Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,076
Mleta mada ameleta hoja za msingi sana,lakini as usual zitapuuzwa na watawala waliolewa madaraka!Mkuu umeongea ukweli !yaani sasa hv ni ubaya ubaya!
Mleta mada ameleta hoja za msingi sana,lakini as usual zitapuuzwa na watawala waliolewa madaraka!Mkuu umeongea ukweli !yaani sasa hv ni ubaya ubaya!
Usitokwe tu na mapovu, bali jibu kwa hoja......Jidanganye utaisubiri sana hiyo unaiitaji hiyo utaisubiri sana yaani watu kama nyie ndio wale ambao mkikuta kwenye mini yenu wake zenu hawana mboga za Julia ugali mnaenda kula kwa mamantilie badala ya kununua mboga mpeleke mkashiriki pamoja nyie mnakula huko wasaliti wakubwa nyie kuanzia mijini kwenu mpaka kwa taifa
Sent using Jamii Forums mobile app
Tena ni ubaguzi wa kutisha.....Ubaguzi mbaya sana.
Hiyo lugha ya wahamiaji haramu ni sahihi kabisa,kwa akili ya kawaida watu wa Tarime wanajisikiaje kusikia Bulaya aliyekuja kuhamaisha uchangiaji maendeleo kakamatwa,kisa kashiriki mkutano jimbo jirani.huu ujinga namna ngapi?Tena ni ubaguzi wa kutisha.....
Nchi hii watawala wetu wameigeuza na kuifanya kuwa wenye haki ya kufanya shughuli za kisiasa hapa nchini ni CCM.....
Kwa tafsiri nyingine ni kuwa ingawa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu inasema kuwa nchi yetu ni ya mfumo wa vyama vingi, lakini kwa matendo yanayofanywa na watawala wetu wa awamu ya 5 ni kama tusharejea kwenye mfumo wa chama kimoja!
Wapinzani makini, hususani vyama vya Chadema na CUF wanakuwa treated kama "wahamiaji haramu" na ndiyo maana almost wabunge wote wa Chadema wana kesi mahakamani kwa makosa yaliyobatizwa jina na watawala wetu kuwa ni makosa ya uchochezi!
Kwasababu hakushinda.Siasa za upinzan zingekua na MASHIKO na zenye maslai kwa watanzania leo hii hoja yako ingekuwa na nguvu sana.tungepata magadi na kila aina ya matukio ya kutisha.Serikal ya jpm imechukiwa toka anatangazwa kuwa mshindi 2015 na toka hapo hijawahi tokea upinzan kumuunga mkono jpm.nakumbuka siku ya kwanza tu alienda BOT kejeli na maneno machafu walitoa wapinzan.kila alilokuwa akilifanya lilionekana baya sana.Mbegu ya ubaguzi na chuki ilipandwa na upinzan wenyewe. Jpm sio malaika maana yake anamapungufu yake lkn haiondoi ukwel kwamba mbegu ya chuki imeanza kupandwa na upinzan wenyewe.
Upinzan haukuwa tayar kukubal kuwa uchaguz umeisha,wao waliendeleza kila aina ya mbinu kuhakikisha jpm hafanikiwi ktk mambo yake. Watu kama hawa kwanini usiwaweke kundi moja na wachawi wa mabadiliko?kabla hujanyoosha kidole kwa jpm kuhusu ubaguz na chuki ebu jichunguzen je mbahubiri upendo na mshikamano?Ni upinzan huuhuu umejipa legitimate ya kila wanachoongea wao ni sahihi na ndo maoni ya watanzania wote na atakaye pinga basi HAJITAMBUI mara ANAJIPENDEKEZA na kejeli kibao.Ni upinzan huuhuu kila kauli yyt ya jpm hata iwe simple kivip lazima ibadilishwe ktk mfumo ambao mwananchi aichukie serikal. Mfano tu kauli ya kuishi ka mashetani pale alipokuwa akiongelea wale wanaopokea mishahara hadi mil 40 huku kuna watu wanapokea lak 3.kauli imebadilishwa na kuwa kila mtanzania ataishi kama shetan na kila jambo likitokea watanzania wanaambiwa alisema mtaishi kama mashetani. Kwa maoni yangu wanaoongoza kwa kutangaza na kueneza chuki ktk jamii ni wapinzan wenyewe.
NI WAKATI SASA UPINZANI UJITAFAKARI NINI WAJIBU WAO KATIKA KUHUBIRI AMANI NA UPENDO kati ya jamii na jamii na jamii na serikal. Huwez simama ukaanza kuongelea ukabila au ukanda na bado ukasem ww ni mtetezi wa wanyonge. Ni mengi mno upinzan unafeli ila kwakua WAMEJIWEKA KUNDI LA MALAIKA NDO MAANA KWA AKILI YA KAWAIDA HUWEZI ONA JINSI GANI UPINZAN NI KIONGOZI WA KUHUBIRI CHUKI KATIKA JAMII
posti fromu Nokia kitochi yuzingi jamii forum
Na ndo chuki mnazoendeleza. U
Alafu kwa unafiki wao wanahubiri uzalendo na mshikamano wa kitaifa.Unaambiwa yanayotendwa na ccm hata Mwovu Shetani kapigwa ganzi kwa mshangao !
