KINANA: Urais wa Samia sio wa Kikatiba, amepatikana kwa Uchaguzi

Asali ukiramba sana inakuparia ssa yye amesha changanyikiwa na utamu tuseme mzeee kazeheka mpka anatapikaalichoramba?
 
Urais wake wa kikatiba..hakuna sehemu baada ya jpm kufariki aliingia barabarani kuomba kura kwa wanachi ili awe rais wa nchi hii...kinana acha upotoshaji kwanza wewe zi uliandika barua ya kustaafu siasa kutokana na umri kilicho kurudisha kwenye siasa ni nini.?kama sio u.. wako.

#MaendeleoHayanaChama
Asali kurba
 
Poor reasoning from Kinana! Kama kweli Kinana anadhania zile Kura Uraisi wa Magufuli zilichangiwa na uwepo wa mama ni kwa nini wananchi hawampendi mama kiasi hicho wakati walimpigia? Hivi anaamini Toka moyoni mwaka 2015 na 2020 watu walimpigia Magufuli kwa sababu yuko na Samia? Ama kweli ukubwa wa Kamasi sio wingi wa Kamasi. Nilitarajia Kinana kwa jinsi anavyosifiwa kuwa na Akili angetumia hoja nzito sana hata za Kifalsafa kumaliza huu mjadala lakini naona ni ajeongea kingumbaru fulani hivi. Eti Makamu Mwenyekiti! Kiongozi wa Chama ni Maono. Hakuna maono yasiyoendana na namna ya kuchambua na kujibu hoja vizuri.
Wewe ndo usompenda kwa chuki zako binafsi.
But haikusaidii kitu sana sana wajizeesha tu, she's there as our President hutaki hama nchi
 
Unafikiri Kwa kutumia kwato badala ya Misuli ya Kichwa. Mimi nimchukie kwani Ndio kwamba Ni Demu kaniacha? Hebu tuwekee hapa Utafiti wa kuonyesha mama anakubalika hapa Nchini? Hebu tusaidie Toka mama ashike madaraka umeona ameshaonana na Kiongozi gani Duniani Mwenye ushawishi? Nakupa huo mfano tu utoshe kukuonyesha kuwa sio watanzania tu wasiomuona mama kuwa ni Kichwa Bali hata wa huko Duniani.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ameweka wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hasasan ni Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amepatikana kwa mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kupigiwa kura na wananchi.

Kinana ametoa ufafanuzi huo jana wakati akizungumza na wana CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutekeleza vema Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025.

“Nataka niseme na vizuri Watanzania wakajua tangu Rais Samia achukue uongozi wa taifa letu kuna kauli nimekuwa nikisikia baadhi ya kauli kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba. Kauli hii ina ukweli lakini haina ukweli.

“Inaukweli kweli kwasababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila chama kitaweka mgombea na mgombe mwenza na Katiba inasema mgombea Mwenza na mgombea wanafasi moja ya kupiga kampeni ya chama chao na kila Chama kinapochagua Mgombea Mwenza,”amesema Kinana.
============

Amefafanua CCM hakimchagua mgombea mwenza kwa kucheza bahati nasibu ya kutumbukiza halafu tuangalie nani kapata nani kakosa bali wameweka sifa, kwa kuangalia uwezo, kukubalika , anafaa ,uwezo wa kufanya kampeni, , anaweza kuleta kura nyingi na mwisho wanajiuliza iwapo mgombea kwa sababu yoyote atakuwa hayupo au ameondoka madarakani je mgombea mwenza atamudu nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vigezo vyote hivyo vilipimwa kwa Samia.

“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.

“Kwa hiyo kwa wale wanaosema huyu ni Rais wa Katiba si kweli , Rais Samia Suluhu Hassan alipimwa kabla ya kupewa hiyo nafasi, bahati nzuri mimi nilikuwa Katibu Mkuu wa Chama, nilishiriki vikao vya awali mwaka 2015 na wengine walikuwepo kwenye vikao, hayo maswali yote tulupojiuliza tukasema anaweza ,ana mudu hiyo kazi, anaongeza kura, ana uzoefu, anakifahamu chama cha mapinduzi lakini kama anahitajika kuwa Rais anaweza.

“Sasa unaposema Rais Samia ni Rais wa Katiba hakuchaguliwa sio kweli lakini kubwa zaidi Rais anapopigiwa kura na mgombea mwenza anapigiwa kura na kabla haijafika muda wa kupiga kura iwapo mgombea mwenza Mwenyezi Mungu atamchukua uchaguzi utasimmamishwa.”

