Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Status
Not open for further replies.
Waziri anaelipwa kwa kodi za wananchi
Anathubutu kutangaza Leo et CDM
Itakuwa imekufa kabla ya pasaka
Eti mwakajana mipango Yao ya kiuwaji ya
Kukiua haikupangwa vizuri Mimi
Nadhani watanzania imetosha kunyamaza
Kwa tamko hili tu ni tayari tumeshaona
Matumizi ya kodi zetu jinsi yatakavyo tumika
Tukatae huu ni ufisadi mbaya kodi nitoe kwa
Matumizi ya kuua matumaini yangu! Tuseme
Hapana. Kwa vitendo
 
Tangu lini ukawa upande wa Zitto? huo ndio unafiki mbaya kuliko wote, huko ni kuchochea migogoro ili mfaidike na mpate cha kusema, eti uko upande wa Zito? CCM uwe upande wa Zito leo? You arent serious Mpwa. Na nimesema kama Mbowe ni fisadi si tuna vikao na si muda utafika pia? sasa hayo ya Mbowe si yamesemwa jana ulitak leo hii tayari vikao vikae na iamuliwe unavyotaka wewe? kumbuka huyo unaesema uko upande wake ishu zake zilianza ever since sio kwamba leo ndio zimechipua ghafla kama uyoga, mind you
Nadhani hapa Newton third law of motion ina fanya kazi yake. Zitto kasemwa sana na wewe ukiwa mmojawapo na muda wote huo kanuna tu hakuwa anajibu. Yale aliyokuwa anasemwa nayo ndio yanamhukumu katika mass na kwenye vikao vya ndani vya chama kuna mengine. Huu ni wakati wa kuonyesha kwamba Zitto is not a pushover kama anavyosema mwenyewe. Kama ni madhaifu anayo lakini haiwezekani madhaifu yake yamfukuzishe uwanachama lakini wenyewe madhaifu yaleyale waendelee kuhukumu wenzao. Waliotumia nguvu kumchafua nawao wakubaliane na majibu ya Zitto. Mimi niko upande wa Zitto kwenye hili. Wanafiki ni lazima wasemwe wazi na sio kuchagua kuchagua. Mbowe kahongwa na Nimrodi Mkono kuuza jimbo nae kukubali hadharani. Kahongwa na Rostam Azizi kakubali. Why Zito na sio Mbowe? Nakubaliana na wewe kuwa taifa lina mambo mengi ya kujadili lakini wanaopelekea mambo hayo kuwa mabaya ni hawahawa tuwanyamaziao na kuwaona wengine ni waovu. Mtizamo wangu.
 
NIjuavyo mimi CHADEMA ina wafuasi wengi Njia ya Morogoro ROAD, bagamoyo Road, KIsarawe Road(kw amana ya Nyerere Road) na Kidogo KIGAMBONI,


Sasa hawa wanao tokea TMK, BUGURUNI, TANDIKA, MWEMBEYANGA ni wanachama wa wapi?
Namini sote twajua ni chama gani chenye wafuasi huko.

by the way wanachama na viongozi wa CHADEMA walishaonywa kujihusisha na ZITTO.
 
Kweli naweza kuwa mtot but mwenye busara kuliko wewe, mimi nime-argue na wewe weka argument zako basi, kusema sijui kichaa gani kasema Chadema itakufa!!! that is nonsense, sema wewe hoja zako ni zipi? za kwangu ndio hizo, ni za kitoto au kizee lakini za kwangu ndio hixo na ndio ninachokiamini, za kwako ziko wapi tuzijadili? Seeds of destruction? Hii misamiati ya kukokoteza hiii itawaponza wengi, haya nendeni mahakamni, but Your Man belongs to the past.
Du!a
Watu wengine mna analyse mambo utafikiri ni watoto wa chekechea!!!

Hata baada ya Wassira kusema hadharani kuwa CDM lazima ife kabla ya 2015 bado hamkumwelewa.
You guys planted your own seeds of destruction, na tatizo kubwa mnashindwa kuappreciate the fact that makosa mengi sana yako kwenu.

CCM haikuwatuma kina Mbowe Dubai, wala kula ruzuku, wala kuonana na Mkono kwa mshiko.
 
Nawezakubali kwamba zzk ana wafuasi wengi sana nchini, waislam na wakrito, kwanini anang'ang'ania chadrma cha kidini na kikabila??? Nakushauri kaka yangu zitto anzisha tu chama hujachelewa kuliko kujidhalilisha na kubishana bila muafaka.
 
Tatizo hawajui siasa zinavyochezwa.

Endapo Zitto atashinda mahakamani,Chadema ya Mbowe/Slaa katu hawataitisha Baraza Kuu ili kusikiliza rufaa ya Zitto kwani ni risk kubwa kwao wakati Zitto atakuwa hana cha kupoteza.Na Zitto akipewa nafasi hiyo ni wazi atatumia hoja nzito zinazonung'unikiwa na wajumbe hao kujenga hoja ya kuwatenganisha na viongozi hawa na wajumbe wa Baraza Kuu na hivyo kuongeza kasi ya kuparaganyika kwa chama.Na kumbuka kumuondoa Zitto kunahitajika theruthi mbili ya kura za siri za wajumbe,what if hazitafika?ni risk kubwa isiyopaswa kujaribiwa na Mbowe/Slaa.

Pili,baada ya Chadema kutoitisha baraza na hivyo kumuachia Zitto uanachama,au kuitisha Baraza na Zitto kuwavuta baadhi ya wajumbe wa Baraza.Hatua ya pili ni kwa Zitto kuanzisha au kujiunga na chama kingine na kushiriki kwenye shughuli zote za kukijenga na kukiimarisha chama hicho ikiwepo vikao na mikutano ya nchi nzima lakini bila kurudisha kadi ya Chadema.Hii itamwezesha pamoja na kukijenga hicho chama lakini pia kuendelee kutumia jukwaa la Bunge kuonyesha uwezo wake wa kuwatetea wananchi Bungeni na kutoa mbadala wa upinzania wa kweli ndani na nje ya Bunge.

Hivi ndivyo walivyofanya Uhuru Kenyatta na William Rutto kwa kuanzisha vyama vyao vya TNA na URP huku wakiendelea na ubunge wao kwa vyama vya ODM na KANU respectively.Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kulitikisa Bunge,hivyo atakuwa na nafasi nzuri kupitia Bunge sio tu kutoa hoja za kutetea wananchi na nchi lakini pia kujijenga mwenyewe na chama chake.

Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kuwaunganisha wapinzani wengine wote Bungeni,na ana uwezo wa kuwavutia au kuwalazimisha kwa shinikizo la umma Wabunge wa CCM na Chadema kukubaliana na hoja zake,na mwishowe kuonyesha uongozi wake ambao Mbowe hana uwezo wa kuuonyesha Bungeni.Hivyo

Chama cha Zitto kina nafasi nzuri ya kujenga timu kubwa na nzito kuelekea 2015 na ata kuchukua dola kama CCM itagawanyika,maana ikigawanyika wataotoka hawatakwenda kwa chama-kampuni(Chadema) bali kwa chama cha kidemokrasia chenye kukubali mabadiliko(Zitto).Nauona mwisho wa zama ya Chadema na mwanzo wa Zitto aliyekomaa mwaka 2015.

Na hii ndiyo njia ninayodhani anapaswa Zitto aipitie kuelekea 2015.

Weeeewe!! Chunga hiyo maneno yako wewe.
Hapana fananisha Uhuru/Ruto na hii ghasia yenu Zitto.
Hii mtu Uhuru iko kwa system tangu tumboni ya mama yake na vilevile iko na chapaa mob hata Ruto iko namna ile chapaa mob.
Halafu Kenya tunaenda tafuta mtu kwa kabila yake, Kikuyu iko kabila kubwa na iko na chapaa mingi.
Sasa hiyo maneno vile wewe unasema kwamba eti zitto atajenga hoja ya kukubalika bungeni akiwa na Chama yake mpya halafu CCM imuangalie tu wakati kule CCM iko mafisi maji mingi inayotaka Urais, weeee.
Labda CCM imchukue na imfanyie kampeni kitu ambacho wakongwe wa chama wanaotaka urais watakataa au walikubali ujue lazima wahujumu chama. Zitto alitakiwa aanze hizo harakati muda mrefu na awe amejitoa CDM muda ili atengeneze nrtwork yake vizuri lkn hii ya kupitia mgongoni kwa CDM(Ubunge, umaarufu bungeni) na CCM(kupata chapaa) ili awe na chama chake sidhani kama itafanya kazi
 
Last edited by a moderator:
TAAHADHARI
Wapo kundi la vijana ambao ni wakutengenezwa nasikia wanasubiri tukifika HC waje kuanzisha fujo wajidai wanadai hela kutoka kwetu, eti tumewanunua n hatujawlipa..ninachosema hakuna anaetudai.[/QUOTE]

Na hawa jamaa ni mafundi wa kutengeneza fitna.........unakumbuka yule jamaa yao wa arusha kaenda kuanzisha fujo chuoni...pembeni akatengeneza video eti anahimiza wanafunzi waache fujo........kuna mwingine akatumia njia hiyohiyo kule mwanza.........na jana tumewasikia wakilia na jamaa wa CUF...eti wanagawa t shirt za chadomo.....achilia mbali ile DVD anayotembea nayo Mbowe kwamba ni ushahidi wa bomu......picha wamepiga wo..wamehariri wao........ni usanii full......