Mimi huwa napata shida sana kusema, "Raisi wetu." Nafsi inagoma kabisa.Umeongea vitu vya ukweli mtupu by 100%
Huu Umoja wa Taifa letu ambao alituachia Mwalimu Nyerere unamomonyolewa kwa kasi ya kutisha na huyu Rais wetu wa sasa.
Matamko yake ya chuki ndiyo yanaleta ufa mkubwa sana.
Kama ulivyosema ni jambo la hatari sana kwa Rais wa nchi kumsifu Spika wa Bunge kutokana na uonevu wa wazi anaowafanyia wabunge wa upinzani bungeni kwa kuwatimua pasipo sababu za msingi......
Na yeye Rais wa nchi anadiriki kutamka hadharani akimsifu na kumwambia Spika utakapomaliza "assignment" yako ya kuwatimua wabunge wa upinzani kule Bungeni, niachie na mimi huku "uraiani" nishughulike nao!
Tumeshuhudia wabunge wote wawili Halima Mdee na Esther Bulaya wote wakikamatwa na kuwekwa ndani na Polisi kwa kile kinachoonekana wazi kuwa ni maelekezo toka juu......
Hebu tujikumbushe moja ya hotuba muhimu ambayo aliitoa Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake aliposema kuwa hatukuwaita wazungu wa Afrika Kusini makaburu kutokana na rangi yao nyeupe, la hasha.......
Mwalimu akaendelea kueleza kwenye hotuba yake hiyo kuwa mtu yeyote anayefanya mambo ya kibaguzi hata awe mtu mweusi naye ni kaburu tuu.....
Kutokana na vitendo vinavyofanywa na watawala wetu wa awamu ya 5 sisi wananchi tunapaswa kuwaita viongozi wetu hao kuwa ni makaburu tuu.......
Kitu ambacho pia viongozi wetu wanaofanya ubaguzi huu wa kutisha sijui kama wanajua madhara makubwa sana watakayolisababishia Taifa letu kwa siku za mbeleni?
Kwa kuwa haiingii akilini kwa mfano mtu kama Humphrey Polepole aweze kuzunguka nchi nzima na afanye mikutano mbalimbali ya kisiasa na Polisi wanamuachia bila kumkamata......
Lakini Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi wa Bunda Esther Bulaya anapoenda kwenye Jimbo jirani la Tarime kwenda kushiriki kwenye uhamasishaji wa harambee, akamatwe na Polisi kutokana na kutii agizo la Rais aliposema kila Mbunge anapaswa kufanya mikutano ya kisiasa kwenye Jimbo lake pekee!
Hivi hao Polisi wanaweza kututajia ni Ibara ipi katika Katiba ya nchi yetu inayowawekea mipaka ya kufanya siasa wabunge wa upinzani?
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3(1) inaeleza wazi kuwa nchi yetu itakuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa na katika kufanya shughuli zao za kisiasa vyama hivyo, hakitakiwi chombo kingine chochote kuingilia shughuli zao za kisiasa.
Sasa tumuulize Rais wetu na Jeshi letu la Polisi, mbona wanaamua kuivunja waziwazi Katiba ya nchi yetu?
Hivi tukiyasema hayo ambayo ndiyo ukweli mtupu nyinyi mapolisi mtatuita wachochezi na kutulazimisha kwenda kutupima mikojo yetu!?
Ila Rais wetu na Jeshi letu la Polisi mjikumbushe msemo mmoja unaosema MWISHO WA UBAYA AIBU..........
Huu ni ujinga wa hali ya juu ambao Taifa hili halijawahi kuushuhudia tokea tupate Uhuru ......Hiyo lugha ya wahamiaji haramu ni sahihi kabisa,kwa akili ya kawaida watu wa Tarime wanajisikiaje kusikia Bulaya aliyekuja kuhamaisha uchangiaji maendeleo kakamatwa,kisa kashiriki mkutano jimbo jirani.huu ujinga namna ngapi?
Kwa mfano hiyo no 5 ya kushikiana bastola hadharani........Hii nchi imekuwa ya ajabu sana msimu huu.
1.Majanga
2. Pesa
3.Siasa
4.Vifo vya kutisha
5. Kushikiana gun hadharani
6.Vipimo vya ajabu eg. Kojo
Heri tukaishi Vietnam maana Zimbabwe watafika tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Na kitu cha kutisha zaidi ni kuwa huyo mtu anadiriki kuleta unafiki kwa kuwaomba waTZ eti wamuombee kwa Mungu!?Alafu kwa unafiki wao wanahubiri uzalendo na mshikamano wa kitaifa.
Never ever!!
Very true Mkuu Erythrocyte.Unaambiwa yanayotendwa na ccm hata Mwovu Shetani kapigwa ganzi kwa mshangao !
Very trueMwisho wa ubaya ni aibu
Ova
Hawana tena hoja za kuwaambia wananchi.jino kwa jino wamebaki kutumia mabavu hawana tena ushawishi kwa wananchi