Ameongeza kwa kueleza “Kwa nini usimamishwe? Kama kweli yeye ni Rais tu wa Katiba tuendeee kupiga kura mambo yaishe .Mwaka 2005 tulikuwa na mgombea mwenza wa CHADEMA Jumbe Rajab Jumbe mwenyezi Mungu akamchukua , uchaguzi ulisimamishwa, kwanini ulismamishwa? Kwasababu na yeye ananafasi muhimu hawezi rais wan chi akapigiwa kura au mgombea akapigiwa kura kama mgombea mwenza hayupo.

“Wanasema Rais Samia ni Rais wa Katiba hawasemi kweli, Rais Samia ni Rais aliyetokana na mchakato wa uchaguzi , alipopigiwa kura Rais Magufuli na Samia alipigiwa kura hapo hapo kama rais aliyemtangulia angekuwa ameondoka madarakani kwa kujiuzulu au kwasababu nyingine yoyote angekuwa Rais lakini kwasababu za Mwenyezi Mungu Rais Samia amechukua dhamana.

“Kwanini basi uchaguzi wa Chadema mwaka 2005 ulisimamishwa? Kwasababu wote wawili wanatokana na utaratibu wa Katiba uliowekwa kwa hiyo Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wale wanaosema ni Rais wa Katiba wana ajenda yao, msiwasikilize. Kama hawajui au wanajifanya hawajui , nadhani sasa watajua, nilisema wanaosema Rais Samia ni wa Katiba hawasemi kweli na nimetoa maelezo.

“Sasa nitoe upande wa pili kweli ni Rais wa Katiba.Katiba inasema hivi kila Chama kitateua mgombea na mgombea mwenza, kwa hiyo kila Chama kinateua Mgombea na Mgombea Mwenza , Rais au mgombea anatokana na matakwa ya Katiba ya Jamhurii ya Muungano wa Tanzania.

“Mgombea mwenza ni matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano , kwa hiyo anateuliwa Samia kuwa mgombea mwenza ambaye baadae anakuwa Rais anatokana na matakwa ya Katiba kwa hiyo Rais Maguli ni Rais wa Katiba , unapendekezwa na chama chako, uakwenda kwa wananchi lakini hupigiwi kura peke yako unapigiwa na mgombea mwenza.

“Iwapo hayupo uchaguz unaahirishwa , kwa hiyo nimalize kwa kusema tukisema kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba husemi ukweli, Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.nchi ya Marekani Rais wa sasa ni Rais wa 46 , katika marais 46 waliowahi kufariki kabla ya muda wao walikuwa marais wa nane baadae wakachukua wagombea wenza ambao baadae wakaja kuwa marais,” alifafanua.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo nchini Marekani hawajawahi kuwaita Marais hao ni WA katiba, “lakini hapa Tanzania wanaotaka kukoroga mambo wanakwambia Rais Samia ni Rais wa Katiba.”

Katika hatua nyingine, Kinana alifafanua kuwa, katika kudhirisha sifa za uongozi wa Rais Samia ameweka alama kubwa za maendeleo katika kila mkoa wilaya na shehia nchi nzima.

“Yote haya ya mefanyika katika muda mfupi wa mwaka mmoja wa uongozi wake
fedha za maendeleo zimetokana na ukusanyaji mkubwa wa kodi kwa njia ya hiyari, fedha za misaada na mikopo zilikuja kotokana na kukubalika kwake duniani.

SHAKA ASEMA RAIS SAMIA,DK.MWINYI 2030

Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameweka wazi kwamba kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Samia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwatumikia na kuwaheshimisha Watanzania, kuiheshimisha Afrika na Dunia awataendelea kuwa madarakani hadi 2030.

Amesema kwa pamoja wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kusimamia maendeleo endelevu na kudumisha na kuimarisha muungano.

“Mitano kwa Rais Samia haina mjadala biashara imekwisha, kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu, Katiba yetu na utamaduni wetu huu mjadala haupo tena.Kama kuna mtu ana ndoto, hizo ndoto zikae pembeni Dk.Mwinyi tunamalizana 2030 , Chama hiki kina msingi na msingi wake mkuu ni Katiba, Kanuni na taratibu lakini kina utamaduni wake , hivyo viongozi hawa watatuvusha mpaka 2030 halafu ndio tunaangalia Katiba inasemaje.

