Kipi tufanye Wasabato mnatuchanganya!

Kipi tufanye Wasabato mnatuchanganya!

Nimepata muda wa kufuatilia mahubiri ya maisha hatimaye yanayorushwa mubashara kutoka Mbeya Tanzania.Nimejiuliza mnataka tufanye nini ikiwa mafundisho yenu yana msigano unaochanganya watu.

Mmoja wenu amekuwa akifundisha kitu kinachoitwa ujasiria mali.Moja ya mafundisho ni ufugaji wa ng'ombe wa nyama na maziwa,pamoja na kuku wa mayai.Maana yake ni kwamba,watu wanahitaji mayai,na maziwa na nyama.

Leo namsikia mhubiri akisema ogopa sana mayai! Mafuta ambayo hata kwenye maziwa yamo mengi sana!Pia akaenda zaidi kusema ogopa hasa nyama nyekundu.Nguruwe ni haram lakini ni kati ya wanyama wenye nyama nyeupe!
Sasa tufanye nini!Tufuge kuku wa mayai kwa ajili ya kuuzia wengine huku sisi tukiyakwepa ama tuache kwa vile mayai ni hatari kama ulivyosema?
kila chakula alichoruhu Mungu kula we kula lakini kwa kila jambo kiasi kinhitajika, uzuri ni kwamba hiyo ishu ya mayai hata mi sikuwa mbali nilikuwa nasikia, hakusema tusile, ila alitoa tahadhali kwa ulaji uliopitializa.
Haya tuje kwenye afya, kile kiini cha ndani cha yai kina mafuta mengi ambayo hayafai kwa afya huwa yanaganda kwenye mishipa ya damu kwa ndani, hivyo kwa ushauri zaidi wale tunaopenda mayai, yai moja kwa siku inatosha sana tena sana tena la kuchemsha.

Nyama nyekundu hakuna daktari asiyejua madhara ya hizi nyama ndio hivyo mi mwenyewe ni mlaji mzuri tu. Tuzoee kula samaki na kuku tena hapo kwenye kuku tuwe tunaondoa ile ngozi ya nje ili kupunguza mafuta masiyofaa mwilini..

kufuga fuga kupata kipato, na kama qaona kacha nyama huwezi kula sana tu maadam sio dhambi, hayo mayai kama kupunguza huwezi kula sana tu maadam sio dhambi, ila kujali afya pia ni kitu cha msingi
 
Endelea kufuatilia hayo mafundisho., fungua akili yako... sambamba na kutofautisha baina ya mafundisho ya uimara wa kiroho; kiafya na kiuchumi. Kila kitu kina kiasi chake; wakati wake na mahali pake.
 
Hahaha hawa wasabato hata akija mungu wa wote watamkataa, kwa ubinafsi wao watataka mungu wao peke yao. Wao hujiona ni special na mbingu ni yao peke yao, hata mungu wao ni tofauti na huyu wetu.

Sishanga, wakikwambia kuku wao ni tofauti na hawa kuku wengine, hata mayai wanayokula wao pia ni tofauti na mayai haya tunayokula sisi.

Wanataka wawe tofauti kwa kila kitu na binadamu wengine.
Siogopi kuwa tofauti,Ila naogopa kubaguliwa na binadamu mwenzangu kwa kigezo cha dini.
 
kila chakula alichoruhu Mungu kula we kula lakini kwa kila jambo kiasi kinhitajika,
Hakuna chakula Mungu amekataza watu kula....Hivyo vyakula vyote ili mradi si sumu wewe kula..

Cha muhimu ni kuwa na kiasi
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Babu aliniambia nisiwe na urafiki na daktari kila kitu anakwambia usitumie wakati kwake anakula na kuvimbiwa
 
Fwatilia vizuri utazidi kuelewa! Hata hivyo sidhani kua ngurue yupo kwenye kundi la nyama nyeupe, kuhusu ujasieiamali hayo ni mafundisho ambayo yapo na hata kwa dini zote na ambao hawana dini kujikwamua kiuchumi, na moja ya mafindisho ya Afya si kwa wasabato tu, hata vitabu na madactari watakuambia nyama nyekundu si nzuri kiafya ila hawajakukataza kula, ila lazima mafundisho yawepo
Maandiko yamejieleza wazi tuwatendee wenzetu kile ambacho tungependa sisi kutendewa. sasa kama mnakataza hivyo vyote kwanini tena mfuge kwaajili ya wengine? nyinyi mfuge mpate hela alafu wenzenu watumie waathirike? Hivi wasabato huwa mnajielewa au mnakwenda kwa hisia?
 
