Kipi kiliwahi kukutokea ukajikuta unaanza kuongea peke yako?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Jana nimekutana na mwamba mmoja kavaa fresh tu na ukimtazamaunajua huyu anaelekea katika ofisi flani yenye hadhi au labda ni mtu mwenye mishe zake za kuelewekwa, lakini ajabu nikaona anaongea peke yake.

Awali wakati namkaribua sikutilia shaka sana hilo niliamini labda kuna kitu kaaa sikioni, si unajua tena siku hizi teknologia ipo juu, lakini haikuwa hivyo, alikuwa hajavaa kifaa chochote na tulipokaribiana nikiwa nimemtolea macho kwa ukaribu, akajishtukia akaacha kuongea.

Ni kama vile mwaba alikuwa kwenu kikao cha kwake mwenyewe kichwani.

Hii sio mara ya kwanza kutokea hali hiyo, hata mimi huwa inanitokea, hivi ni changamoto ya Afya ya Akili au maisha tu yanatupeleka puta.
 
Mkuu Usisahau ule utafiti uliosema Kati ya Watanzania wanne, mmoja ni kichaa.
Mtu kuongea peke yake ni dalili ya ukichaa!
Na kichaa siyo lazima aokote makopo!
Kila kunapokucha maisha yanazidi kuwa magumu ambayo yanaleta changamoto nyingi.
 
Over concentration tu, unazama kwenye jambo fulani mpaka unajikuta unaongea na kucheka au kusikitika mwenyewe.
 
Kwa mujibu wa Likudd wa Jamii Forums, kuna faida kubwa sana kwenye ubongo wa mtu pale mtu anapo ongea peke yake. Likudd wa Jamii Forums amesema hayo kupitia Ukurasa wake wa Facebook swali lililoulizwa kwenye page ya Facebook ya jamiiforums kuhusu sababu gani kuwafanya watu kuongea peke yao.
 
Attachments

  • Screenshot_20231112-184001.png
    Screenshot_20231112-184001.png
    55.5 KB · Views: 15
Jana nimekutana na mwamba mmoja kavaa fresh tu na ukimtazamaunajua huyu anaelekea katika ofisi flani yenye hadhi au labda ni mtu mwenye mishe zake za kuelewekwa, lakini ajabu nikaona anaongea peke yake.

Awali wakati namkaribua sikutilia shaka sana hilo niliamini labda kuna kitu kaaa sikioni, si unajua tena siku hizi teknologia ipo juu, lakini haikuwa hivyo, alikuwa hajavaa kifaa chochote na tulipokaribiana nikiwa nimemtolea macho kwa ukaribu, akajishtukia akaacha kuongea.

Ni kama vile mwaba alikuwa kwenu kikao cha kwake mwenyewe kichwani.

Hii sio mara ya kwanza kutokea hali hiyo, hata mimi huwa inanitokea, hivi ni changamoto ya Afya ya Akili au maisha tu yanatupeleka puta.
Kitendo cha kuacha kuongea baada ya wewe kumfikia, kinaonesha kuwa hakukuwa na tatizo
Alikuwa anafanya hivyo kwa makusudi na kwa manufaa yake.

Alikuwa ama anaaply kanuni ya kiimani au ya kiroho au ya Kisaikolojia.

Kama ni ya kiroho, basi alikuwa anaifanyisha imani yake kazi.

Na kama ni katika mtazamo wa Kisaikolojia, basi alikuwa anafanya kile kiitwacho AUTOSUGGESTION!
 
Kuna siku nilikuwa na father akiendesha gari hapa nilikuwa na age ya 10y. Namuona mzee anaongea peke yake mpaka akaanza kuugonga usukani🤣. Hapa ilibidi nimuulize mzee vipi tena baba mbona unaongea peke yako na unapika usukani?. Mzee aliniangalia na kutabasamu tu.

Hapa nilipo nafanya kama mzee sasa alivyofanya kuna siku najua mwanangu ataniuliza swali kama nililo muuliza father. Maisha hayana utani😂
 
Back
Top Bottom