Asilimia 90 ya maudhui ya Redio, TV na mitandao Tanzania ni Simba VS Yanga, Muziki na Umbea kutwa nzima

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Ukisikiliza au kutazama vyombo vya habari vya Tanzania utagundua "serious stories" ni chache sana licha ya kuwa na utitiri wa vyombo vya habari kuanzia "main stream media hadi TV za mtandaoni.

Kuna mambo mazito yanayoendelea nchini na yanahitaji mijadala mizito. Mfano:

1. Katiba mpya
2. Udhaifu wa mihimili ya mahakama na Bunge.
3. Mgogoro wa Loliondo
4. Kuongezeka kwa kasi kwa Deni la Taifa na
5. Kuongezeka kwa gharama za maisha.
6. Mjadala kuhusu Bajeti ya 2022/2023.
7. "Updates" ya Miradi mikubwa ya kimkakati km SGR na Bwawa la Mwl. Nyelele.
8. Miradi ya gesi n.k

Haya ni mambo ambayo ni vema Watanzania wakawa wanayasikia kila mara kujua kinachoendelea na kujadili nini kifanyike.

Kwa wenzetu Kenya kwa mfano, ukifungulia TV asubuhi unakutana na jopo la wachambuzi wabobezi( Panelists) wakijadili current issues very serious and deeply about their Nation.

Sisi kwetu kutwa nzima story ni Simba vs Yanga, Music na habari za umbea. TV za mitandaoni ndo kabisaa! Ujinga wote umejaa huko. Mijadala ni Kufumaniana, mapenzi ya Konde na kajala na upuuzi mwingine. Ni Tanzania pekee ambako machawa wanahusudiwa na kupewa udhamini (endorsement) kwa sababu ya uchawa wao.

What a shameful country! kwamba Baba Levo na Mwijaku ni "ma-rolemodel" wa watoto wetu,tunajenga taifa gani baadae?

Miaka ya nyuma wakati magezeti yana nguvu kipindi km hiki cha Bunge la bajeti ilikuwa moto sana. Ni kupitia mijadala mikali na uandishi wa kiuchunguzi ndipo kuliibuliwa kashifa kubwa kubwa km Richmond, Dowans n.k. Ndio maana sasa hivi akina Mwigulu wametuandalia bajeti mbovu kuwahi kutokea lakini hakuna " criticism" zozote. Sisi vyovyote sawa tu muhimu ni Yanga na Simba yetu.

Hata bungeni pia kumekuwa na utoto na mzaha mwingi kuhusu Yanga na Simba. Utazani tuliwatuma wakazodoane kuhusu mpira. Taifa limefanywa kuwa la mizaha mizaha kwa mgongo wa Simba na Yanga. Wanasiasa wanafurahia kwani ni rahisi sana kuongoza watu wasiojali mijadala na hoja nzito.

TV au Radio wanaofanya mijadala, wanafanya kwa namna ya komedi. Wachambuzi wenyewe ndo akina Mwijaku, Baba Levo, Zembwela na Mpoki. Kipindi kizima ni makelele na kucheka cheka tu. Nchi hii ukisha kuwa maarufu no matter ni umaarufu wa nini basi wewe tayari ni zaidi ya Profesa. Mtu yupo tayari ajidhalilishe ili apate umaarufu.Watu wamefunga hadi ndoa feki just for the kiki and trending. Very disgusting!

Taifa limekuwa la machawa,watengeneza kiki na wambea.Ili kijana a-make maisha kirahisi lazima eti afuate huo mkondo.

Tunaenda kujenga Taifa la ajabu ajabu sana kama tusipobadirika.

Nawasilisha.
 
Kwenye vyombo vya usafiri kama mabasi ndiyo balaa unakuta movie zinazowekwa ni kuuana tu. Bado kwenye vibanda mitaani movie ni za kuuana tu, yaani tangu early age watoto wanafundishwa kuuana.
 
Dah, jamaa umeandika kwa hisia kali Sana, hali kwenye hii nchi imekuwa ngumu mno. Afya ya akili ya vijana sasa hivi imepata hitilafu. Someone has to rescue this generation. Truly, it pains.
 
nje ya media walaji vistors nao wanataka umbea kuliko seriously story
Hichi ndio kisingizio media wanatumia kutulisha ufala wao,walaji hawataki umbea ila media Kwa kurahisisha mambo wameona umbea ni rahisi kuupata na hautumii Akili wakawafanya mpaka walaji waupende umbea. Mwisho wa siku media zote hakuna content
 
Nani atajali na viongozi wenyewe ndio hao wasiopenda kuambiwa ukweli

Hao kina mwijaku na Levo wanafanya mambo ambayo alitakiwa afanye binti ilimradi mkono uende kinywani so sad
 
Tukisema nchi imejaa mazuzu mnakasirika, sema ukijifanya kurusha habari kugusa watawala unapotezwa…. hizi ndizo redio ambazo GENTAMYCINE anasikiliza kutwa nzima.
 
Kuanzia asubuhi hadi jioni redio zote ni uchambuzi wa michezo na muziki, usiku ni taarifa ya habari kisha ala za roho na malavidavi.
 
Back
Top Bottom