hukushauri akae pembeni?!!
 
Back
Top Bottom