Kipi Kinachoendelea nyuma ya michakato ya ajira katika Utumishi wa Umma?

Kipi Kinachoendelea nyuma ya michakato ya ajira katika Utumishi wa Umma?

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,506
Reaction score
2,898
Vijana wengi wamekuwa wakipitia msongo mkubwa wa mawazo wanao sababishiwa na hii sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa Umma na haya ni baadhi ya maswali wanayo jiuliza bila majibu

1; Inakuwaje nafasi za kazi zinatangazwa na watu wanajitokeza kufanya usaili lakini zoezi la kuwapangia vituo vya kazi linachukua muda mrefu zaidi ya miezi mitatu wengine Hadi mwaka mzima?
Kwa mfano Kuna nafasi za kazi zilitangazwa mwaka Jana mwezi October na usaili ukafanyika mwezi December lakini Hadi Leo hao watu hawajawahi kuitwa kazini.

2:Kwanini kunakuwa na utofauti wa idadi maswali na alama za ufauru kwenye usaili wa kada Moja?
Kwa mfano mwaka 2024 kada x waliitwa kwenye usaili na wakapimwa kwa maswali 25 na alama ya ufauru ilikuwa 65 lakini mwaka 2025 kada hiyo hiyo waliitwa kwenye usaili wakapewa maswali 50 na alama ya ufauru ikawa 75.

Je katka hili sekretarieti ya ajira Ile kauri mbiu yenu ya Haki, Ukweli, na Uwazi inafanyaje kazi?

3:Kwanini sekretarieti ya ajira wanaficha alama za usaili wa mahojiano na hawaweki wazi watu waliofaninikiwa kuwekwa kwenye database ili kuwapunguzia gharama vijana?

4;Inakuwaje Sekretarieti ya ajira wanawapangia kazi watu kwenye vituo ambavyo tayari vimejaa?

Je sekretarieti ya ajira hawana mawasiliano ya kujua ni sehemu ipi unahitaji mtumishi , mtu amesafiri kutoka mtwara anaenda kigoma lakini anafika anaambiwa nafasi zimejaa je hawaoni uchungu na vijana wa taifa hili?

Pia soma: Mfumo wa Ajira Tanzania: Ukiritimba unaodhoofisha Nguvu Kazi ya Taifa Na mustakabali wa vijana
 
Nadharia fikirishi:-

1.Hazina imekauka no ngumu kulipa mishahara ya waajiriwa wapya!

2.Ajira za spinning matukio ya kisiasa kupoza upepo was siasa za kipindi zinazovuma kwa kasi!!

Unaweza kuongezea mengineyo!
 
Ajira portal pasua kichwa..hujui oral ulipata ngapi? Hujui kama upo kwenye database? Hujui oral walichukua kuanzia alama ngapi? Sasa kwa hali hii kwanini vijana wasiiendelee kubet..Sishauri kubet..Mwanangu mpaka sasa haamini kama alichezea namba za viatu au yeboyebo kwenye oral maana hakubahatika kuitwa.
 
Ajira portal pasua kichwa..hujui oral ulipata ngapi? Hujui kama upo kwenye database? Hujui oral walichukua kuanzia alama ngapi? Sasa kwa hali hii kwanini vijana wasiiendelee kubet..Sishauri kubet..Mwanangu mpaka sasa haamini kama alichezea namba za viatu au yeboyebo kwenye oral maana hakubahatika kuitwa.
😂😂😂😂😂
 
Huu uzi ni wakipumbavu, na bila shaka umeanzishwa na mwalimu au hawa watu wa diploma za kuunga unga za afya
 
Nikupe siri moja: Ni vigumu sana mambo kwenda perfect kama unavyotaka; always, strategy nzuri ni wewe mwenyewe kujiminya ili uenee kwenye mfumo na sio kutaka mfumo ubadilike ili wewe uenee.
 
Back
Top Bottom