Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

safisana kingunge CCM,haiwezi kumkata mtu eti kwa kigezo cha sio mwadilifu.ni nani aliye mwaminfu ccm.waliopanga kuliibia shirika la umeme kupitia escrow na kufanikisha mpaka wafadhili wakasitisha misada leo wanamshoonyeshea mkono Edo.kingunge hongera akikwatwa mtu lazima pachimbike
 
Hivi chadema wanatangaza mgombea lini?au wanasubiri masalia ya CCM

ukawa na wao wameniangusha mno kwani walishindwa kung'amua mtego mkubwa ambao ccm wamewafanyia ukiwa ni wa kimkakati haswa na mpaka waje kushtuka wazungu husema " it is too late ". unawaacha ccm watiririke tu kuchukua fomu huku vtombo vyote vya habari vikiwa navyo vimetekwa kwa kufanya agenda setting ambayo inawapa coverage ya kutosha ccm kama ccm na hao watangaza nia kwa kipindi cha miezi miwili na nusu unategemea nini? na hata kama ukawa watasema kuwa wanangojea ccm imtangaze mgombea ndiyo wao waanze kuamka bado haitawasaidia kivile kwani ninavyowajua ccm kwa mipango, mbinu na mikakati hata baada tu ya hiyo july 12, 2015 watahakikisha wanazidi kukamata airwaves zote za media hapa tanzania na kuzidi kukipa chama publicity kitu ambacho kitawasaidia kwa kiasi kikubwa tu. ukawa ile msemo wa wahenga wa " aliye juu mngoje chini " umewaangusha na utawaponza na badala yake mngeubadilisha huo msema na kuwa " aliyejuu mpandie huko huko ng'adu kwa ng'adu ". ushauri wa bure tu kama mtanzania mwema nisiye na upande nawashaurini ukawa sasa nguvu zenu nyingi ziwekeni kuchukua majimbo mengi ya ubunge ili muwe wengi bungeni kuzidi wabunge wa ccm na hapo nadhani mtakuwa na nguvu kubwa ya kuiwajibisha serikali na nchi itakaa sawa ila kwa upande wa nafasi ya urais nasikitika kusema kwamba " mtashindana tu lakini hamtashinda " na hii ni kutokana na mapungufu makubwa ya kimkakati mliyoyafanya.
 
Hakuna sababu ya El kukatwa ni woga tu wa wahafidhina wanaolinda masilahi yao ndani na nje ya Chama, Kwa kuwa wanajua vema El si mtu wa kuyumbishwa ovyo na si mwoga wa Kuamua jambo na kulisimamia ilpaswavyo tofauti kabisa na mwenyekiti wa Sasa anayemaliza Muda wake
 
watamkataje .kwa kigezo gani
hatukubali jembe letu likatwe
 
Nawaza kama watu wanaijuwa serikali, nawaza kama watanzania wanajuwa kuwa hili taifa linawatu na mataifa wanayo saidia ktk ulinzi na usalama. Hili ni taifa lenye heshima na dunia nzima wanajuwa haiwezekani na mpaka hata Yesu anarudi watu ama mtu kuingia ikulu kwa ajenda ama masilah binafsi bila mamlaka zilizopo kuchukua hatuwa. Kweli ni bora watu wakae kimya kumsubiri Rais ajaye pasipo kuapizana nani anajuwa kuwa Lowasa hakatwi jina?
 
kwa hili la kingunge simwamini tena lakini si la kushangaa sana kama mtu kumkata mungu na dini huu si wehu
 
Hatuwezi achia nchi iende kwa mafisadi miaka 20 mliyo wazurumu watz inatosha.hakuna reli wa air tz.mnataka malori yenu yabebe mizigo aibu kubwa hii
 
Aliisha onja raha ya ufisadi pale alipokuwa anakusanya ushuru stand ya ubungo sasa anamfagilia fisadi mwenziye kumkomoa Wariri mkuu Pinda aliyemfukuza stand hiyo kubwa nchini
 
Hapa ndio tutapojifunza. Kipi bora, kushika mpini au kushika jembe lenyewe.
 
Nawaza kama watu wanaijuwa serikali, nawaza kama watanzania wanajuwa kuwa hili taifa linawatu na mataifa wanayo saidia ktk ulinzi na usalama. Hili ni taifa lenye heshima na dunia nzima wanajuwa haiwezekani na mpaka hata Yesu anarudi watu ama mtu kuingia ikulu kwa ajenda ama masilah binafsi bila mamlaka zilizopo kuchukua hatuwa. Kweli ni bora watu wakae kimya kumsubiri Rais ajaye pasipo kuapizana nani anajuwa kuwa Lowasa hakatwi jina?

Hakuna wa kumkata jina lowasa
 
Hata asipokatwa, Wananchi tutamkata kwenye sanduku la kura, haiwezekani fisadi aende Ikulu.
 
Hakuna wa kumkata jina lowasa
CCM wakimshindwa, wapiga kura tutamkata tu, ikulu haendi Lowassa, nyie mnaopiga mpunga wake, pigeni tu ila mwisho wa siku muungane na sisi rusiopenda kununuliwa kumwadabisha.
 
Back
Top Bottom