JAMHURI
Ni wajinga na wapuuzi wanaosema hajapatikana kwa Katiba wakati wanafahamu kabisa kwamba amezunguka Nchi hii kama mgombea mwenza wa Rais kutafuta kura..

At least wanaosema awamu ya 5 Sio ya sita unaweza waelewa but all in all huu ndio ukweli..
 
Kama yeye yalivyo mawazo yake na wenye kauli pia hayo ni mawazo yao, na kama wenye kauli nao ni wapiga kura huwezi kuwapangia / kuwachaguliwa walipiga kura kuchagua nani au nini....

Huu muda wangetumia vema kutatua changamoto wala wasingepata tabu ya as the saying goes "Put Lipstick on you know What".....
 
Mfano mwingine hai. Dr. Mpango hajapigiwa kura na wananchi. Hivyo hawezi kuwa Rais endapo kutatokea vacancy kwa namna yoyote ile.

Ila SSH ni sawa maana alipita Tanzania nzima kuomba kura.
Nadhan katiba haimzuii Mpango ku ascend kwenye power kama ikitokea incapacitation yoyote...Kinana yuko kazini, na kayasema aliyoyasema kwenye viunga vya nyumbani na shughuli yenyewe ilikua ndo haswa sehemu ya kupakana mafuta...ila kwa katiba yetu ilivyo...Kazi namba moja ya makamu wa RAIS ni kuwa back up ya RAIS..na ndio maana RAIS akiteua Makamu kama ilivyotokea kwa Mpango...Bunge kwa niaba ya wananchi wanatakiwa wamdhibitishe/ wampigie Kura..
 
Akili KUBWA PEKEE ndio itamwelewa kinana!

"Ukiona mkeo anakwambia KWA wewe ndio Baba wa Familia ujue kuna Baba Mwingine yupo"

Kauli ya kinana inahalalisha Jambo FULANI kutokea!kwamba kuna watu au kundi litajitokeza au tayari linasema mama sio chaguo ni bahati mbaya tu amepata urais!!

Mama atapigwa tukio Hadi atashangaa!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.
Kinana unajua kuwa wale traffic wako hawajapunguzwa barabarani kutokana na siasa zako !!!
 
Katiba mbovu na hatari sana!!makamu anaweza shiriki njama za kumuua aliyeko madarakani ili achukue kijiti
Mfano mwingine hai. Dr. Mpango hajapigiwa kura na wananchi. Hivyo hawezi kuwa Rais endapo kutatokea vacancy kwa namna yoyote ile.

Ila SSH ni sawa maana alipita Tanzania nzima kuomba kura.
 
Uchaguzi upi?

Tukiacha mbambambaaa wakaweka mambo sawa ndani ya chama kugombea nafasi ya ugombea urais akawashinda wote kama Shujaa hapo tutaita uchaguzi akaingia barabarani kuomba kura
 
Poor reasoning from Kinana! Kama kweli Kinana anadhania zile Kura Uraisi wa Magufuli zilichangiwa na uwepo wa mama ni kwa nini wananchi hawampendi mama kiasi hicho wakati walimpigia? Hivi anaamini Toka moyoni mwaka 2015 na 2020 watu walimpigia Magufuli kwa sababu yuko na Samia? Ama kweli ukubwa wa Kamasi sio wingi wa Kamasi. Nilitarajia Kinana kwa jinsi anavyosifiwa kuwa na Akili angetumia hoja nzito sana hata za Kifalsafa kumaliza huu mjadala lakini naona ni ajeongea kingumbaru fulani hivi. Eti Makamu Mwenyekiti! Kiongozi wa Chama ni Maono. Hakuna maono yasiyoendana na namna ya kuchambua na kujibu hoja vizuri.
Nani alimpigia kura Magufuli kwa wingi? Wacha uwongo wa mchana. Magufuli alimshinda Lowasssa mwaka 2015 kwa wizi wa kura za kupitia kituo cha Masaki. Muulize Medestus Kapilimba, Kinana na Januari.

Mwaka 2020 aliammua kuziiba kura zote mwenyewe Magufuli kwa kutiki makaratasi kutokea Jamana Printers na Kambi ya Mbweni Kisha ma DSO na DED wakagawiwa makatasi yaliyopigwa. Zile kura tulizopiga wananchi hazikuhesabiwa.

