Kipimajoto ITV miaka 18 bila Baba wa Taifa; Je, misingi ya utaifa aliyosimamia inaenziwa na kuendelezwa

Kazi zake ni tatu tu
1. Kutetea chama
2.Kutetea chama popote
3.Kutetea chama popote kwa namna yoyote

Huwezi kutegemea mawazo mazuri kwa mjadala kama unadhani jukumu lako ni kutetea chama.
Nadhani ajifunze sasa kutofautisha masuala ya chama na masuala ya kitaifa
 
Heshima Kwenu,

Jana Ijumaa usiku kulikuwa na malumbano ya joja/mjadala juu ya Legacy ya Mwalimu JK Nyerere. Hoja ilikuwa 'Miaka 18 bila Nyerere, Je, Aliyoyasimamia Yanaenziwa na Kuendelezwa?Waalikwa walikuwa Prof.Mwesiga Baregu, Prof.Joseph Mbwiliza na Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Niliwasikiliza wachangiaji wote na bila shaka waliofuatilia waliona mjadala ulivyoendelea. Jambo la msingi ambalo nilijifunza ni kwamba, Nyerere alikuwa anasisitiza sana juu ya maendeleo ya watu, maendeleo endelevu pamoja na uzalendo, kwa maana yake halisi. Hakuwa shabiki wa maendeleo ya vitu.

Nyerere alijenga taasisi na miundombinu kwa ajili ya maendeleo ya watu. Kulikuwa na shule chache lakini zenye uwezo wa kutoa elimu bora, zipo mpaka leo ingawa zimechoka. Tulikuwa katika kumi bora ya literacy rate miaka ya sabini. Viwanda vilikuwepo mpaka vilivyo katika kundi la kuwezesha viwanda vingine, mfano Kilimanjaro Machine Tools. Reli ya Kati na TAZARA nk.

Kuna wakati Prof. Baregu alijadili kuhusu uwepo wa maadui watatu ambao waliainishwa kuwa ni kikwazo cha maendeleo ya Taifa, ujinga, umaskini na maradhi. Maadui hao bado wapo ingawa kuna mwingine ameongezeka. Adui hofu. Wanasiasa wamewageuza maadui watatu pamoja na mwingine mpya kuwa ajenda.

Polepole alihamaki. Alianza kumshambulia Prof. Baregu. Alielezea mafanikio ya awamu ya tano,akijaribu kwa kificho kumponda Mwalimu Nyerere na kujaribu kuelezea kuwa yale aliyoshindwa Nyerere, awamu ya tano ya Rais Magufuli inayatekeleza. Alielezea mambo kadhaa likiwemo kuhusu reli. Alisema reli itakayojengwa itakuwa na kasi ya kilometa 160 kwa saa. Hiyo ndiyo Legacy ya Mwalimu Nyerere kwa mtazamo wa Polepole.

Mjadala haukuwa wa kuvutia baada ya hapo kwa kuwa Polepole alitaka aendelee kuongea na kuwazuia Prof. Mbwiliza na Baregu kuongea. Alimlaumu Baregu kwa kuharibu vijana(kama mhadhiri).

Kuna mambo ya kuzingatia ukitaka kushiriki mjadala au kualika wasemaji wakuu.Jambo la msingi kuliko yote ni uwezo wa mwalikwa kuchangia mjadala.
Pili ni kiwango chake cha elimu au uwiano wa taaluma yake na mjadala uliopo kwa siku hiyo. Kwa jinsi mjadala ule ulivyokuwa, umri ulitakiwa uwe kigezo pia. Uelewa wa kisomi pamoja na kushuhudia kwa macho na kuyaishi aliyoyasimamia Mwalimu wakati akiwa hai ni muhimu sana. Umri wa Polepole(labda na elimu) haukufaa yeye kuitwa kujadili mada na wazee wahadhiri na wasomi wa kiwango cha profesa. Sikuona umuhimu wa Polepole kuwepo kwenye mjadala ule.Hakuutendea haki.

