Waheshimiwa, poleni na kazi ya kulijenga taifa letu ilhali mkiubomoa utaifa wetu!

Apr 8, 2023
26
17
"Poleni na kazi" Kauli hii ndiyo aghalabu ilikuwa ikitumiwa na mtu kuwapongeza ama kuwashajihisha kila awakutapo watu ama mtu kazini.

Na hata wakati mtu anapotoka kazini wale wenye kutaka kumpa faraja walikuwa wakimwambia pole na kazi; hata hivyo maneno kama ilivyo maumbo ya watu na vitu, hunyumbuka na ama kupoteza au kubadili sifa yake kwa kadri muda upitavyo, tukaambiwa tusiseme tena pole na kazi, bali Hongera na kazi hasa kwa vile kazi si adhabu. Binafsi naomba nikupeni waheshimiwa pole na kazi ya kulijenga taifa letu ilhali mkiubomoa utaifa wetu. Poleni na kazi.

Unauliza nasema nini? Pana wakati si muda mrefu sana, kulikuwa na maoni miongoni mwa wasemaji wa jamii yetu hoja kwamba kaya yetu ilikuwa na 'ombwe la uongozi' kwa upande mmoja huku upande wa pili ukijitapa kujenga 'uzalendo' miongoni mwa wanakaya; na hata kukawa na hoja ikiwa uzalendo ni kukosoa tu ama kusifia tu?

Binafsi nilifikiri (na ningali kufikiri) kwamba uzalendo ni zaidi ya mawili hayo; hata hivyo yote hayo yalikuwa katika zama ambazo wanaotutangulia wakilitusadikisha kuacha yote na kuamini hapa kwenye kaya yetu ni kazi tu, poleni na kazi.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kauli (kama ni mbiu ama mbinu amueni wenyewe) ilikuwa "Tuliahidi, tumetekeleza, tunasonga mbele" na hivyo haikushangaza basi wakati mlipotulali kwa kauli moja kusema "Kazi iendelee", na miye kwani najua nini!!? Poleni na kazi.

Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya uchumi, miradi ya kimkakati na hata kuzitimiza ndoto na maono ya wale waliokuwa kabla yetu kwenye kaya yetu hii, vyote vilikuja pamoja na juhudi na mikakati ya kuhakikisha wanakaya wanatiwa shime kuona na kuamini kwamba kaya yetu ilikuwa kwenye safari ya kujikomboa kiuchumi na ukombozi huo ungekuja kwa "vita vya kiuchumi" na kama wasemavyo watani zangu "bhita ni bhita murah".

Si ajabu kwamba leo wakati wanakaya wanaohoji nini kilitokea kwamba wakati uchumi wa dunia ukitandikwa na Korona, sisi tuliambiwa tumeingia 'uchumi wa kati wa chini' na hivyo wakati thamani ya dola ya Marekani inaonekana kupindukia shilingi 3000, wanakaya wanavuja jasho kwa kazi ngumu, lakini swali linabakia ikiwa ni kazi ya kujenga ama kubomoa? Hata hivyo, poleni na kazi.

Ujenzi wa Bwawa la Nyerere uliopaswa kumaliza tatizo sugu la umeme hapa kwetu na kufikia wananchi huko mitandaoni kuja na lugha "tanzagiza", ulitarajiwa kuwa sehemu ya gridi ya taifa mwishoni mwa 2021, tukasogeza mbele na sasa hatuna tarehe wala muda rasmi kwa vile "tuko kwenye hatua za umaliziaji" na tusitie shaka kazi inaendelea. Wote tujipongeze na kujipa pole na kazi.

Kupanda kwa gharama za maisha kutoka kule ambako kilo ya unga ilikwishafika shilingi 800 na sukari ikiwa 1800 hadi sasa ambapo bei ya sukari ni kati ya 3800 hadi 5000, kazi inaendelea na tuendelee kujipongeza na kujipa pole na kazi?

Nimemsikiza kwa umakini kwa kadri niwezavyo liwali mwenye dhamana na matumbo yetu, na kusema kweli nadhani analia hujuma. Analia kuhujumiwa na wafanyabishara na wenye viwanda na huenda hii ni moja ya dalili ya kushuka kwa ama uzalendo au utaifa wetu kwa taifa letu, na japo hiyo si hoja yangu leo, leo miye nakupeni tu pole na kazi; poleni na kazi.

