#COVID19 Kinachofanyika Kigoma mechi ya Simba Vs Yanga ni aibu kwa nchi

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Uwanja ulishajaa watu bado wanaingia

Corona kuna wagonjwa Kigoma lakini uwanja umejaa kupita kiasi.

Watu bado wanaingia mpaka sasa

Halafu kesho munaanza kutusumbua kwenye public transport eti tuvae mabarakoa.

Na hawa watu wametoka karibu mikoa yote ya Tanzania maana yake maambukizi yatasambaa nchi nzima!!

Uwanja unajazaje watu kuliko uwezo wake wa idadi?


Kinachoendelea kigoma muda huu ni utoto.
 
Corona limekuwa jambo la kisiasa.hivo linaibua hisia tofauti kwA watu tofauti

Serikali ingetoa ufafanuzi huu - kuwa hospitali zetu haziwezi kuhudumia watu wengi kwA wakati mmoja hivyo ni vema kujikinga,ili tusifikie huko......as long as serikali wanavumilia haya ,basi naendelea kuamini in an epidemeologic standpoint,Hali sio mbaya kivile
 
Hii mechi ingefutwa tu
 
Hahahaah si nimesema nikaonekana Mimi Chadema! Yaani wapuuzi badala ya kuangalia kama ninachoongea kina mashiko au lah wao wanaongea ujinga. Na CCM mwaka huu mtazika sana
 
Angalia comments za CCM

 
Reactions: BAK
Wewe ni wakala wa corona?

Kila uzi corona corona jifie huko na makorona yako
 
Mkuu, Serikali yenyewe inajua Corona sio big deal hapa nchini kiivyo, ila kwa kuwa wana njaa na Pesa ya mabeberu ni lazima wawahadae kwa kujifanya wanafuata Yale mabeberu wanataka kusikia.
 
CCM wanawahadaa tu wakubwa wa hii duniani ili waweze kupata fedha za mikopo na misaada wazitumie wanavyojua wao ila sio kweli kuwa wako serious kupambana na corona.
 
Acheni wivu Corona corona corona mnaboa sana kutaka kutawala kila kitu kisa mambo yenu hayaendi mnavyotaka. Kufa kupo pale pale.
 
Hii vita ya korona imekaa kisiasa zaidi wala sidhani hata hao wanaozuia msongamano kama wanamaanisha. Ni vile tu wana jambo lao.
 
Hii mechi ingekuwa taifa linalojielewa isingechezwa, au ichezwe bila mashabiki, hii Corona tunaigiza kupambana nayo.
Hapo yanaangaliwa mapato zaidi. Kama umeshindwa kujikinga mwenuewe utajijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…