Dhana ya kwamba Magufuli alikuwa anapendwa ni UWONGO, kadanganye wanao au wajinga wenzio
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ameweka wazi kuwa Rais Samia Suluhu Hasasan ni Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amepatikana kwa mchakato wa uchaguzi mkuu kwa kupigiwa kura na wananchi.

Kinana ametoa ufafanuzi huo jana wakati akizungumza na wana CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutekeleza vema Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025.

“Nataka niseme na vizuri Watanzania wakajua tangu Rais Samia achukue uongozi wa taifa letu kuna kauli nimekuwa nikisikia baadhi ya kauli kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba. Kauli hii ina ukweli lakini haina ukweli.

“Inaukweli kweli kwasababu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila chama kitaweka mgombea na mgombe mwenza na Katiba inasema mgombea Mwenza na mgombea wanafasi moja ya kupiga kampeni ya chama chao na kila Chama kinapochagua Mgombea Mwenza,”amesema Kinana.
============

Amefafanua CCM hakimchagua mgombea mwenza kwa kucheza bahati nasibu ya kutumbukiza halafu tuangalie nani kapata nani kakosa bali wameweka sifa, kwa kuangalia uwezo, kukubalika , anafaa ,uwezo wa kufanya kampeni, , anaweza kuleta kura nyingi na mwisho wanajiuliza iwapo mgombea kwa sababu yoyote atakuwa hayupo au ameondoka madarakani je mgombea mwenza atamudu nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vigezo vyote hivyo vilipimwa kwa Samia.

“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.

“Kwa hiyo kwa wale wanaosema huyu ni Rais wa Katiba si kweli , Rais Samia Suluhu Hassan alipimwa kabla ya kupewa hiyo nafasi, bahati nzuri mimi nilikuwa Katibu Mkuu wa Chama, nilishiriki vikao vya awali mwaka 2015 na wengine walikuwepo kwenye vikao, hayo maswali yote tulupojiuliza tukasema anaweza ,ana mudu hiyo kazi, anaongeza kura, ana uzoefu, anakifahamu chama cha mapinduzi lakini kama anahitajika kuwa Rais anaweza.

“Sasa unaposema Rais Samia ni Rais wa Katiba hakuchaguliwa sio kweli lakini kubwa zaidi Rais anapopigiwa kura na mgombea mwenza anapigiwa kura na kabla haijafika muda wa kupiga kura iwapo mgombea mwenza Mwenyezi Mungu atamchukua uchaguzi utasimmamishwa.”

Ameongeza kwa kueleza “Kwa nini usimamishwe? Kama kweli yeye ni Rais tu wa Katiba tuendeee kupiga kura mambo yaishe .Mwaka 2005 tulikuwa na mgombea mwenza wa CHADEMA Jumbe Rajab Jumbe mwenyezi Mungu akamchukua , uchaguzi ulisimamishwa, kwanini ulismamishwa? Kwasababu na yeye ananafasi muhimu hawezi rais wan chi akapigiwa kura au mgombea akapigiwa kura kama mgombea mwenza hayupo.

“Wanasema Rais Samia ni Rais wa Katiba hawasemi kweli, Rais Samia ni Rais aliyetokana na mchakato wa uchaguzi , alipopigiwa kura Rais Magufuli na Samia alipigiwa kura hapo hapo kama rais aliyemtangulia angekuwa ameondoka madarakani kwa kujiuzulu au kwasababu nyingine yoyote angekuwa Rais lakini kwasababu za Mwenyezi Mungu Rais Samia amechukua dhamana.

“Kwanini basi uchaguzi wa Chadema mwaka 2005 ulisimamishwa? Kwasababu wote wawili wanatokana na utaratibu wa Katiba uliowekwa kwa hiyo Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wale wanaosema ni Rais wa Katiba wana ajenda yao, msiwasikilize. Kama hawajui au wanajifanya hawajui , nadhani sasa watajua, nilisema wanaosema Rais Samia ni wa Katiba hawasemi kweli na nimetoa maelezo.

“Sasa nitoe upande wa pili kweli ni Rais wa Katiba.Katiba inasema hivi kila Chama kitateua mgombea na mgombea mwenza, kwa hiyo kila Chama kinateua Mgombea na Mgombea Mwenza , Rais au mgombea anatokana na matakwa ya Katiba ya Jamhurii ya Muungano wa Tanzania.