Hawa jamaa wameshajiaminisha kuwa watanzania ni mfala wa kulaghaiwa watakavyo.
 
Najua chadema wengi mnanidharau, ila mtaniheshimu tuu. Nimependekezwa bunge la katiba.. Nyota yangu inawaka

Unatia hasira, you are provocator and that will not help you. Mkakati wenu kuiangusha cdm but you won't reach your goal. Utaheshimiwa kwa lipi? ccm kubaki madakani wakiiba malihasili zetu? You will not.....unajichosha bure. CDM ingini kubwa. the good think mlishasema 2013 cdm itakufa so you are working along that line and and we do against.
 
Tatizo hawajui siasa zinavyochezwa.

Endapo Zitto atashinda mahakamani,Chadema ya Mbowe/Slaa katu hawataitisha Baraza Kuu ili kusikiliza rufaa ya Zitto kwani ni risk kubwa kwao wakati Zitto atakuwa hana cha kupoteza.Na Zitto akipewa nafasi hiyo ni wazi atatumia hoja nzito zinazonung'unikiwa na wajumbe hao kujenga hoja ya kuwatenganisha na viongozi hawa na wajumbe wa Baraza Kuu na hivyo kuongeza kasi ya kuparaganyika kwa chama.Na kumbuka kumuondoa Zitto kunahitajika theruthi mbili ya kura za siri za wajumbe,what if hazitafika?ni risk kubwa isiyopaswa kujaribiwa na Mbowe/Slaa.

Pili,baada ya Chadema kutoitisha baraza na hivyo kumuachia Zitto uanachama,au kuitisha Baraza na Zitto kuwavuta baadhi ya wajumbe wa Baraza.Hatua ya pili ni kwa Zitto kuanzisha au kujiunga na chama kingine na kushiriki kwenye shughuli zote za kukijenga na kukiimarisha chama hicho ikiwepo vikao na mikutano ya nchi nzima lakini bila kurudisha kadi ya Chadema.Hii itamwezesha pamoja na kukijenga hicho chama lakini pia kuendelee kutumia jukwaa la Bunge kuonyesha uwezo wake wa kuwatetea wananchi Bungeni na kutoa mbadala wa upinzania wa kweli ndani na nje ya Bunge.

Hivi ndivyo walivyofanya Uhuru Kenyatta na William Rutto kwa kuanzisha vyama vyao vya TNA na URP huku wakiendelea na ubunge wao kwa vyama vya ODM na KANU respectively.Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kulitikisa Bunge,hivyo atakuwa na nafasi nzuri kupitia Bunge sio tu kutoa hoja za kutetea wananchi na nchi lakini pia kujijenga mwenyewe na chama chake.

Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kuwaunganisha wapinzani wengine wote Bungeni,na ana uwezo wa kuwavutia au kuwalazimisha kwa shinikizo la umma Wabunge wa CCM na Chadema kukubaliana na hoja zake,na mwishowe kuonyesha uongozi wake ambao Mbowe hana uwezo wa kuuonyesha Bungeni.Hivyo

Chama cha Zitto kina nafasi nzuri ya kujenga timu kubwa na nzito kuelekea 2015 na ata kuchukua dola kama CCM itagawanyika,maana ikigawanyika wataotoka hawatakwenda kwa chama-kampuni(Chadema) bali kwa chama cha kidemokrasia chenye kukubali mabadiliko(Zitto).Nauona mwisho wa zama ya Chadema na mwanzo wa Zitto aliyekomaa mwaka 2015.