Ni vema viongozi na wazee wa CCM kuangalia mtu wa kumtuma kwenye mijadala mizito kama ile. Kinana angeweza kufaa zaidi au angeshindwa kwenda, Nape angechukua nafasi.

Chama kinajishusha hadhi kwa kutuma watu kwa kigezo cha ukada. Polepole anakijua chama kwa kiwango gani? Amekisaidiaje chama mpaka hapo kilipo?

Nawasilisha.
Hata mimi niliuangalia mkuu.Ni kweli Pole pole alipwaya sana.Ilionekana wazi kwamba uelewa wake wa mambo ya msingi wa evolution ya siasa za Tanzania ni mdogo sana, ukilinganisha na magwiji wa siasa za Tanzania kama Prof.Mbwiliza na Baregu.Ni kweli umri wa Polepole na experience yake katika chama vilionekana kuchangia kupwaya,ingawa udogo wa elimu yake na kutomfahamu Mwalimu first hand kulichangia pia.In summary, edge waliyokuwa nayo Baregu na Mbwiliza over Polepole ni kumfahamu first hand Mwalimu,umri wao,experience ya siasa za Tanzania na elimu zao.

Nilipenda comment ya Baregu kwamba maadui wa Watanzania leo wamekuwa mtaji wa wanasiasa,hii ni kweli na iko wazi.Comment hii ilionekana kumkera sana Polepole ni kweli,jambo ambalo nililitegemea for obvious reasons.

Finally because of the foregoing discussion,nakubaliana na wewe mkuu kwamba Polepole hakuwa mtu sahihi kwenye mjadala ule na wala sidhani kama Nape au Kinana wangefaa kama ulivyo-suggest.Bila shaka yeyote match ya Prof.Mbwiliza na Baregu ingekuwa Mzee Ngombale Mwiru.

Kwa ujumla ni kweli Polepole hakuutendea haki mjadala ule,badala ya ku-discuss legacy ya Mwalimu, yeye akawa ana discuss performance ya awamu ya tano!What an obvious mistake.
 
Hahahahah polepole juzi kwenye mjadala alikuwa kama kibaka furani hahah


Swissme
 
Lengo la mjadala ule halikuwa kutetea vyama ! Ni kujadili legacy ya mwalimu! Sio kila.wakati tunapojadili mambo kama wanawanchi tuingize itikadi za vyama! Kina polepole huku wakiitana " macombred" nyerere ni wa ccm ni hawa walimfananisha magufuli na nyerere
 
Alafu ana kambinu kake akiwa kwenye vyomba vya habari,ni kuzungumza endlessly yaani usipokuwa mjanja wa ku m interupt ili uongee kipindi kinaweza kuisha anamsifia tu mtukufu na CCM,kuna haja watangazaji wanaomwalika wawe wana mwambia kama wamemwalika akiw amevaa kofia gani,yaani wawe wanamwambia kabsa kuwa tumekualika kama mwanachi na mdau wa maendeleo tuu na sio kama msemaji wa chama
 
Polepole wa katiba mpya sio kabisa polepole wa itikadi na uenezi wa CCM.

Chama kimemcorrupt huyu kijana kabisa
 
Si vyema Polepole kutumia tactics za Cheapshots ( Vijembe) dhidi ya Wazee kama Mzee Baregu, kwa sababu mada ile haikuwa kufanya Propaganda za Kisiasa, ilikuwa ni kuzungumza Kwa " Muktadha wa Uongozi wa Mwalimu".

Sasa yeye Polepole anamshambulia Lissu kuwa ni Kibaraka wa Wezi wa Rasilimali zetu, mtu ambaye anaumwa anapigania uhai wake hospitali, hii naona kama ni insensitive!!!

Anadownplay tukio la Lissu kupigwa risasi eti mbona yalipotokea Kibiti watu hawakujadili au kuguswa sana kama ilivyo kwa Lissu. That was bad!!, haya mambo yanahusianaje na utawala wa mwalimu?.
 
Back
Top Bottom