King'amuzi cha kwenye smart tv za kisasa yani DVB-T2

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
72,431
Reaction score
191,696
Wadau mko poa?

Nadhani kwa ambao mmenunua flat tv recently kuna marketing term ambayo wanaitumia wauzaji TV kwamba "Ina king'amuzi ndani" utaona channel zote bure.Nimeleta mada mezani tupeane uzoefu juu ya matumizi ya hiko king'amuzi cha ndani. Navyoelewa hicho king'amuzi ni mbadala wa decoder, ama reciever za ma dish zile tulizozoea kununua separately na dish lake.

Je, ukichomeka dish moja kwa moja kwenye tv yako au antenna kama ya startimes kuna uwezekano ukapata channel za FTA? Hasa hizi za locals? Kuna mtu yeyote ambae amejaribu kufanya hilo ikafaa?
Chief-Mkwawa
 
Hiyo DVB-T2 kwenye TVs inapokea channels nyingi tu, ni frequency za Startimes na Continental ila channels nyingi zipo scrambled, zinaonyesha channel chache tu hazifiki tano, ila inategemea na eneo ulipo.
Mm natumia antenna ya ndani kupata hizo channels, bado sijajaribu kutumia antenna ya nje.

Copyright [emoji767] 2017-2019 Mr. Mobile, Inc. All Rights Reserved.
 
Wadau mko poa?

Nadhani kwa ambao mmenunua flat tv recently kuna marketing term ambayo wanaitumia wauzaji TV kwamba "Ina king'amuzi ndani" utaona channel zote bure.Nimeleta mada mezani tupeane uzoefu juu ya matumizi ya hiko king'amuzi cha ndani. Navyoelewa hicho king'amuzi ni mbadala wa decoder, ama reciever za ma dish zile tulizozoea kununua separately na dish lake.

Je, ukichomeka dish moja kwa moja kwenye tv yako au antenna kama ya startimes kuna uwezekano ukapata channel za FTA? Hasa hizi za locals? Kuna mtu yeyote ambae amejaribu kufanya hilo ikafaa?
Chief-Mkwawa
Mkuu kuna DVB-T na DVB-S pamoja na version zake.

Hio DVB T ndio terrestrial, ni digitali lakini inatumia antena kama mfumo wa startimes na continental, utapata chanells ila kama mawimbi yapo eneo lako.

DVB S yenyewe ndio ya madishi na satelite, hii ndio unafunga Dishi na kuelekezea ipande fulani ili upate chanell zake.

Hio DVB T wanatumia sana watu ila ni hit na miss haina uhakika asilimia 100 tokana na eneo
 
Kwa hiyo ni vyema kununua zenye DVB S?
 
Kwa hiyo ni vyema kununua zenye DVB S?
Mkuu nafikiri jibu sahihi ni angalia matumizi yako.

DvB-T ni rahisi unaweza tumia hata kibakuli kama antena na inaweza kidhi mahitaji yako, wengine local chanell mbili zinawatosha, pia technology hii ipo karibia tv zote.

DvB s si rahisi gharama za kununua dishi na kufunga masuala ya kusearch etc pia si tv zote zina hii tech ila uzuri wake chanell ni uhakika, kuna muelekeo wa local chanell.

Pia DVB S hii haina biss key, power vu wala kochakachuzi chochote itakuwa limited compare na receiver kama strong
 
DVB T - Digital Video Broadcast - Terrestrial , hii inatumia antena na sio satellite dish na ndio ipo kwenye tv nyingi zinasemwa kuwa na king'amuzi cha ndani.

DVB S - Digital Video Broadcast - Satellite, huu ndio mfumo ambao unaweza kutumia satellite dish, hivi kuna tv ambazo zina DVB S?

DVB C - Digital Video Broadcast - Cable, huu ni mfumo ambao unapata channels za tv kwa kutumia cable mfano cable tv ambazo mikoani zipo nyingi.

