Katumbasongwe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2018
- 1,017
- 1,149
Is just a fear of unknown, fanya likupendezalo na lisilo kinyume cha sheria za nchi yako. Kwani wewe ni msabato?-Hodi, wasalaam wanajamvi!
Mkuu mafundisho ya wasabato mara nyingi ni ya kimwili kuliko kiroho!
Mara 'ubatizo wa maji madogo huendi mbinguni'! kwani lengo hasa la ubatizo ninini?
'Mnywa pombe haendi mbinguni', ebo! mbinguni tunakwenda kwa usafi wa mioyo yetu ati!
'Kula nguruwe huendi mbinguni'! basi mbinguni mliundiwa nyie? acheni kuhukumu wengine, tafakarini matendo na njia zenu!
Una maanisha muislaam anaweza fuga nguruwe kwa ajili ya ujasiliamali? Si dhani kama ni sawa. Hawa wasabato tuwaweke ktk mabanoFwatilia vizuri utazidi kuelewa! Hata hivyo sidhani kua ngurue yupo kwenye kundi la nyama nyeupe, kuhusu ujasieiamali hayo ni mafundisho ambayo yapo na hata kwa dini zote na ambao hawana dini kujikwamua kiuchumi, na moja ya mafindisho ya Afya si kwa wasabato tu, hata vitabu na madactari watakuambia nyama nyekundu si nzuri kiafya ila hawajakukataza kula, ila lazima mafundisho yawepo
Una maanisha muislaam anaweza fuga nguruwe kwa ajili ya ujasiliamali? Si dhani kama ni sawa. Hawa wasabato tuwaweke ktk mabano
Huwa wananichanganya sana unakuta msabato ni mlevi anakwambia mdudu ni haramu lakini pombe anakunywa,
WAACHE UNAFIKI
Kuna mambo mengi sana watu kwa kutosikiliza vizuri na kuelewa huwafanya watu wasiwaelewe Wasabato,pia kuna wale wanaosikiliza ili kupata cha kukosoa tu,hawa hawasikilizi ili wajifunze,bali wapate upenyo wa kukosoa.Nielezee kidogo vitu vingi ambavyo watu hudhani wasabato wakisema usivitumie,watu hudhani wasabato wanavikaza kabisa
Watu wengi ukikutana nao ukawaambia mimi Msabato,atakuuliza kwanini hamnywi cocacola,chai.Kwanini hamli nyama,lakini hawaulizi hata kidogo kwanini hamnywi pombe?
Leo wote msio wasabato na mlio wasabato lakini mnapotosha mambo haya kwa makusudi ama ili kuonekana mnashika sana imani au kwa uvivu wa kujifunza vizuri na kwa undani zaidi,Kwa msimamao wa Kanisa na mafundisho yake kunywa Chai, kahawa,cocacola, pepsi,na soda zote kwa aina zake,na kula nyama isipokuwa zilizo zuiliwa kwa mujibu wa kitabu cha WALAWI siyo dhambi hata kidogo.Kwenye kanisa haya yote huitwa Mashauri ya afya ukipenda sema mafundisho ya afya na kiasi. Nimafundisho yanayoelezea madhara ya vitu vinavyounda hiyo cocacola hadi ionekane ilivyo,kwahiyo hata unapotumia utumie ukijua madhara yake mwilini,na ikiwa mwili wako ni hekalu , je unaona ni sahihi kuingiza vitu vinavyoudhuru hekalu?
Wasabato hawafundishi kuwa ukitumia hivi vitu hutaurithi uzima wa milele la hasha,bali kipimo ch kurithi uzima wa milele ni AMRI KUMI ZA MUNGU,ndio kipimo pekee cha DHAMBI.Bahati ni kuwa wasabato hivi vitu tulifundishwa mapema kabla ujio wa teknolojia ambayo sasa inawezesha watu kutafuta habari wenyewe kwenye.Ukiachilia mbali wasabato kufundisha haya mambo ya ubaya wa hivi vitu.leo hii kuna maelfu ya watu wasio wasabato wanaeleze ubaya wa madhara ya soda kwa aina zake na vinywaji vingi tena kwasababu za kitabibu na kiutafiti,na wengine walifanya utafiti ili kuthibitisha kinachosemwa na wasabato au kutafuta sababu za kuwakosoa wakaishia kuthibitisha madhara ya vitu hivi.Leo hii machapisho mengi yanayo eleza juu ya madhara ya hivi vitu unayoweza kuyapata kwenye mitandao, mengi siyo ya wasabato ni ya watu wa madhehebu mengine ya kiKristo, na hata dini zingine,na pia wasio na dini.
Kwahiyo Wasabato hawajawahi kumzuia muumini wao kunywa soda ama juisi ya viwandani bali hufundisha madhara ya hivyo vitu ili ukiamua kutumia au kutotumia iwe juu yako mwenyewe.Uwe kama daktari anayemwambia mgonjwa wake madhara ya sigara na pombe kitabibu huku yeye mwenyewe anatumia hivyo vitu.Ndio maana hata kwenye sherehe za Wasabato utakuta Soda kwa aina zake na juisi kwa aina zake.
Kwa wale ambao ukosoaji wao juu ya Wasabato huegemea kwenye mafundisho haya,ni wadhaifu wa kujifunza na hutoa hoja kondefu sana.
Mayai sio ya kisasa ni kienyeji.Nimepata muda wa kufuatilia mahubiri ya maisha hatimaye yanayorushwa mubashara kutoka Mbeya Tanzania. Nimejiuliza mnataka tufanye nini ikiwa mafundisho yenu yana msigano unaochanganya watu.
Mmoja wenu amekuwa akifundisha kitu kinachoitwa ujasiriamali. Moja ya mafundisho ni ufugaji wa ng'ombe wa nyama na maziwa, pamoja na kuku wa mayai. Maana yake ni kwamba, watu wanahitaji mayai, maziwa na nyama.
Leo namsikia mhubiri akisema ogopa sana mayai! Mafuta ambayo hata kwenye maziwa yamo mengi sana! Pia akaenda zaidi kusema ogopa hasa nyama nyekundu. Nguruwe ni haramu lakini ni kati ya wanyama wenye nyama nyeupe!
Sasa tufanye nini! Tufuge kuku wa mayai kwa ajili ya kuuzia wengine huku sisi tukiyakwepa ama tuache kwa vile mayai ni hatari kama ulivyosema?