Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 123,250
- 98,243
Jana Kingunge Ngombale Mwiru kada wa siku nyingi wa CCM na mmoja wa wazee wa zamani na muasisi wa chama hicho alipanda katika jukwaa la kampeni la Lowassa mmoja wa watia
nia na kusema kuwa amenusa harufu mbaya ndani ya CCM eti kuna mpango wa kamati kuu ya chama hicho kukata jina la Lowassa huku akidai ikiwa hilo litatokea basi 'patachimbika' na 'hawatakubali'
Kimsingi ni aibu kubwa kwa mzee ambaye ni miongoni mwa walezi wa chama kuonyesha mapenzi ya waziwazi kwa mgombea mmoja huku kukiwa na atagombea wengine wengi na mbaya zaidi yeye kama yeye kutoa kauli za vitisho kwa chombo cha maamuzi ambacho yeye siyo mmoja wao!
Leo Kingunge anataka kutuaminisha kuwa katika taifa hili yeye ndiye mwamuzi wa mwisho na mbaya zaidi akili yake hakuna wa kuipinga "huu ni ujinga"
Kingunge anataka kamati kuu ya CCM isikilize amri yake na sasa hakuna haja ya kikao chochote kile cha maamuzi kinachotakiwa kuketi kwani tayari Kingunge kashamaliza kazi na kutoa uamuzi ya kwamba fulani ndiye rais!
Kingunge alianza mwaka 2005 kwa kauli eti "Salim Ahamed Salim hatakuwa rais wa Tanzania mimi Kingunge ndiye nimesema" na hapo likaanza kuundwa zengwe lililoongozwa na Lowassa kumchafua Salim!
Juzi mkoani Arusha Kingunge alimtaka Kikwete akae na Lowassa eti 'wayamalize' ili kufanikisha mkataba waliowekeana.
Tofauti na miaka ya nyuma sasa Kingunge amemtaja waziwazi 'rais wake' na mbaya zaidi kutoa onyo kali kwa kamati kuu ya CCM ambayo ndiyo 'think tank' la CCM huku akijua kuwa mgombea wake mbali na kashfa alizonazo pia ni mchovu sana kiakili na kiafya kupewa nchi! Kama mtu ni mzuri hakuna haja ya kutumia nguvu na vitisho ili apite atapita tu!
Kingunge aelewe kuwa Tanzania siyo mali yake na kauli yake ni hatari kubwa kwa chama chake! Aache vyombo vya maamuzi vifanye yake bila ya kutishwa na kushurutishwa.
Kuna watu wanadhani kuwa wana hatimiliki ya CCM mfano Nimrod Mkono aliwahi kutoa kauli kama hii ya 'patachimbika' ila yeye ndiye aliishia kuomba radhi achilia mbali kukosa alichokitaka! Kingunge ni lazima aelewe kuwa kuna vigezo vitakavyotumika kumpitisha mgombea na asiye na sifa 'ATAKATWA' na kama 'PATACHIMBIKA' basi ni kwa upande wake na akichelewa kutambua atamalizika kabisa!
Hujui kuwa kingunge ndiye mwenye chama?