Na hii ndiyo njia ninayodhani anapaswa Zitto aipitie kuelekea 2015.
Aina hii ya ushawishi ndiyo waliyotumia usalama wa taifa kumfanya awe msaliti wa mabadiliko ambayo wananchi wanayataka kwenye yao kupitia CHADEMA.Huku ni kumpotosha Zitto na kuandika vitu ambavyo vinadhihirisha kuwa watu wengi hawamfahamu huyu Zitto wa sasa wamebaki taswira ya Zitto wa Buzwagi,huyu wa sas kwa taarifa yenu ni toy tu la yule wa zamani,huyu keshauza utu wake kwa vipande thelasini vya fedha hana lolote moyoni mwake kwa ajili ya kumtetea common mwananchi,akiibua kitu sasa hivi ni kwa ajili ya kupigia dili si vinginevyo,Zitto is corrupt,he is good for nothing when it comes to an issue of a trustworthy politician we yearn for.
 
Nimependa pale uliposema kuwa jiji la dar linaenda kusimama kwa muda.
Kweli CHADEMA ni baba lao, inaenda kusimamisha jiji la Dar.
Nahisi utakua hujamuelewa. Watakaokwenda kuusimamisha Jiji la Dar-essalam leo ni wafuasi wa Mh.Zitto sio walevi wenzio kama unavyo fikiri.
 
Kuna kauli inasema KAMA HUKUBALIANI NAO JIUNGE NAO hiyo inamana unapokuwa ndani ya kundi alafu huriziki na kilekinacho tendeka kwa suluhisho sio kutoka nikipambana ndani hadi atuwa ya mwisho na mimi namshauri zito asijittowe cdm abaki hadi hatuwa ya mwisho kwni nyinyi ndio mlianza cdm niyawatu wote sio ya slaa wala mbowe na
 
Kila la heri mkuu sixgates mpenda amani tupo pamoja kaka.

Leo wanaccm na maliberal ------------ kadi za cdm na kupewa bendera na Zitto.

Ila ukweli utadhihirika tu leo mkuu wa wachawi ataondoshwa na matunguli yake mchana kweupeeee.
 
Last edited by a moderator:
NIjuavyo mimi CHADEMA ina wafuasi wengi Njia ya Morogoro ROAD, bagamoyo Road, KIsarawe Road(kw amana ya Nyerere Road) na Kidogo KIGAMBONI,


Sasa hawa wanao tokea TMK, BUGURUNI, TANDIKA, MWEMBEYANGA ni wanachama wa wapi?
Namini sote twajua ni chama gani chenye wafuasi huko.

by the way wanachama na viongozi wa CHADEMA walishaonywa kujihusisha na ZITTO.
Mkuu, hata ukisikia kujitoa akili sio kama huku. Nani kakwambia TEMEKE hakuna mwanachama wa CDM? We unafikiri Tandika hakuna Wachaga? Acha hizo bhana.
 
Magetisita tupe update za jiji la Dar kusimama kwa muda coz muda si mrefu huu uzi wako utaisha wachangiaji, tutakuwa tunapata updates from ndani ya mahakama then tutarudi tena baadaee kuangalia jinai mateja walivyokung'utwa mabomu.
 
Du!a
Watu wengine mna analyse mambo utafikiri ni watoto wa chekechea!!!

Hata baada ya Wassira kusema hadharani kuwa CDM lazima ife kabla ya 2015 bado hamkumwelewa.
You guys planted your own seeds of destruction, na tatizo kubwa mnashindwa kuappreciate the fact that makosa mengi sana yako kwenu.

CCM haikuwatuma kina Mbowe Dubai, wala kula ruzuku, wala kuonana na Mkono kwa mshiko.

Macho ya watu yanamakengeza.
 
Mkuu, hata ukisikia kujitoa akili sio kama huku. Nani kakwambia TEMEKE hakuna mwanachama wa CDM? We unafikiri Tandika hakuna Wachaga? Acha hizo bhana.

Nani kakwambia CUF hakuna wachaga
 
Mnajihangisha bure issue ya zitto imekwisha na ni hitoria. Mchukueni mkazihe chamahen nan'ang'ania si yenu. Chapeni lapa haa chenu. Kwisheizzk na washirika wake. Ngoma kiua sana hupasuka mapema
 
Nawezakubali kwamba zzk ana wafuasi wengi sana nchini, waislam na wakrito, kwanini anang'ang'ania chadrma cha kidini na kikabila??? Nakushauri kaka yangu zitto anzisha tu chama hujachelewa kuliko kujidhalilisha na kubishana bila muafaka.

WINNERS DON'T QUIT.......aliyekwambia mwenye hakimiliki ya kubaki hapo Chadomo ni nani ?....washauri kina Mbowe na Slaa wakaazishe chama kingine ...kwani nao si wana wafuasi....

Ondoa ushauri wako wa nguvu za giza hapa....

........WINNERS DON'T QUIT.............
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom