Jamani tulishawahi kuujadili vyakutosha huko nyuma kuhusiana na waraka huu. Huyu mzee anajua tofauti kati ya waraka na ilani. Lakini kwa makusudi kabisa anaamua kutumia neno "ILANI" mahali pa "WARAKA" ili kuwapumbaza watu kuwa kanisa linaandaa ilani (manifesto) itakayofuatwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi ujao. Huu ni opotoshaji mkubwa ambao watu wenye mawazo na mtizamo chanya wanapaswa kumkemea huyu babu. Iweje watu waelekezwe namna ya kuchagua miongoni mwetu viongozi waadilifu iwe ni kuchochea udini? Au ni kwa namna gani watu wakumbushwe jinsi ya kujali utu na rasilimali za taifa iwe ni ubaguzi? Ni kwanini huyu mzee hataki kuonyesha kwenye huo waraka mahali ama vipengele vinavyohashiria udini ama machafuko katika jamii? Nafikiri kuna sababu ya kumpuuza kwa kukaa kimya kwani pia hiyo ni adhabu tosha.
Mtu wa pwani
Baba wa Taifa mwl Nyerere angekuwepo kingunge asingekuwa anakusanya kusanya vikodi ,kodi pale ubungo, PInda !!..... pinda !!! tusomeeee basi hiyo ripoti ya kituo cha basi cha ubungo
Sasa kama umemuelewa ebu tueleze tatizo analoliona kwenye Waraka wa Wakatoliki ni ipi?Wakatoliki wanawaelimisha waumini wao mambo mengi pamoja na namna ya kuwatambua Viongozi waadilifu,tatizo liko wapi?Somo la Civics linafundishwa mashuleni hapo vipi unajua hiyo?Si chama cha siasa tu ndio kina jukumu la kuwafundisha wananchi juu ya uadilifu wa Viongozi hata wewe ni jukumu lako.Viongozi wa Dini watawaongoza je waumini wanaonyonywa na masikini wa kutupwa bila kuwaepusha na unyanyaji huu?Upo hapo fafanua basi uelewa wako.Mimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu
Kwa wale waliomsikiliza na kumuona Kingunge akiongea na waandishi wa habari jana bila shaka watakuwa na maoni tofauti kuhusu kikongwe huyu. Binafsi namuona kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa. Alikuwa anazungumzia Waraka wa Kanisa Katoliki lakini mpangilio wake wa maneno ni wa kushangaza na hauna mantiki. Mpaka sasa hajasema ni nini hasa anachoona yeye ni kibaya katika waraka huo unaohamasisha wananchi kuchagua viongozi waadilifu, zaidi ya kusisitiza kwamba utaigawa nchi.
Mzee Kingunge ni hypocrite. Nasema hivyo kwa sababu kwenye mambo ambayo ni ya msingi kama vile ufisadi na swala la mahakama ya kadhi ambalo hasa ndio chimbuko halisi ya waraka huu unaopigiwa sana kelele hasemi kitu. Hivi kweli kuna swala linatishia kugawa nchi kama ufisadi, IOC na mahakama ya kadhi hapa nchini? Wakati tume ya Christian Proffesionals of Tanzania ( waasisi wa waraka wa wakatoliki) walipokwenda kuwaelezea wabunge Dodoma athari za IOC na mahakama ya kadhi Kingunge alikuwa usingizini? Anataka kutwambia hakujua kilichokuwa kinaendelea pale Dodoma au anagwaya kwa vile mambo aliyoweka kwenye ilani ya CCM 2005 matokeo yake ndio hayo!! AJILAUMU mwenyewe kwa kuwa myopic kwenye maswala ya kitaifa.
Mzee Kingunge ni hypocrite. Hivi kweli kuna swala linatishia kugawa nchi kama ufisadi, IOC na mahakama ya kadhi hapa nchini? AJILAUMU mwenyewe kwa kuwa myopic kwenye maswala ya kitaifa.
Swali ninalojiuliza ni kwa nini JK amekuwa kimya sana juu ya swala hili?ni kwa nini Pinda aliposema kule bungeni hakutoa kauli nyooofu?bila shaka watanzania wenzangu kuna jambo hapa linalofichwa hapa na serikali yetu....Hii ni dalili tosha ya aina ya viongozi tulionao
1) Huficha ukweli
2) Kila anayejitahidi kuleta mabadiliko hupigwa vita
3) Njia rahisi kwao ya kutatua matatizo ni kuyakwepa
SAIDSABKEMimi nadhani ambaye hajamuelewa ni mbumbumbu aliyoyaeleza ni ukweli mtupu iweje anayeukosoa kitemdo cha Roman Catholic kuandaa waraka anaambiwa fisadi na kubezwa ili kila hali tunajua kuwa Dini isichanganywe na siasa.Hivi kweli Mwenye akili timamu anataka watanzania tuongozwe na Mashikh na Maaskofu nani wa kumchagua.Au hizi fedha chafu zinazotolewa kama njugu kama misaada zinatufanye tupoteze misimamo yetu