Kinachoendelea nchi hii ni Ubaya kwa Ubaya

Kinachoendelea nchi hii ni Ubaya kwa Ubaya

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,530
Reaction score
139,817
Bila shaka wote tunafahamu ni nani ametufikisha hapa! Jamii zinafanyiana ubaya-ubaya. Ubaya unalipwa kwa ubaya!

Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala inayiendekea juu ya matukio ya kisiasa na kijamii yanayiendelea nchi hii. Kwa ufupi naweza kusema nchi imepoteza kabisa mshikamano.

Tumekuwa kama familia maadui na mahasimu kiasi kwamba kila familia inaiombea nyingine majanga au ishindwe katika jambo fulani.

Tumefikaje katika hatua hiyo?
Wapinzani na wafuasi wao wamejengewa chuki na serikali iliyopo madarakani. Serikali iliyopo madarakani imewafanyia wawakilishi wao ubaya.......imewabeza,imewafunga,imewadharirisha,imewatukana na kuwanyima haki zao za kikatiba! Wapinzani wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao,kila wanachosema kinabezwa!

Lakini kubwa zaidi na linalouma ni kudhalilishwa na kufanyiwa ukandamizaji wa hali ya juu. Hili limeleta chuki kubwa sana.

Hata sharia ya makosa ya mitandao utekelezaji wake umekuwa wa kibaguzi. Wanaokamatwa ni wale wanaomkashifu Magufuli na CCM. Lakini Lowasa,Mbowe,Lissu,Maalimu Seif wanakashifiwa na kutukanwa sana. Hapo ndipo wafuasi wa niliowataja hapo juu wanaona kumbe sheria zinatungwa kibaguzi kama wakati wa makaburu South Afrika.

Mfuasi wa Tundu Lissu hawezi kuwa tayari kuiunga mkono serikali wakati unamtesa na kumdhalilisha mwakilishi wake. Mfuasi wa Bulaya na Heche anaona uonevu anaofanyiwa mbunge wake,hivyo amejengewa chuki ya hali ya juu sana. Serikali ikishindwa kwake ni furaha.

Serikali ielewe kwamba hivi ndivyo namna magaidi wanavyozaliwa,Boko Haram na Alshabaab ndivyo ilivyoanza,jamii moja kuona inaonewa na nyingine.

Maana yake ni kwamba Serikali imekuwa ikilazimisha mshikamano wakati matendo yake ni kinyume.

Wakati upinzani ukiomba intelijensia za nje kama CIA isaidie kumtafuta Ben Saanane serikali inasema hapana,hapo unategemea wafuasi wa Ben,wafuasi wa upinzani na ndugu wa Ben wanaitafasiri vipi serikali?

Rais Magufuli na dola ionekane ikitenda haki badala ya kusema tu wananchi waiunge mkono serikali!Binafsi naona kuna mambo serikali inafanya poa,lakini ninapooana wapinzani wananyanyaswa namna hii,najikuta sioni cha kuipongeza serikali,yoote yanakuwa yamemezwa kwenye uonevu

Maoni ya Mdau
That is very true

Na huyu jamaa ndiye atakayesababisha nchi iingie kwenye machafuko kutokana na tabia yake ya kuwa-treat viongozi wa upinzani kama wakimbizi haramu ndani ya nchi hii.

Hivi anawezaje kuwaagiza Polisi wake kwa mfano wamkamate Mbunge wa Bunda Esther Bulaya eti kwa kile ambacho anakiita kuwa yeye hataki mbunge wa upinzani wa Jimbo Fulani kwenda kujiunga na mbunge mwingine wa Jimbo lingine kufanya shughuli za harambee!

Hao Polisi wetu tunawaomba watutajie ni Ibara ipi ndani ya Katiba ya nchi yetu inayokataza Mbunge wa Jimbo Fulani kwenda kuungana na mbunge mwenzake wa Jimbo lingine kwa ajili ya kufanya harambee ya shughuli za maendeleo?

Hivi unyanyasaji wote anaowafanyia wapinzani, bado akisimama majukwaani anafanya unafiki wa hali ya juu kuwa eti yeye ni Rais wa watanzania wote na habagui mtu kutokana na Imani yake ya dini au itikadi yake ya kisiasa!

Lakini ambacho tunapenda kumtahadharisha Magu ni kuwa Mungu huwa hafanyiwi usanii, na yeyote anayefanya hivyo huwa anamshushia mapigo ya hali ya juu.

Mapigo mengine tayari tumeshaanza kuyaona yameshaanza kushushwa kama hilo la kukamatwa kwa Bombardier yetu huko Canada.
 
