Kingunge akerwa, akemea yanayoendelea ndani ya CCM

Kingunge akerwa, akemea yanayoendelea ndani ya CCM

Huyu mzee anazeeka vibaya, ukisikilza vizuri lile kongamano la warioba hamprey na butiku wamemnanga hasa hasa.

Naam! Wamemshangaa sana Kingunge badala ya kumshauri Rais yeye anajificha kwa mgombea mmoja. Ajifunze kwa Butiku na Warioba, wao wanaonesha njia na kumshauri Rais. Hao ndo wenye chama nchi wanaijua leo wamemaliza ni kuchinja tu.
 
sasa anaaminikeje? kwa nini tusiamini kwamba anasema kwa lengo la kumbeba mgombea wake?
anatumia haki yake ya Kidemokrasia na sidhani kama anaongea uongo! Kosa analofanya Kikwete ni kutaka kutupatia Rais ajaye kwa majungu huku akijisahau kuwa hana influence hiyo! Anataka kujifanya Nyerere chama kitampasukia...:llama:
 
LOWASSA aliwahi kuiibia nini Nchi hii zaidi ya majungu, fitina, na umbea usiokuwa na ushahidi?

Vyombo vyenye mamlaka ya RUSHWA, UFISADI, WIZI etc havijawahi kumtia hatiani LOWASSA kwa lolote lile, iweje wewe na ubush lawyer wako umtuhumu LOWASSA kuwa ni mwizi?

CCM yenyewe lishindwaje kumwajibisha muda wote huo? matokeo yake ikaona LOWASSA yu safi kiasi cha kuweza kupewa fomu ya kugombea Urais kupitia CCM?

Hizi Porojo hazina nafasi tena ndani ya CCM. Kwakuwa LOWASSA ndiye anayekubalika ndani na nje ya CCM,

tumchague huyo, hatuna option nyingine kama chama.

Mwalimu Nyerere alipokuwa hai alisema bayana kuwa utajiri wa huyu kiumbe Lowasa tene wakati huo akiwa kijana una mawaa kwani alikopata huo utajiri na namna alivyoupata haijulikani; Lowasa hakuwahi kujibu wala kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.

Lowasa anahusishwa na migogoro mingi ya ardhi iliyoshika kasi hapa nchini kuanzia kwenye viwanja hadi wakulima na wafugaji na migogoro hii ilianza kufukuta wakati akiwa Wizara ya Ardhi;

Lowasa yupo kwenye list ya mafisadi iliyotajwa Mwembe Yanga mwaka 2007; kwa kutajwa huko hakuwahi kujibu wala kufungua mashitaka kwa kuchafuliwa jina lake;

Lowasa anashutumiwa kuwa mhusika mkuu wa kashfa ya Richmond iliyomfanya aachie nafasi yake kama Waziri Mkuu, tangu azire nafasi hiyo hajawahi kuweka bayana kuhusika ama kutokuhusika kwake kwenye kashfa hiyo;

Lowasa anatuhumiwa kutumiwa ama kushirikiana na wafanyabiashara haramu inayohusu utakatishaji wa fedha haramu ikijumuisha ushikiano na wezi, mafisadi na wahujumu uchumi wa taifa hili na ndiyo wanaotumia nguvu kubwa ya fedha, ghiliba, ulaghai na hata nguvu za giza kuhakikisha kuwa anakuwa rais wa Tanzania kwa minajili ya kufanikisha mambo yao, hadi leo Lowasa hajawahi kukanusha hilo ikiwemo kuweka wazi vyanzo ama anakopata fedha za kugharamia mambo mengi ikiwemo michango anayotoa kwenye taasisi za dini badala yake ameishia kusema kuwa ana marafiki wanaomsaidia;

Yako mengi ya kujiuliza lakini hayapatiwi majibu fasaha.....
 
Warioba hajasema Makongoro apitishwe wao wako neutral sana, hawajaegemea upande wowote wanachotaka fisadi asipitishwe basi. Kingunge ameamua kuacha kulea chama na kuwa mshauri kwa wagombea wote akaamua kuwa mpambe wa safari ya matumaini.

haa haa ni kweli mkuu kingunge tayari ana mgombea wake lowasa. na kashasema lowasa asipopitishwa ccm itapoteza mwaka huu...
 
Naunga mkono maneno yako. Lakini ngoja leo nikukumbushe kidogo kuhusu Kikwete; rejea akipowageuka watanzania kwenye katiba mpya baada ya chama chake kumtisha. Ataweza leo kutupa rais msafi. R.I.P Nyerere.

Tumwamini kuwa atafanya hivyo, hii ndio zawadi yake ya mwisho kwa Watanzania.Anastahili kulilinda taifa kutoka kwa kikosi hiki cha wezi na mafisadi.
 
Imevuma sana hii na sasa inalazimika kupasuka itake isitake ..asante Kingunge kwa kuuchochea
 
mwalimu nyerere alipokuwa hai alisema bayana kuwa utajiri wa huyu kiumbe lowasa tene wakati huo akiwa kijana una mawaa kwani alikopata huo utajiri na namna alivyoupata haijulikani; lowasa hakuwahi kujibu wala kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.

Lowasa anahusishwa na migogoro mingi ya ardhi iliyoshika kasi hapa nchini kuanzia kwenye viwanja hadi wakulima na wafugaji na migogoro hii ilianza kufukuta wakati akiwa wizara ya ardhi;

lowasa yupo kwenye list ya mafisadi iliyotajwa mwembe yanga mwaka 2007; kwa kutajwa huko hakuwahi kujibu wala kufungua mashitaka kwa kuchafuliwa jina lake;

lowasa anashutumiwa kuwa mhusika mkuu wa kashfa ya richmond iliyomfanya aachie nafasi yake kama waziri mkuu, tangu azire nafasi hiyo hajawahi kuweka bayana kuhusika ama kutokuhusika kwake kwenye kashfa hiyo;

lowasa anatuhumiwa kutumiwa ama kushirikiana na wafanyabiashara haramu inayohusu utakatishaji wa fedha haramu ikijumuisha ushikiano na wezi, mafisadi na wahujumu uchumi wa taifa hili na ndiyo wanaotumia nguvu kubwa ya fedha, ghiliba, ulaghai na hata nguvu za giza kuhakikisha kuwa anakuwa rais wa tanzania kwa minajili ya kufanikisha mambo yao, hadi leo lowasa hajawahi kukanusha hilo ikiwemo kuweka wazi vyanzo ama anakopata fedha za kugharamia mambo mengi ikiwemo michango anayotoa kwenye taasisi za dini badala yake ameishia kusema kuwa ana marafiki wanaomsaidia;

yako mengi ya kujiuliza lakini hayapatiwi majibu fasaha.....
kwa kiliyako uliyosomeshwa kwa.mkopp ambaoau jalipa serikalini.kuna.kesi waliomfungulia.katiya hizo.na.kama.sio

usiandike.----- tena kwenye.ma great thinkers
 
Hivi ndani ya chama chenu kuna msafi? Tangu lini? Kikwete mwenyewe mwizi na fisadi. Ndiyo sababu alipotamka kauli ya kulivua gamba ili kuwafukuza mafisadi ndani ya chama chenu cha mafisi akina fisadi Lowassa, fisadi Chenge, fisadi Rostam na mafisadi wengine na wao kuamua kumtisha kwamba wataamua kuanika uozo na madudu yake hadharani akanywea. Usijibaraguze kama vile huujui uchafu wa fisadi Mamvi Lowassa.

LOWASSA aliwahi kuiibia nini Nchi hii zaidi ya majungu, fitina, na umbea usiokuwa na ushahidi?

Vyombo vyenye mamlaka ya RUSHWA, UFISADI, WIZI etc havijawahi kumtia hatiani LOWASSA kwa lolote lile, iweje wewe na ubush lawyer wako umtuhumu LOWASSA kuwa ni mwizi?

CCM yenyewe lishindwaje kumwajibisha muda wote huo? matokeo yake ikaona LOWASSA yu safi kiasi cha kuweza kupewa fomu ya kugombea Urais kupitia CCM?

Hizi Porojo hazina nafasi tena ndani ya CCM. Kwakuwa LOWASSA ndiye anayekubalika ndani na nje ya CCM,

tumchague huyo, hatuna option nyingine kama chama.
 
Wewe ni muhuni tu, Tunakufahamu kupitia JAMIIFORUMS muda mrefu, Huna ubavu wa kufanya utafiti wowote. LOWASSA anapendwa na wanachama wa CCM, wasio wanachama wa CCM, na wasio na vyama kabisa.

tuthibitishie mkuu hayo unayoyasema...
 
anatumia haki yake ya Kidemokrasia na sidhani kama anaongea uongo! Kosa analofanya Kikwete ni kutaka kutupatia Rais ajaye kwa majungu huku akijisahau kuwa hana influence hiyo! Anataka kujifanya Nyerere chama kitampasukia...:llama:

hiyo haki yake isilazimishe wengine. tumeshamshitukia huyo mzee ni timu lowasa.
 
CCM, sikieni kilio cha walio wengi, Tuwekeeni LOWASSA tumpitishe kwa kura za NDIYO, ashinde kwa kishindo asubuhi ya October 25.
 
Huo Ushahidi wa kutumia Pesa, hata mimi nataka sana kuuona, ili nichague mbivi na mbichi, nimeshauulizia mara nyingi sana, ndani na nje ya JF, lakini naaambulia Porojo tu.

Unajua usinipandishe hasira, ngoja nikwambie kidogo tu. Mzee wa matumaini alivyokwenda Mwanza kuomba kudhamini, alikusanya wazee ISAMILO HOTEL Wakanywa na kula na bahasha za kaki ilikuwa ngumzo hahaha!!
 
Lakini bw. Sam wote tumeisikiliza hiyo taarifa ya habari na hakuna popote alipomtaja yeyote kwa jina. Angeweza akawa alikuwa anamlenga Kikwete au Nape.
Toa maoni yako kuhusu ile sentensi ya Kingunge kwamba wamepita marais kadhaa lakini hawakukifanya chama kuwa kama mali yao! Unadhani inamlenga nani?
 
Imevuma sana hii na sasa inalazimika kupasuka itake isitake ..asante Kingunge kwa kuuchochea

kiujumla huyu babu alipaswa kucheza na wajukuu nyumbani badala ya kuhangaika kuwatetea wagombea wenye madoa kwa taifa letu...
 
Unajua usinipandishe hasira, ngoja nikwambie kidogo tu. Mzee wa matumaini alivyokwenda Mwanza kuomba kudhamini, alikusanya wazee ISAMILO HOTEL Wakanywa na kula na bahasha za kaki ilikuwa ngumzo hahaha!!
Una Ushahidi wowote kuhusu hilo? Au ndio unaendeleza porojo tu? Nyie wahuni ndio maadui wa demokrasia TANZANIA.
 
Back
Top Bottom