DVB H - Digital Video Broadcast - Handheld, huu ni mfumo ambao unapata channels za tv kwa kutumia mobile phone. Mfumo huu unafanya DVB T /T2 kuwa accessible na simu.

DVB H bado ipo kwenye majaribio na kampuni kama Qualcomm bado wanaendelea kukomaa nayo. Ila ni mfumo ambao haukufanikiwa kibiashara na baadhi ya nchi mfano FINLAND walizima signals za DVB H.
 
Mkuu kuna DVB-T na DVB-S pamoja na version zake.

Hio DVB T ndio terrestrial, ni digitali lakini inatumia antena kama mfumo wa startimes na continental, utapata chanells ila kama mawimbi yapo eneo lako.

DVB S yenyewe ndio ya madishi na satelite, hii ndio unafunga Dishi na kuelekezea ipande fulani ili upate chanell zake.

Hio DVB T wanatumia sana watu ila ni hit na miss haina uhakika asilimia 100 tokana na eneo
Dah nimejaribu jana kwenye TCL smart tv. Inanzengua ilikuwa ina search kitu kinaitwa DTV na ATV ila chenga tu sijabahatisha hata moja. Ina technology ya DVB-T na DVB-C!
 
Eneo lako kuna mtu anapata chanell?
 
mijuzi nikijaribu kwenye tv yangu ya lg nikapata chanile.sta tv itv eitv cluas tv staa move sta mziki bbc nazinge kama 2 ila.changamoto kunakipind zingine.azishiki na wakati mwingine zinarudi ila itv na staa tv hazisumbui nimepata afazali kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna DVB-T na DVB-S pamoja na version zake.

Hio DVB T ndio terrestrial, ni digitali lakini inatumia antena kama mfumo wa startimes na continental, utapata chanells ila kama mawimbi yapo eneo lako.

DVB S yenyewe ndio ya madishi na satelite, hii ndio unafunga Dishi na kuelekezea ipande fulani ili upate chanell zake.

Hio DVB T wanatumia sana watu ila ni hit na miss haina uhakika asilimia 100 tokana na eneo
Samahani mkuu hii DVB-S cable unachomeka hapo hapo kwenye port ya antenna?
 
Dah nimejaribu jana kwenye TCL smart tv. Inanzengua ilikuwa ina search kitu kinaitwa DTV na ATV ila chenga tu sijabahatisha hata moja. Ina technology ya DVB-T na DVB-C!
Pole mkuu ila usichoke jaribu kuweka antenna ndefu mie pia ninatumia TCL ila napata chaneli za ITV,EATV,CLOUDS TV, STAR TV, AGAPE, STAR BUNGE, BBC, STAR MOVIE (kwa sasa imeganda/stuck) UHAI TV, TV1, (mawimbi yake si mazuri sana, ila chaneli ni nyingi kwa eneo langu zingine sizikumbuki
 
We uko maeneo gani mkuu? Na miji inaonesha miji gani maana kwangu zinaonekana nchi za ulaya tu. Kwa Africa ni South Africa tu. Umeitega nchi gani mkuu!?
 
Je hii kwa watu wa mikoani kama Lindi huku inafanya kazi ,mahitaji muhimu ya kufanikisha zoezi hili ni yapi manake sina uelewa wowote kuhusu vitu hivi nahitaji mwongozo Nina tumia tcl
 
Samahani mkuu hii DVB-S cable unachomeka hapo hapo kwenye port ya antenna?
Separate port angalia mfano wa picha ya ports kwenye tv yenye dvb s2

tivi-lg-43lf631v-1-org-12.jpg

Kunakuwa na port ya Antenna na LNB
 
Mkuu kama una dish elekeza uelekeo wa Amos 5. Kwa kutumia hiyo built in receiver yako kwenye Tv.
Nina miez kadhaa sasa napata free channels more than 30 nina receiver ya mpeg4 Dvb T2 & S2.

SangaweJr
 
Back
Top Bottom