Hawa jamaa ni waongo wakubwa ukiwafuata huishi dunia hii hata wao karibia vyote wanavyojinadi ni vibaya wanagonga

1. Wanajifanya hawanywi cocacola lakini wanagonga mitaani kama kawa

2. Wanajifanya hawanywi chai ya majani ya chai ama kahawa na badala yake eti wanajanani gani dizain ambayo hayawezi kufanya kazi ya chai lakini wanazigonga tii kama kawa

3. Wanajifanya eti mdudu ni haramu lakini wanamgonga kimya kimya

4.Siku hizi wamekuwa ni waganga wa kienyeji na wanaibia watu wenye magonjwa sugu kwa kitu wanachokiita "SANITARIUM CLINIC" tena eti wana compyuta ambayo ukishika inatbaini magonjwa yoote mwilini. Utapeli mtupu wametajirika lakini watu wanaendelea kuteseka na magojwa yao
Yote uliyoyasema ni 100% alafu wanajitamba wao ni first class wakristo. mimi huwa nawashangaa sana. yaani kama huyo ndodi kitu anachowafanyia watanzania. hizo mbingu atakazoingia na mimi naamini lazima niingie. mwizi tapeli na kanisa linamsapoti kwa utapeli wake wala hawataki kujitenga nae wamemkumbatia kuwa ni tabibu kumbe bonge moja la tapeli. Usabato ni shida.
 
Hawa jamaa ni waongo wakubwa ukiwafuata huishi dunia hii hata wao karibia vyote wanavyojinadi ni vibaya wanagonga

1. Wanajifanya hawanywi cocacola lakini wanagonga mitaani kama kawa

2. Wanajifanya hawanywi chai ya majani ya chai ama kahawa na badala yake eti wanajanani gani dizain ambayo hayawezi kufanya kazi ya chai lakini wanazigonga tii kama kawa

3. Wanajifanya eti mdudu ni haramu lakini wanamgonga kimya kimya

4.Siku hizi wamekuwa ni waganga wa kienyeji na wanaibia watu wenye magonjwa sugu kwa kitu wanachokiita "SANITARIUM CLINIC" tena eti wana compyuta ambayo ukishika inatbaini magonjwa yoote mwilini. Utapeli mtupu wametajirika lakini watu wanaendelea kuteseka na magojwa yao
Apo kwenye 4 ni 100%.
Matapeli wengi wa mitishamba ni wasabato, wamewatapeli watu sana na dawa zao bila kupona.
 
Usiwapimie hao yaani hata ulaya wanakwenda bila visa.
Kumbe bado hujaelewa! Hata hujui tofauti ya wale waliotaka kwenda ulaya bila visa na waadventista wasabato (SDA) hua uwe unasoma soma na kujua mambo ndio useme,
 
Kumbe bado hujaelewa! Hata hujui tofauti ya wale waliotaka kwenda ulaya bila visa na waadventista wasabato (SDA) hua uwe unasoma soma na kujua mambo ndio useme,
Ndio wale wale kasoro tarehe
 
Huyu jamaa kweli tatizo ni akili yake na wala siyo wasabato. Tangu lini nguruwe akawa nyama nyeupe? Ni fungu gani kwenye biblia linakataza kula nyama nyekundu au maziwa na mayai? Vitu vingine siyo amri kumi za Mungu, bali ni ushauri wa kiafya, madaktari wote duniani wanajua kuwa ulaji wa red meat si salama kwa afya. Lakini za kuambiwa changanya na zako. Ni kiwango gani cha ulaji huo ni hatari kwa afya yako? Hakuna palipoelezwa. Wasabato hawakatazi kula nyama nyekundu bali ni ushauri wa kitaalam kama unaweza. Kama huwezi chapa nyama kwa kwenda mbele. Isipokuwa kama ilivyo kwa watu wa nje, kuna baadhi ya watu au kundi la watu wachache ambao sijui niwaite ni extremist ambao huchukulia mambo kila kitu kwa mrengo wa kulia. Hili kundi lipo kila dhehebu, iwe kwa waislamu, wakatoliki au walokole. Ni kundi hatari sana. Na watu wa nje wanapowaona wanadhani ndo wasabato au waislamu walivyo.

Hivi mnakumbuka kuna kundi lilishawahi kwenda airport wakijiandaa kupanda ndege kwenda kuhubiri ulaya bila visa wala pasport? Siyo Wasabato kama kanisa, bali ni kundi lililojitenga na kujiwekea mrengo flani wa kiimani, kundi ambalo hata ndani ya kanisa halitambuliwi, lakini huko nje wakajua ni wasabato. Ajabu kweli.
Lakini kumbuka nguruwe huyohuyo yuko kwenye kundi la wanyama wenye mafuta ambayo ni unsaturated fatty ,,na unsaturated fatty ndio inayoshauriwa na hao unaowaita 'madaktari' ingawaje si wao wanaoshauri bali ni wahudumu wa afya wote wanalifahamu hili,, so kwenye suala la kitifire njoo kivingine ueleweke na sio kuja na hoja ambazo hata wewe huelewi ulichoandika
 
Fuata Biblia inachosema. Hayo mengine yote ni ufafanuzi tu kwa wenye upeo mdogo.
 
Back
Top Bottom