Najiuliza, kama kumbe tulifahamu kupitia TMA kwamba mvua zitaathiri hali ya sukari, kuanzia mwezi wa kumi vibali vikatolewa kwa wafanyabishara ili tusiwe na shida tuliyo nayo sasa, na bado tuna shida kama ilivyo leo, tuwapeni hongera ama pole na kazi? Kwani kazi inapimwa kwa wingi wa jasho na muda wa kukaa shambani ama matokeo ya kazi? Haya, sijui lolote Nanga miye, poleni na kazi.

Najiuliza, ikiwa tuko hapa tulipo kwa sababu ya hujuma na liwali wetu anasema hatuna mwarobaini wala namna ya kuwashughulikia wahujumu na wasaliti wetu hawa mpaka atakapopeleka muswada bungeni mwezi wa sita, hii ni kusema mpaka wakati huo, tunabakia kuwa 'mateka' wa wahujumu hawa kwa vile hatuna 'mamlaka' ya kuwashughulikia kabisa, na hivyo wakati sisi wengine tunajenga, wahujumu wanabomoa na wote jasho linatutoka kwa vile kazi inaendelea? Poleni na kazi!

Kama tuliwapa vibali kwa ajili ya kuleta tani 100 wakatuletea asilimia kumi tu, wakati tunawapa vibali walituthibitishiaje uwezo wao wa kifedha, miundombinu na kadhalika katika kutimiza majukumu waliyoomba kuyafanya? Hizo "insentivu" tuliwagawia kama karanga bila kuwa na namna ya kuwashughulikia ikiwa watashindwa kutimiza makubaliano? Tumerejea kwenye miundombinu, mipango mikakati, upembuzi yakinifu na mengineyo? Midhali jasho linatoka kwa wingi, bila shaka kazi inaendelea, basi poleni na kazi.

Kama wana Wasambazaji wachache (mmoja kwa kila mikoa 11), walikuwa wanafanyaje wakati ule hatukuwa na uhaba na sasa wanafanyaj!? Je! Yawezekana shida siyo idadi ya wasambazaji kama ambavyo madaraja yalikuwa yanavunjika na kukaa bila kujengwa kwa miaka mitatu, halafu tukaanza kuona madaraja yanavunjika na kujengwa kwa wiki mbili na kisha kazi inaendelea?

Kilichopungua ama kukosekana ni nini hapa? Haya, ebu nisikuchosheni kwa Ubananga wangu huu, nasema midhali wote tunahema kwa nguvu na jasho linavuja, bila shaka kazi inaendelea na hivyo poleni na kazi!

Bado unauliza nasema nini? Hata miye sijui, nawaza tu kibanangabananga na hizi ni salaam tu nawasalimia!
 
"Poleni na kazi" Kauli hii ndiyo aghalabu ilikuwa ikitumiwa na mtu kuwapongeza ama kuwashajihisha kila awakutapo watu ama mtu kazini. Na hata wakati mtu anapotoka kazini wale wenye kutaka kumpa faraja walikuwa wakimwambia pole na kazi; hata hivyo maneno kama ilivyo maumbo ya watu na vitu, hunyumbuka na ama kupoteza au kubadili sifa yake kwa kadri muda upitavyo, tukaambiwa tusiseme tena pole na kazi, bali Hongera na kazi hasa kwa vile kazi si adhabu. Binafsi naomba nikupeni waheshimiwa pole na kazi ya kulijenga taifa letu ilhali mkiubomoa utaifa wetu. Poleni na kazi.