“Mgombea mwenza ni matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano , kwa hiyo anateuliwa Samia kuwa mgombea mwenza ambaye baadae anakuwa Rais anatokana na matakwa ya Katiba kwa hiyo Rais Maguli ni Rais wa Katiba , unapendekezwa na chama chako, uakwenda kwa wananchi lakini hupigiwi kura peke yako unapigiwa na mgombea mwenza.

“Iwapo hayupo uchaguz unaahirishwa , kwa hiyo nimalize kwa kusema tukisema kwamba Rais Samia ni Rais wa Katiba husemi ukweli, Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.nchi ya Marekani Rais wa sasa ni Rais wa 46 , katika marais 46 waliowahi kufariki kabla ya muda wao walikuwa marais wa nane baadae wakachukua wagombea wenza ambao baadae wakaja kuwa marais,” alifafanua.

Aliongeza kuwa, pamoja na hayo nchini Marekani hawajawahi kuwaita Marais hao ni WA katiba, “lakini hapa Tanzania wanaotaka kukoroga mambo wanakwambia Rais Samia ni Rais wa Katiba.”

Katika hatua nyingine, Kinana alifafanua kuwa, katika kudhirisha sifa za uongozi wa Rais Samia ameweka alama kubwa za maendeleo katika kila mkoa wilaya na shehia nchi nzima.

“Yote haya ya mefanyika katika muda mfupi wa mwaka mmoja wa uongozi wake
fedha za maendeleo zimetokana na ukusanyaji mkubwa wa kodi kwa njia ya hiyari, fedha za misaada na mikopo zilikuja kotokana na kukubalika kwake duniani.

SHAKA ASEMA RAIS SAMIA,DK.MWINYI 2030

Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, tikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameweka wazi kwamba kwa kazi nzuri anayoifanya Rais Samia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwatumikia na kuwaheshimisha Watanzania, kuiheshimisha Afrika na Dunia awataendelea kuwa madarakani hadi 2030.

Amesema kwa pamoja wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kusimamia maendeleo endelevu na kudumisha na kuimarisha muungano.

“Mitano kwa Rais Samia haina mjadala biashara imekwisha, kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu, Katiba yetu na utamaduni wetu huu mjadala haupo tena.Kama kuna mtu ana ndoto, hizo ndoto zikae pembeni Dk.Mwinyi tunamalizana 2030 , Chama hiki kina msingi na msingi wake mkuu ni Katiba, Kanuni na taratibu lakini kina utamaduni wake , hivyo viongozi hawa watatuvusha mpaka 2030 halafu ndio tunaangalia Katiba inasemaje.

JAMHURI
Yaani anampiga jiwe halafu anampamba. What is politics?
 
Mfano mwingine hai. Dr. Mpango hajapigiwa kura na wananchi. Hivyo hawezi kuwa Rais endapo kutatokea vacancy kwa namna yoyote ile.

Ila SSH ni sawa maana alipita Tanzania nzima kuomba kura.
Hivi ulikuwa unaona mikutano yake.? Ulikuwa huwezi hata kuifatilia.
 
Urais wake wa kikatiba..hakuna sehemu baada ya jpm kufariki aliingia barabarani kuomba kura kwa wanachi ili awe rais wa nchi hii...kinana acha upotoshaji kwanza wewe zi uliandika barua ya kustaafu siasa kutokana na umri kilicho kurudisha kwenye siasa ni nini.?kama sio u.. wako.

#MaendeleoHayanaChama
Nadhani watu hawajui maana ya Mgombea mwenza na Vice President kwa nchi zenye mfumo kama wetu.Vice President hayupo tu kumsaidia Rais mawazo Bali ni kuchukua majukumu Rais akitoka.Ukisema akapigiwe kura Tena ni ujuha wa katiba na sheria.Tulishajiwekea huo utaratibu wa wote kupigiwa kura kwa Pamoja sasa ya Nini turudi kupiga kura wakati utaratibu unajulikana.
 
Ni wajinga na wapuuzi wanaosema hajapatikana kwa Katiba wakati wanafahamu kabisa kwamba amezunguka Nchi hii kama mgombea mwenza wa Rais kutafuta kura..

At least wanaosema awamu ya 5 Sio ya sita unaweza waelewa but all in all huu ndio ukweli..
Awamu zinatokana na Rais aliyeko madarakani huwezi SEMA awamu ya Tano wakati Samia ni Rais wa Sita.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom