Kipanya kalewa sifa na kukosa uzalendo sasa

Kipanya kalewa sifa na kukosa uzalendo sasa

kp26032014.jpg

kp25032014.jpg


kp17032014.jpg
kp24032014.jpg


kp18032014.jpg



kp20032014.jpg
kp28032014.jpg
 
usilaumu, ni njia nzuri ya kuwasilisha ujumbe kuonesha jinsi matotonya yanavyofanywa huko bungeni ilhali kodi zetu zinateketea. Ni uzalendo wa hali ya juu.
 
Umeelewa picha vibaya mkuu maana kwa mujibu wa picha kipanya kasikia tu hayo maneno sehemu na yeye anashangaa inakuwaje watu wanaroho za hadi kuwafikiria wenzao mauti
 
Mimi sio lakini madhara ya kupotea ndege yanajulikana ni kwamba wale watu walikufa kwa hiyo na hawa wabunge ina maana ni bora wafe kivile? Huu sio ubinadamu sasa
kupitia katiba wanayoitengeneza wanaweza kutengeneza maangamizi kwa taifa na mpasuko mkubwa na watu wakauwawa maelelfu. kwa kweli bora wafe wao na si kutengeneza kaburi kwa watu wasio na hatia kwa manufaa ya chama chao. nasema tena ile katuni imepeleka ujumbe mzito kwa viongozi wajinga. KATI YA KIPANYA NA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA NANI KALEWA SIFA? KAMA HAKILI HAZIKUTOSHI UTATUAMBIA NI KIPANYA KAMA UNAVYOSEMA. wale wabunge ni zaidi ya wachawi wanaotuona watanzania kama misukule. haiwezekani sisi wananchi kwa uwingi tukasema tunataka hiki alafu kwa upumbavuu wao wanasema hili chama hakitaki. kwani nchi hii ni ya CCM ama ya wananchi. KIPANYA NI MZALENDO SANA NA NINAMPONGEZA KWA UJUMBE HUO MZITO. SPIKA SI SPIKA YAANI NI UPUUZI TU.
 
Wahuni kama akina Masudi enzi zile za nyerere walikuwa hawaachwi watambe. Wamshukuru JKikwete anawachukulia poa tu.

tatizo watu hampendi ukweli na hasa ukiwa mchungu.kwahiyo ulitaka asifie tu hata kama hakuna cha maana kinachofanyika.
 
Katika katuni yake ya leo anasema "Hiyo ndege iliyopotea bora ingekuwa imebeba wajumbe wa bunge la Katiba".
Naamini hii ni kulewa sifa na kukosa ubinadamu kabisa. Siku zote napenda katuni zake lakini hii hapana!

tena siku ile Jk analihutubia.......ingekuwa safi sana!
 
Ndugu yangu hiyo ni lugha ya kifalsafa..iliyobeba ujumbe kuwa wabunge wa bunge la katiba wanachefua kwa kauli na matendo yao ambayo hayaonyeshi dhamira ya kutunga katiba mpya kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na wananchi.

Hata km ni lugha ya kifalsafa ni vizuri pia kufanya tathmini ya matokeo ya ile ndege iliyopotea na kushababisha maangamizi ya binadamu. Tunaongea kiurahisi kwa sababu hayajatukuta sisi! Anyway Watanzania ndivyo tulivyo!
 
Kipanya yuko sahihi tulipeleka bunge maalumu la katiba na wasipotuletea katiba ya wananchi adhabu yao ndio hiyo. Wanapindisha pindisha badala ya kujadili rasimu waliyopewa hata kama wanabadili wabadili katika mfumo ambao unakubalika na wananchi! Haya mambo ya mwamaba ngoma yatatufikisha pabaya na watakaoumia ni sisi sio hao wakubwa!
 
Ni mzalendo zaidi maana hawa wajumbe wa katiba ni watu wasiojali muda wala kodi zetu, ni utumwa kama hautawachukia
 
Hata km ni lugha ya kifalsafa ni vizuri pia kufanya tathmini ya matokeo ya ile ndege iliyopotea na kushababisha maangamizi ya binadamu. Tunaongea kiurahisi kwa sababu hayajatukuta sisi! Anyway Watanzania ndivyo tulivyo!

Wacha wabunge wote wateketee kwa moto, hawana faida yoyote ila wajue hayo ni maoni yetu sisi WENYE NCHI.
 
Nadhani umemwelewa kwa mtazamo huo ila mimi kwa upande wangu nimeelewa kua hayo ni maneno ya wananchi kupitia katuni hiyo na inaonyesha ni kiasi gani wananchi wamechoshwa na kukerwa na maigizo yanayoendelea bungeni huku kodi zetu zikiteketea.

Kwa hiyo mdau, nionavyo mimi, hayo si maneno ya Kipanya ila ni ya wananchi. Kipanya kayawasilisha tu.

Huu ni mtazamo wangu pia.

Ni kweli,kipanya amewakilisha maneno ya wananchi wanayosema mtaani.si kipanya ndo kasema.
 
Katika katuni yake ya leo anasema "Hiyo ndege iliyopotea bora ingekuwa imebeba wajumbe wa bunge la Katiba".
Naamini hii ni kulewa sifa na kukosa ubinadamu kabisa. Siku zote napenda katuni zake lakini hii hapana!

Mkuu you should have taken it literary not literally otherwise wewe ndiye unayeonekana kuwa sio mzalendo! Hebu iangalie vizuri hiyo katuni utaona hayo maneno yanasemwa ndani ya nyumba halafu kipanya mwenyewe anaguna tu. Mkuu fasihi hiyo inataka shule kuielewa!
 
Tatizo watu wanaimba uzalendo kama kasuku lakini hawajui maana yake. Mtu anaweza kuwa rais lakini akawa sio mzalendo.

hata ukiwa na mke au mume wako akienda upinzani au kusapoti upinzani c mzalendo!!!ccm bhana watatuambia hata kuchapiwa siri ya ndani eti mtu hana uzalendo kwa taifa
 
Katika katuni yake ya leo anasema "Hiyo ndege iliyopotea bora ingekuwa imebeba wajumbe wa bunge la Katiba".
Naamini hii ni kulewa sifa na kukosa ubinadamu kabisa. Siku zote napenda katuni zake lakini hii hapana!

hajakosea kabisa, na m/kiti wa ccm taifa angekuwamo pia maana hawataki tuwe na katiba ya kizalendo! hata wewe ungekuwemo poa tu!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom