Kinachomuangusha Rais wetu ni wateule wake!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,658
20,991
Mteule ni nani?
Mteule ni mtu fulani aliyeaminiwa na mteua au kiongozi wa mamlaka fulani ili amsaidie kwa uaminifu katika shughuli za uangalizi, utendaji kuwa mkweli kwa mteua, kumshauri kwa kile kilicho chema bila kumwingiza mteua katika aina yoyote ya uwongo ulaghai wizi na maovu yoyote yale yatakayo mvunjia heshima mteua mbele ya Jamii aliyoapa kuisimamia kwa haki.
 
Kazi ya rais ni kuwasimamia hao wateule wake watimize majukumu Yao, ndo maana tumempa mamlaka ya kuwapiga chini na kuteua wengine akiona hawafanyi vyema kwenye nafasi walizopewa

Kinachonipa wasiwasi ni swala la sisi raia kupaza sauti zetu kwa wingi juu ya ufisadi na mienendo mibaya ya wateule wake, badala ya yeye kuchukua hatua na yeye anarudi kwetu akilalamika kuhusu hao wateule wake bila kuchukua hatua yoyote

Ewe Tanzania yangu!!!
 
Kweli mkuu SHE SHOULD ACT QUICKLY OVER THOSE BURGLARS.
 
Tubadilishe Katiba, Wakuu wa mikoa, wilaya, RAS, DAS na DED wote wachaguliwe na wananchi
 
Kwa heshima tuachane na hadithi za wafu,tuwaache wapumzike kwa amani.
Hilo neno mweleze mzee Y. Marope, Goli la Mkono na wajumbe Mkutano Mkuu CCM

Sisi tunajua na tumaelewa kuwa marehemu anajengewa mnara wa aibu na regime hii. Badala ya kutibu madhara ya awamu iliyopita mnachofanya ni kuhubiri madhara yake.

Wateule kwa asilimia 90 wamepewa nafasi na wanaitumia nafazi hizo kwa kupambana na aliyepo nje ya upeo wa akili na fahamu.

Tumeanza kuzifikia nyama baada ya kufakamia mtori kwa pupa
 
Kinachomzuia kuwatimua walioboronga ni nini?? Rais unaomba watu wajiuzulu!!!?? Haya ni masikhara
 
Mteule ni nani?
Mteule ni mtu fulani aliyeaminiwa na mteua au kiongozi wa mamlaka fulani ili amsaidie kwa uaminifu katika shughuli za uangalizi, utendaji kuwa mkweli kwa mteua,kumshauri kwa kile kilicho chema bila kumwingiza mteua katika aina yoyote ya uwongo ulaghai wizi na maovu yoyote yale yatakayo mvunjia heshima mteua mbele ya Jamii aliyoapa kuisimamia kwa haki.
Kama mteule yupi na amefanyaje? Na lini Wateule hawakuwahi kuwa tatizo hapa Tanzania?
 
Mteule ni nani?
Mteule ni mtu fulani aliyeaminiwa na mteua au kiongozi wa mamlaka fulani ili amsaidie kwa uaminifu katika shughuli za uangalizi, utendaji kuwa mkweli kwa mteua,kumshauri kwa kile kilicho chema bila kumwingiza mteua katika aina yoyote ya uwongo ulaghai wizi na maovu yoyote yale yatakayo mvunjia heshima mteua mbele ya Jamii aliyoapa kuisimamia kwa haki.
Kwani wateule hujiteua wenyewe
 
Yeye na wateule wake lao moja vingenevyo angewatengua

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Tatizo sio wateule, tatizo ni mamlaka ya uteuzi. Ni lazima umjue unayemteua, rekodi yake ya utendaji huko alikotoka na kwa sababu gani unamteua.

Mambo ya kuteua kwa vimemo, sijui mtoto wa fulani au huyu nina mahaba nae, madhara yake ndio haya.
 
Mteule ni nani?
Mteule ni mtu fulani aliyeaminiwa na mteua au kiongozi wa mamlaka fulani ili amsaidie kwa uaminifu katika shughuli za uangalizi, utendaji kuwa mkweli kwa mteua, kumshauri kwa kile kilicho chema bila kumwingiza mteua katika aina yoyote ya uwongo ulaghai wizi na maovu yoyote yale yatakayo mvunjia heshima mteua mbele ya Jamii aliyoapa kuisimamia kwa haki.
True ila sio kosa lake Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
P
 
Back
Top Bottom