Bila shaka wote tunafahamu ni nani ametufikisha hapa! Jamii zinafanyiana ubaya-ubaya. Ubaya unalipwa kwa ubaya!

Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala inayiendekea juu ya matukio ya kisiasa na kijamii yanayiendelea nchi hii. Kwa ufupi naweza kusema nchi imepoteza kabisa mshikamano.

Tumekuwa kama familia maadui na mahasimu kiasi kwamba kila familia inaiombea nyingine majanga au ishindwe katika jambo fulani.

Tumefikaje katika hatua hiyo?
Wapinzani na wafuasi wao wamejengewa chuki na serikali iliyopo madarakani. Serikali iliyopo madarakani imewafanyia wawakilishi wao ubaya.......imewabeza,imewafunga,imewadharirisha,imewatukana na kuwanyima haki zao za kikatiba! Wapinzani wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao,kila wanachosema kinabezwa!

Lakini kubwa zaidi na linalouma ni kudhalilishwa na kufanyiwa ukandamizaji wa hali ya juu. Hili limeleta chuki kubwa sana.

Mfuasi wa Tundu Lissu hawezi kuwa tayari kuiunga mkono serikali wakati unamtesa na kumdhalilisha mwakilishi wake. Mfuasi wa Bulaya na Heche anaona uonevu anaofanyiwa mbunge wake,hivyo amejengewa chuki ya hali ya juu sana. Serikali ikishindwa kwake ni furaha.

Serikali ielewe kwamba hivi ndivyo namna magaidi wanavyozaliwa,Boko Haram na Alshabaab ndivyo ilivyoanza,jamii moja kuona inaonewa na nyingine.

Maana yake ni kwamba Serikali imekuwa ikilazimisha mshikamano wakati matendo yake ni kinyume.

Wakati upinzani ukiomba intelijensia za nje kama CIA isaidie kumtafuta Ben Saanane serikali inasema hapana,hapo unategemea wafuasi wa Ben,wafuasi wa upinzani na ndugu wa Ben wanaitafasiri vipi serikali?

Rais Magufuli na dola ionekane ikitenda haki badala ya kusema tu wananchi waiunge mkono serikali!Binafsi naona kuna mambo serikali inafanya poa,lakini ninapooana wapinzani wananyanyaswa namna hii,najikuta sioni cha kuipongeza serikali,yoote yanakuwa yamemezwa kwenye uonevu
Serikali haitaji pongezi za wasaliti mkuu!!
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU umesema kweli tupu..

Huyu aliyeingia awamu hii amekuja kuvuruga ule mshikamano na upendo uliokuwepo miongoni mwa Watanzania..

Yeye ajiulize kwanini watu wakimuona JK leo hii wanamshangilia na kumlilia..??!

Ni kwasababu JK alipenda watu wake. Wapinzani na wana CCM wote kwake ilikuwa sawa. JK anapendwa na watanzania sio kwasababu alikuza uchumi au huduma za kijamii, la Hasha..
Ni UPENDO wake kwa watanzania..

Natoa mfano mmoja ulio hai..
Bomoabomoa inayofanyika hivi sasa Maeneo ya Kimara na Mbezi along Morogoro Rd ilikuwa ifanywe na Jpm akiwa Waziri lakini JK alikataa.
Huyu alikuwa na UTU.
JPM hana chembe ya utu.

Mkuu wa Nchi unawezaje kumpa maelekezo kwenye public Spika wa Bunge aende akawashugulikie wabunge wapinzani Bungeni??
Unategemea Mwananchi wa Ikungi anapotoka Lissu akisikia Kiongozi wake anashugulikiwa bungeni kwa maelekezo ya Rais kwa Spika ataipenda serikali??

Huyu ni mbaguzi na amekuja kuharibu kabisa umoja wa watanzania.
 
Watanzania jengeni utamaduni wa kupima kojo bila shuruti. CCM oyee
 
kwa tunapo endea watu watafunga na kuombea mabaya tu, liwalo na liwe maana kuna kundi lina hisi hii nchi ni yao.

mambo yakichacha wanajivua uhusika na kuanzisha wimbo wa "uzalendo"
 
Mheshimiwa Magufuli anatakiwa alete umoja katika jamii, asibague watu kwa itikadi zao, kitu anatakiwa atende haki na asikilize wapinzani wanasema nini, maombi ya upinzani sio ya kudharau, haya mambo ya kuwafunga mara kuwazuia wasifanye mambo ya mikutano yanaleta chuki katika jamii, suala Zima la umoja na ushirikiano katika jamii Kwa kweli Mh Rais hafanyi vizuri.
 
Back
Top Bottom