Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Kingunge: Hatutokubali Lowassa akatwe jina

Huyo mzee anatumika kama chombo, badala ya kujua uzee ni dawa. Pole yake.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Kama lowasa akubali kukatwa nana atakubali kukatwa???
 
Hivi chadema wanatangaza mgombea lini?au wanasubiri masalia ya CCM
 
Nina mashaka na busara za huyu mzee inamaana kwakwe wakikatwa wengine sawa ila lowasa hapana.

Hili ndilo tatizo la kununuliwa uzeenu na mafisadi

muacheni mzee wa ili awe surprised bado ahamini kama enzi zake sad
sa zimebaki ni historia.... na uo ndo ukweli kaupata toka jikoni
 
Jana Kingunge Ngombale Mwiru kada wa siku nyingi wa CCM na mmoja wa wazee wa zamani na muasisi wa chama hicho alipanda katika jukwaa la kampeni la Lowassa mmoja wa watia nia na kusema kuwa amenusa harufu mbaya ndani ya CCM eti kuna mpango wa kamati kuu ya chama hicho kukata jina la Lowassa huku akidai ikiwa hilo litatokea basi 'patachimbika' na 'hawatakubali'

Kimsingi ni aibu kubwa kwa mzee ambaye ni miongoni mwa walezi wa chama kuonyesha mapenzi ya waziwazi kwa mgombea mmoja huku kukiwa na atagombea wengine wengi na mbaya zaidi yeye kama yeye kutoa kauli za vitisho kwa chombo cha maamuzi ambacho yeye siyo mmoja wao!

Leo Kingunge anataka kutuaminisha kuwa katika taifa hili yeye ndiye mwamuzi wa mwisho na mbaya zaidi akili yake hakuna wa kuipinga "huu ni ujinga"

Kingunge anataka kamati kuu ya CCM isikilize amri yake na sasa hakuna haja ya kikao chochote kile cha maamuzi kinachotakiwa kuketi kwani tayari Kingunge kashamaliza kazi na kutoa uamuzi ya kwamba fulani ndiye rais!

Kingunge alianza mwaka 2005 kwa kauli eti "Salim Ahamed Salim hatakuwa rais wa Tanzania mimi Kingunge ndiye nimesema" na hapo likaanza kuundwa zengwe lililoongozwa na Lowassa kumchafua Salim!

Juzi mkoani Arusha Kingunge alimtaka Kikwete akae na Lowassa eti 'wayamalize' ili kufanikisha mkataba waliowekeana.

Tofauti na miaka ya nyuma sasa Kingunge amemtaja waziwazi 'rais wake' na mbaya zaidi kutoa onyo kali kwa kamati kuu ya CCM ambayo ndiyo 'think tank' la CCM huku akijua kuwa mgombea wake mbali na kashfa alizonazo pia ni mchovu sana kiakili na kiafya kupewa nchi! Kama mtu ni mzuri hakuna haja ya kutumia nguvu na vitisho ili apite atapita tu!

Kingunge aelewe kuwa Tanzania siyo mali yake na kauli yake ni hatari kubwa kwa chama chake! Aache vyombo vya maamuzi vifanye yake bila ya kutishwa na kushurutishwa.

Kuna watu wanadhani kuwa wana hatimiliki ya CCM mfano Nimrod Mkono aliwahi kutoa kauli kama hii ya 'patachimbika' ila yeye ndiye aliishia kuomba radhi achilia mbali kukosa alichokitaka! Kingunge ni lazima aelewe kuwa kuna vigezo vitakavyotumika kumpitisha mgombea na asiye na sifa 'ATAKATWA' na kama 'PATACHIMBIKA' basi ni kwa upande wake na akichelewa kutambua atamalizika kabisa!
 
Kama lowasa akubali kukatwa nana atakubali kukatwa???

wazee hawa na watia nia wa ccm inabidi wawe makini sana na ndimi zao mbele ya jamii la sivyo muda mfupi kabla au baada ya uchaguzi tanzania inaweza kuwa uwanja wa vita na tusikubali tufikishwe huko wakuu. mara ccm itashinda hata kwa goli la maradona na mara tena mzee na kada mkubwa tu wa chama nae anasema kuwa hawatubali mtu wao akatwe. hapa anataka kutuandaa vipi watanzania kisaikolojia?
 
haa haa mkuu kingunge ni kilongola tu aliyejitoa mhanga kumsemea lowasa na wenzake. nyuma yake wako wanaccm wengi waliotekwa na lowsa...

Kwa nini awe yeye na sio wengine??!!
Immunity hiyo inatika wapi na imejengeka juu ya nini mkuu??!!
 
wazee hawa na watia nia wa ccm inabidi wawe makini sana na ndimi zao mbele ya jamii la sivyo muda mfupi kabla au baada ya uchaguzi tanzania inaweza kuwa uwanja wa vita na tusikubali tufikishwe huko wakuu. mara ccm itashinda hata kwa goli la maradona na mara tena mzee na kada mkubwa tu wa chama nae anasema kuwa hawatubali mtu wao akatwe. hapa anataka kutuandaa vipi watanzania kisaikolojia?

Ndipo hapo mkuu...ikulu hawawez kwenda wote 40 but unatakiwa mmoja...sasa ulisema maneno yasiyokuwa na fikra kama hayo nn maana yake..asikusumbue by da way sasa ni zamu ya ukawa ccm wamechoka
 
Wamekijenga na sasa wanakibomoa . . . . . . .wanasema kila siku chama kina wenyewe. . . .So waacheni
 
Ccm haiwezi kusambaratishwa na mchumia tumbo. Sana atasambaratika mwenyewe
 
You are entitled the right to voice out your opinions. And you are making the most of it..
 
Back
Top Bottom