Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Kingu: Wabunge wa CCM tusiyumbishwe!

Wabunge wa CCM Tusiyumbe.

Nimeanza kwa Wabunge wa CCM kwa sababu kubwa kwanza sisi chama chetu ndicho kilicho na dhamana ya kuwaongoza watu wa nchi hii.

Lobbing zimeanza za Makampuni makubwa ya Migodi kupinga sheria ya Fao la kujitoa.makampuni binafsi nayo yataanza soon kupinga uamuzi huu kwa maslahi ya wachache Maslahi yasiyozingatia maono ya nchi na Usalama wa Taifa.Maslahi yanayoangalia siasa za muda za kuwafurahisha wanaharakati huku taifa likikosa nguvu ya kiuchumi.

Nawatahadharisha wabunge wote na hasa wa Chama changu CCM,tuwe makini na kila move hasa kipindi hiki ambacho Rais Magufuli amekuja na mwanga juu ya hatma ya viwanda vya nchi hii;Magufuli ameamua nchi iwe ya viwanda kupitia Mifuko hii ya kijamii,Lakini naona mapandikizo yakutaka kuidhoofisha mifuko hii,Mipango hii wanajua wanaoiratibu nia yao lakini wabunge wenzangu na wana CCM fao lakujitoa ni miongoni mwa mipango ovu ya kutaka kumdhoofisha Rais Magufuli na kudhoofisha mapato ya mifuko hii iliyoelekezwa kusimamia mageuzi ya viwanda nchini.

Kwanini watanzania kila jambo tuliwekee siasa?Uimara wa mifuko.ya kijamii popote duniani ndio kiini cha Usalama wa Taifa,Usalama.wa nchi katika kila nyanja iwe ya dharura za kiulinzi au kukuza uchumi hii ni roho ya nchi hasa nchi Hizi zinazoendelea.

Tuwe makini sana juu ya hawa wanaotaka kuturudisha nyuma.Rais anadira ya viwanda,Mifuko hii imepewa jukumu hili kwanini tuanze kutaka kuwadhoofisha.Kwa haraka haraka NSSF wanaweza kuokoa karibu biln 60 pesa ambazo kwa nchi changa kama hii zikiwekezwa kwa busara na uzalendo zinalifanya taifa lipae kiuchumi.

Watanzania tuache siasa pesa hizi ni za watanzania wakifikisha umri unaostahili watalipwa nchi hii lazima itangulize maslahi ya wengi kwa faida ya vizazi,tuache harakati na siasa za kutaka sifa kwa mambo mazito yanayogusa ustawi na usalama wa nchi.

Tuache mifuko ikusanye pesa a kuwekeza kwenye viwanda .Tuache ubinafsi kwa faida ya vizazi vinavyokuja.

Kingu Elibariki
MP Singida West
Daaaaaaaaaaah afu wewe ni mbunge unaetetea wananchi
 
Pale Watanzania wanapofanywa mangumbaru, ATI MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NI KIINI CHA USALAMA WA NCHI!!!

Great THINKERS nielimisheni labda sijui lolote juu ya hili, ni kwa jinsi gani hii mifuko ya jamii inakuwa kiini cha usalama?

Ili twende sawa kwa faida ya kizazi kijacho, basi wabunge wote hasa wa chama changu cha CCM, na mwenyekiti wao watoe mafao yao yawekezwe kwenye ujenzi wa viwanda. Uzuri wanaenda kulipwa soon next two years..

Shibe mbaya sana. Hapaswi kurudi mjengoni huyu.
 
Na ndio mabunge ya ccm yako hivi, mengine sasa hivi yanatoa lame excuses, eti "hatukuona hicho kipengele" utafikiri vipengele vingine ni vya maana. Yapo yapo tu, yamenenepeana kama vyura.
 
Kingu nimesoma na wewe japo nilikuwa mbele yako. Nilikuwa nakuamini lakini sikuwahi kuwaza kuwa wewe ni mjinga kiasi hicho. Inakuwaje uwapangie watu matumizi ya pesa zao au upange bajeti zako za Viwanda kwa maumivu ya wenye pesa na kinyume na matakwa yao
Nilikuwa namtafuta anayemfahamu huyu mtu, je alisoma primary morogoro? Mtakuja Primary? naanzia hapo kwanza. Sekondary sifahamu ila kama ni yeye mama yake alikuwa headteacher hiyo shule.
 
Kuna mama jirani yangu ni mnazi wa ccm vibaya sana, mwakani anastaafu ni mwalimu...aliposikia sheria hii mpya mama wa watu amepigwa na baridi anaumwa kila siku. Nilijaribu kuchunguza tatizo ni nini nikaambiwa alikopa sana akitegemea kupewa pesa nyingi kwa mkupuo ili zingine alipe madeni na salio afungue biashara.

Hua namtania mama VP umejiandaaje na sheria mpya, anasema mwanangu we acha tu....mwisho namwambia ni maombi ya chama chetu kwa serikali lazima tuyakubali kwa mikono miwili....anakua kimya.

Ila ccm mtawauwa wanachama wenu kwa pressure jamani....mnadhani mnamkomoa Mbowe na kampani yake kumbe sisi neo tunaumia, ipo siku jua litawaka wakati wa giza tororo
 
ccm ndiyo wamepata mtaji kwa kuwanyonga wanyonge!!!!Kama serikali hii inavyojinadi kuwa ya wanyonge inatakiwa wanyonge msilalamike furahini mkiitwa wanyonge ili Mnyongwe vizuri.
Hii ni serikali ya wanyongwe sio wanyonge!
 
Kingu nimesoma na wewe japo nilikuwa mbele yako. Nilikuwa nakuamini lakini sikuwahi kuwaza kuwa wewe ni mjinga kiasi hicho. Inakuwaje uwapangie watu matumizi ya pesa zao au upange bajeti zako za Viwanda kwa maumivu ya wenye pesa na kinyume na matakwa yao

Niliwahi kutana na huyo bwana akiwa AC Igunga...Kichwa yake Mhhhh!
 
Huyu mbunge ni fala am sorry to say this nadhani kichwani akili zimeyumba au hazipo
 
Naweza nisiwe tofauti na wewe katika nia njema ya kuimarisha mifuko na uchumi wetu.

Naomba hicho mnachochukua baada ya miaka mitano ambacho ni 40% ya mishahara yote, mkiondoe katika gratuity Kwa kutunga sheria ili kiwekwe kwenye mifuko ya hifadhi za jamii ili tukuze uchumi wetu. Hapo mtaeleweka.

Tehee teh naona leo nawe umeguswa!
 
Kweli kuna wasiasa wanamawazo ya kishenzi sana yaani yeye kwake mifuko ni jambo muhimu kwake kuliko mfanyakazi anaye porwa fedha yake aliyokuwa anakatwa ktk utumishi wake. Ndo maana mntunga sheria za kikandamizaji ili mwonekane mna hela benki badala ya kujali maslahi ya watumishi. Huu utawala kweli ni waajabu.
 
Back
Top Bottom