auferet dominus
JF-Expert Member
- Jul 18, 2017
- 1,804
- 1,294
kama unazungumzia shughuli inayofanana na kutoa tamko kwa siku zile ni wanaume tu ndio waliokuwa wakifanya hiyo. hata hivyo neno la Mungu katika King James Version iliyotoka katika lugha za kwanza za Biblia linasema brothers katika mafungu yote niliyompa ndugu yako Jiwe la majiwe, hakuna undugu wa udada au ushangazi hapo. ni brazaz. usilete porojo yako hapa kwamba brazaz ininclude na wakina dada. hata kama unatolea mfano tu huu haufai.Kwanza neno Ndugu ni jumuishi( wale wote wa ukoo wako ni ndugu zako) kwahiyo Dada, Kaka,Mjomba,Shangazi,Binamu na kadhalika wote ni ndugu. Hivyo basi chukulia umetokea msiba wa Bwana John na MC atangaze" ndugu zake marehemu waje kutoa neno" Je tutategemea watu gani wajitokeze?.
hili hasa ndilo linalosema kuwa Yesu alikuwa wa kwanza kuzaliwa toka tumbo la mariamu kabla wakina yakobo hawajazaliwa.Pili biblia hajaelezea familia ya Yesu kwamba ilikuwa ya watu zaidi ya 3 yaaani Maria, Yosefu na Yesu inaonesha mwanzo mwisho walikuwa wakiisha watu watatu tu mpaka Yesu anaanza kuhubiri.
Excellent!Kwa Ayo machache tuna hakika pasipo shaka kuwa Yesu mpaka anafikisha miaka 12 hakuwa na Mdogo wake au Kaka yake aliyezaliwa na Mama yake.
hapa sasa ndio umelisha watu upupu. umejifanya mjanja kuchukua mafungu mawili tu ya ufunuo yanayofit purpose yako ya kudanganya watu kuwa mwanamke anayezungumzwa hapa ni maria. sasa kipande cha mwisho cha ufunuo 12:6 kinakuanika kizungumzia habari ya siku 2300. sijui hata kama unajua hizi siku ni kitu gani.Ufunuo 12:5-6. (5 Naye akazaa mtoto mwanaume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata hata kwa mungu...........! 6: Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo anamahali palipotengenezwa na mungu,............!). Haya maono ya Yohane yanaonesha huyo mwanamke anazaa mtoto mmoja mwanaume ana baada ya huyo mtoto kunyakuliwa( kupalizwa) na yeye huyo mwanamke anaifadhiwa nyikani palipoandaliwa na Mungu, hivyo basi kwenye maono haioneshi huyo mwanamke akizaa watoto wengine. Labda Tuangalie tena hapohapo mstari wa 17. Inaonekana yule Joka baada ya kumshindwa yule mwanamke anarudi kupambana na Wazao wake waliosalia wale wenyeshuhuda juu ya Yesu kristo. Ukiangalia hapo utaona mwandishi wanafunzi wake Yesu wote( ambao ndo wenye Shuhuda juu Yesu kristo) akiwaita Uzao wa Maria maana hata Yesu aliwaita ndugu zake.
Kwa hayo machache nawasilisha!
ok tuendelee sasa unataka kutuambia ni maria aliyekimbilia nyikani? wapi ulisoma kuwa alikimbilia nyikani maria wakati maria aliishi nyumbani kwa yohana baada ya kuondoka Yesu. kwa yohana ndio nyikani. historia imerekodi kuwa maria aliishi kama miaka 11 baada ya Yesu kuondoka kwa hiyo alikufa kama 41AD. huko kaburini ndio nyikani?
wakati Paulo alipokwenda yerusalem kumtembelea petro alikaa huko siku 15. hakumwona mtume yeyote huko Kasoro yakobo nduguye Bwana (Yesu) (Mdo 1:18,19). haya yote yanasema Yesu alikuwa na wazaliwa wenzake wa tumbo moja wewe.
kwanza ukilichukua hili fungu la 17 la ufunuo 12 ndio likusaidie kudefend hoja yako kuwa maria alikuwa bikira mpaka alipokufa au sijui alipopaa litakuumbua kwa sababu linasema hivi joka akarudi kupambana "uzao" wale waliosalia. sasa huo uzao atakuwa aliupataje kama sio kwa kuzaa watoto baada ya Yesu.Labda Tuangalie tena hapohapo mstari wa 17. Inaonekana yule Joka baada ya kumshindwa yule mwanamke anarudi kupambana na Wazao wake waliosalia wale wenyeshuhuda juu ya Yesu kristo.
Nakushauri hili fungu liache halihusiani na bikira maria. maria kafa, yuko kaburini. ipo tu account kuwa naye hakuwa anaamini kuwa mtoto wake ndie masihi mpaka alipofufuka. hilo kuamini japo very late hilo ndio linaweza kumuokoa na hukumu ya mwanakondoo.
umeleta jambo interesting hapa linalosema kuwa wazao wake waliosalia wale wanaoshika amri za Mungu na wenye ushuhuda wa Yesu ingawa pale kwenye kushika amri za Mungu ulipakwepa. Unafahamu vizuri wewe unachokizungumza?
haya njoo wewe na mwenzio jiwe tuzungumze. BTW otorongongo anakaa mtaa gani siku hizi. amepona wazimu wake?