kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,633
- 7,021
Nimepata muda wa kufuatilia mahubiri ya maisha hatimaye yanayorushwa mubashara kutoka Mbeya Tanzania. Nimejiuliza mnataka tufanye nini ikiwa mafundisho yenu yana msigano unaochanganya watu.
Mmoja wenu amekuwa akifundisha kitu kinachoitwa ujasiriamali. Moja ya mafundisho ni ufugaji wa ng'ombe wa nyama na maziwa, pamoja na kuku wa mayai. Maana yake ni kwamba, watu wanahitaji mayai, maziwa na nyama.
Leo namsikia mhubiri akisema ogopa sana mayai! Mafuta ambayo hata kwenye maziwa yamo mengi sana! Pia akaenda zaidi kusema ogopa hasa nyama nyekundu. Nguruwe ni haramu lakini ni kati ya wanyama wenye nyama nyeupe!
Sasa tufanye nini! Tufuge kuku wa mayai kwa ajili ya kuuzia wengine huku sisi tukiyakwepa ama tuache kwa vile mayai ni hatari kama ulivyosema?