Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Anazeeka vibaya huyu mzee, kwahiyo akikatwa atachukua hatua gani labda!
 
kingunge hashinikizi uteuzi wa Lowassa ila anahitaji haki kutendeka kwa kuzingatia kura za maoni na sio kupitia maamuzi ya wachache wanaoamini katika kukata jina ili kumwondoa ulingoni,tatizo tunapenda kudanganywa tu lazima ukweli usemwe wazi na kuikosoa ccm sio dhambi ila mzee anakumbusha palipo dhaifu,hivo Lowassa aparekebishe.
TEAM lowassa
Hapana mkuu hakuna kura za maoni CCM huyu mzee wetu kaonjeshwa damu ya fedha Ubungo akili zimemruka, halafu kachagua zimwi likujualo maana ukianza na kura za maoni kwa mgombea Je, uwezo na sifa 13 za mgombea utaziweka wapi?

Mara zote chama huanza kumtafuta mgombea ambaye ataweza kusimamia utekelezaji wa ILANI yake kwanza, na hapo kuna kutazama uwezo na sifa zinazotakiwa. Hivyo mgombea unajipima kiuwezo na sifa hizo pindi unaposhauriwa, Ukisha jiaminisha unachukua fomu kwenda kutafuta wadhamini. Mgombea anapokwenda kwa wanachama wake kuomba dhamana ni utaratibu wa mwanzo kama alivyotakiwa kutoa mil. 1 kuchukua fomu. Lowassa hata kama angetoa billini 10 isingemaanisha lolote zaidi ya kwamba amelipa ada iliyotakiwa. Wagombea hawashindani nani atalipa zaidi ya wengine wala nani mwenye wadhamini wengi.

Wadhamini haswa humaanisha watu wanaokujua wewe vizuri na kwamba yote uloyaandika katika fomu hiyo ya maombi ni ya kweli na wao ni mashahidi. Sasa sijui kama hawa watu wote wanamjua Lowassa kivile pengine hata siku yake ya kuzaliwa hawaijui.. Unapopewa idadi ya wadhamini, kisha wewe ukaongeza wako zaidi haiongezi uzito wa kuaminiwa..tena basi sehemu nyingine ukimdhamini mgombea unaweza pigiwa simu ukaulizwa maswali juu ya mdhamana wako..

Kwa hiyo wagombea wote 40 watapimwa kutokana na uwezo na sifa zilizo ainishwa na chama kwanza, na kwa kila mmoja wao huwa na plan B ya kwamba kama jina langu litaenguliwa basi nitampa support mgombea fulani (kati ya watano bora) kwa sababu aidha mna mtazamo sawa juu ya dira na upeo hivyo ungependa kushirikiana naye katika serikali ijayo ama nawe unaingia hatua ya pili ya umaarufu wake utampa ushindi. Wanapobakia wagombea watano hapo sasa ndio mambo mengine nje ya chama yanapochukua nafasi..

Swala ya Umaarufu na mtu anayependwa huwa lipo NEC sio hatua ya kwanza ya kamati kuu. hapa inatazamwa bendera ya chama nani kati yao ataweza kuibeba. Umaarufu utaukuta NEC ambako sasa watu wanaonyesha jinsi gani mgombea fulani anakubalika ndani ya chama na Kitaifa.
 
Hawatakubali yeye na nani? Hajui enzi zake zimeisha? Huyu Mzee sasa hivi hajitambui na hafuati tena misingi aliyoamini.
Unauliza swali ambalo una majibu yake.Au wewe husomi na kuangalia alama za nyakati?Maelfu ya wanaomiminika kumlaki na kumdhamini,ndiyo wanaoitoa kauli hiyo kwamba hatutakubali jina lake kukatwa na si Kingunge.Yeye Kingunge anaiwakilisha sauti ya wengi,kwa hekima ya kisiasa,kama ujumbe wa kuwasaidia wale watakaofanya maamuzi.Ila naona mpo watu mnaokiombea hatima chama chetu kwa kutaka kiendeleze mifumo ya kidkiteta na si ya kidemokrasia.Demokrasia inakubali wengi wape sasa wewe unatakaje?
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar Ramadhan Madabida siku ya Jumamosi iliyopita akitoa salamu za wanachama wa CCM mkoa wa Dar wakati wa shamrashamra za ujio wa Lowassa kusaka wadhamini katika mbio za kutaka kuteuliwa kuwa mgombea urais wa CCM mwaka huu alisema, UADILIFU, UCHAPAKAZI NA KUPENDWA NA WATU WENGI KWA LOWASSA anamfananisha na Mtume Muhamad!!

Source:Gazeti la Mwananchi la Jana.

*Binafsi nimechukizwa sana na kauli hiyo, kwa kuwa ni kufuru tena ni kufuru kubwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kumfananisha na -----. Nitashangaa sana kama wanachama wa CCM mkoa wa Dar watakaa kimya kuhusu kauli chafu kama hii ikapita hivi.

CC Ritz
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom