Bila shaka wote tunafahamu ni nani ametufikisha hapa! Jamii zinafanyiana ubaya-ubaya. Ubaya unalipwa kwa ubaya!
Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala inayiendekea juu ya matukio ya kisiasa na kijamii yanayiendelea nchi hii. Kwa ufupi naweza kusema nchi imepoteza kabisa mshikamano.
Tumekuwa kama familia maadui na mahasimu kiasi kwamba kila familia inaiombea nyingine majanga au ishindwe katika jambo fulani.
Tumefikaje katika hatua hiyo?
Wapinzani na wafuasi wao wamejengewa chuki na serikali iliyopo madarakani. Serikali iliyopo madarakani imewafanyia wawakilishi wao ubaya.......imewabeza,imewafunga,imewadharirisha,imewatukana na kuwanyima haki zao za kikatiba! Wapinzani wamekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yao,kila wanachosema kinabezwa!
Lakini kubwa zaidi na linalouma ni kudhalilishwa na kufanyiwa ukandamizaji wa hali ya juu. Hili limeleta chuki kubwa sana.
Hata sharia ya makosa ya mitandao utekelezaji wake umekuwa wa kibaguzi. Wanaokamatwa ni wale wanaomkashifu Magufuli na CCM. Lakini Lowasa,Mbowe,Lissu,Maalimu Seif wanakashifiwa na kutukanwa sana. Hapo ndipo wafuasi wa niliowataja hapo juu wanaona kumbe sheria zinatungwa kibaguzi kama wakati wa makaburu South Afrika.
Mfuasi wa Tundu Lissu hawezi kuwa tayari kuiunga mkono serikali wakati unamtesa na kumdhalilisha mwakilishi wake. Mfuasi wa Bulaya na Heche anaona uonevu anaofanyiwa mbunge wake,hivyo amejengewa chuki ya hali ya juu sana. Serikali ikishindwa kwake ni furaha.
Serikali ielewe kwamba hivi ndivyo namna magaidi wanavyozaliwa,Boko Haram na Alshabaab ndivyo ilivyoanza,jamii moja kuona inaonewa na nyingine.
Maana yake ni kwamba Serikali imekuwa ikilazimisha mshikamano wakati matendo yake ni kinyume.
Wakati upinzani ukiomba intelijensia za nje kama CIA isaidie kumtafuta Ben Saanane serikali inasema hapana,hapo unategemea wafuasi wa Ben,wafuasi wa upinzani na ndugu wa Ben wanaitafasiri vipi serikali?
Rais Magufuli na dola ionekane ikitenda haki badala ya kusema tu wananchi waiunge mkono serikali!Binafsi naona kuna mambo serikali inafanya poa,lakini ninapooana wapinzani wananyanyaswa namna hii,najikuta sioni cha kuipongeza serikali,yoote yanakuwa yamemezwa kwenye uonevu