Unauliza nasema nini!!? Pana wakati si muda mrefu sana, kulikuwa na maoni miongoni mwa wasemaji wa jamii yetu hoja kwamba kaya yetu ilikuwa na 'ombwe la uongozi' kwa upande mmoja huku upande wa pili ukijitapa kujenga 'uzalendo' miongoni mwa wanakaya; na hata kukawa na hoja ikiwa uzalendo ni kukosoa tu ama kusifia tu!? Binafsi nilifikiri (na ningali kufikiri) kwamba uzalendo ni zaidi ya mawili hayo; hata hivyo yote hayo yalikuwa katika zama ambazo wanaotutangulia wakilitusadikisha kuacha yote na kuamini hapa kwenye kaya yetu ni kazi tu, poleni na kazi.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 kauli (kama ni mbiu ama mbinu amueni wenyewe) ilikuwa "Tuliahidi, tumetekeleza, tunasonga mbele" na hivyo haikushangaza basi wakati mlipotulali kwa kauli moja kusema "Kazi iendelee", na miye kwani najua nini!!? Poleni na kazi.

Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya uchumi, miradi ya kimkakati na hata kuzitimiza ndoto na maono ya wale waliokuwa kabla yetu kwenye kaya yetu hii, vyote vilikuja pamoja na juhudi na mikakati ya kuhakikisha wanakaya wanatiwa shime kuona na kuamini kwamba kaya yetu ilikuwa kwenye safari ya kujikomboa kiuchumi na ukombozi huo ungekuja kwa "vita vya kiuchumi" na kama wasemavyo watani zangu "bhita ni bhita murah", si ajabu kwamba leo wakati wanakaya wanaohoji nini kilitokea kwamba wakati uchumi wa dunia ukitandikwa na Korona, sisi tuliambiwa tumeingia 'uchumi wa kati wa chini' na hivyo wakati thamani ya dola ya Marekani inaonekana kupindukia shilingi 3000, wanakaya wanavuja jasho kwa kazi ngumu, lakini swali linabakia ikiwa ni kazi ya kujenga ama kubomoa!!? Hata hivyo, poleni na kazi.

Ujenzi wa Bwawa la Nyerere uliopaswa kumaliza tatizo sugu la umeme hapa kwetu na kufikia wananchi huko mitandaoni kuja na lugha "tanzagiza", ulitarajiwa kuwa sehemu ya gridi ya taifa mwishoni mwa 2021, tukasogeza mbele na sasa hatuna tarehe wala muda rasmi kwa vile "tuko kwenye hatua za umaliziaji" na tusitie shaka kazi inaendelea. Wote tujipongeze na kujipa pole na kazi.

Kupanda kwa gharama za maisha kutoka kule ambako kilo ya unga ilikwishafika shilingi 800 na sukari ikiwa 1800 hadi sasa ambapo bei ya sukari ni kati ya 3800 hadi 5000, kazi inaendelea na tuendelee kujipongeza na kujipa pole na kazi!!?

Nimemsikiza kwa umakini kwa kadri niwezavyo liwali mwenye dhamana na matumbo yetu, na kusema kweli nadhani analia hujuma. Analia kuhujumiwa na wafanyabishara na wenye viwanda na huenda hii ni moja ya dalili ya kushuka kwa ama uzalendo au utaifa wetu kwa taifa letu, na japo hiyo si hoja yangu leo, leo miye nakupeni tu pole na kazi; poleni na kazi.

Najiuliza, kama kumbe tulifahamu kupitia TMA kwamba mvua zitaathiri hali ya sukari, kuanzia mwezi wa kumi vibali vikatolewa kwa wafanyabishara ili tusiwe na shida tuliyo nayo sasa, na bado tuna shida kama ilivyo leo, tuwapeni hongera ama pole na kazi!!? Kwani kazi inapimwa kwa wingi wa jasho na muda wa kukaa shambani ama matokeo ya kazi!!? Haya, sijui lolote Nanga miye, poleni na kazi.

Najiuliza, ikiwa tuko hapa tulipo kwa sababu ya hujuma na liwali wetu anasema hatuna mwarobaini wala namna ya kuwashughulikia wahujumu na wasaliti wetu hawa mpaka atakapopeleka muswada bungeni mwezi wa sita, hii ni kusema mpaka wakati huo, tunabakia kuwa 'mateka' wa wahujumu hawa kwa vile hatuna 'mamlaka' ya kuwashughulikia kabisa, na hivyo wakati sisi wengine tunajenga, wahujumu wanabomoa na wote jasho linatutoka kwa vile kazi inaendelea!!? Poleni na kazi!

Kama tuliwapa vibali kwa ajili ya kuleta tani 100 wakatuletea asilimia kumi tu, wakati tunawapa vibali walituthibitishiaje uwezo wao wa kifedha, miundombinu na kadhalika katika kutimiza majukumu waliyoomba kuyafanya!!? Hizo "insentivu" tuliwagawia kama karanga bila kuwa na namna ya kuwashughulikia ikiwa watashindwa kutimiza makubaliano!!? Tumerejea kwenye miundombinu, mipango mikakati, upembuzi yakinifu na mengineyo!!? Midhali jasho linatoka kwa wingi, bila shaka kazi inaendelea, basi poleni na kazi.

Kama wana Wasambazaji wachache (mmoja kwa kila mikoa 11), walikuwa wanafanyaje wakati ule hatukuwa na uhaba na sasa wanafanyaje!!? Je! Yawezekana shida siyo idadi ya wasambazaji kama ambavyo madaraja yalikuwa yanavunjika na kukaa bila kujengwa kwa miaka mitatu, halafu tukaanza kuona madaraja yanavunjika na kujengwa kwa wiki mbili na kisha kazi inaendelea!!? Kilichopungua ama kukosekana ni nini hapa!!? Haya, ebu nisikuchosheni kwa Ubananga wangu huu, nasema midhali wote tunahema kwa nguvu na jasho linavuja, bila shaka kazi inaendelea na hivyo poleni na kazi!

Bado unauliza nasema nini!!? Hata miye sijui, nawaza tu kibanangabananga na hizi ni salaam tu nawasalimia!
Poleni kwa kazi ni kauli ya kivivu, ikome! Hongereni kwa kazi...!
 
Eaaaaaaaaasy...;

Tufanye hivi kama taifa:

Pole na kazi wapewe wanawake wakitoka kazini

Hongera na kazi wapewe wanaume wakitoka kazini

From me: private consultant of the nation
 
Inakomaje? Pole na kazi, pole kwa uchovu wa majukumu ya kazi. Ina uvivu gani?
Huwezi ukasikia 'pole kwa kazi' kwa wazungu katika tafsiri yoyote; watakuambia great job, yaani kazi nzuri umefanya, congratulations, yaani hongera, lakini sio sorry for your job!, unaelewa sio?
 
Huwezi ukasikia 'pole kwa kazi' kwa wazungu katika tafsiri yoyote; watakuambia great job, yaani kazi nzuri umefanya, congratulations, yaani hongera, lakini sio sorry for your job!, unaelewa sio?
Usitafasiri kila kitu. Utapotea
 
Huwezi ukasikia 'pole kwa kazi' kwa wazungu katika tafsiri yoyote; watakuambia great job, yaani kazi nzuri umefanya, congratulations, yaani hongera, lakini sio sorry for your job!, unaelewa sio?
Wazungu wanatumia pia Sorry wanapomaanisha samahani kama wanavyomaanisha pole. Sisi tunatumia samahani wanapotumia Sorry. Lakini pia kwanini "Wazungu" wawe ndiyo kipimo cha ubora wa utumizi wa lugha yetu!!? Kwanini wasiwe Wahindi, Waarabu na hata Wachina!!? Au ndiyo bado ukoloni haujesha vichwani!!?
 
Wazungu wanatumia pia Sorry wanapomaanisha samahani kama wanavyomaanisha pole. Sisi tunatumia samahani wanapotumia Sorry. Lakini pia kwanini "Wazungu" wawe ndiyo kipimo cha ubora wa utumizi wa lugha yetu!!? Kwanini wasiwe Wahindi, Waarabu na hata Wachina!!? Au ndiyo bado ukoloni haujesha vichwani!!?
Ukoloni utaisha tutakapokuwa na vitu tulivyovitengeneza wenyewe kama magari, computer, simu, uchumi mkubwa na usio tegemezi kwa wageni.
 
Ukoloni utaisha tutakapokuwa na vitu tulivyovitengeneza wenyewe kama magari, computer, simu, uchumi mkubwa na usio tegemezi kwa wageni.
Hakuna jamii ama mtu kwenye maisha asiyetegemea mtu ama jamii nyingine. Hata mwajiri anategemea mwajiriwa.
 
Back
Top Bottom