Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Kinachoendelea mitaani kwa ajili ya kumpa support ZZK leo pale H.C

Status
Not open for further replies.
Aina hii ya ushawishi ndiyo waliyotumia usalama wa taifa kumfanya awe msaliti wa mabadiliko ambayo wananchi wanayataka kwenye yao kupitia CHADEMA.Huku ni kumpotosha Zitto na kuandika vitu ambavyo vinadhihirisha kuwa watu wengi hawamfahamu huyu Zitto wa sasa wamebaki taswira ya Zitto wa Buzwagi,huyu wa sas kwa taarifa yenu ni toy tu la yule wa zamani,huyu keshauza utu wake kwa vipande thelasini vya fedha hana lolote moyoni mwake kwa ajili ya kumtetea common mwananchi,akiibua kitu sasa hivi ni kwa ajili ya kupigia dili si vinginevyo,Zitto is corrupt,he is good for nothing when it comes to an issue of a trustworthy politician we yearn for.

Na tatizo kubwa mnadhani Mbowe/Slaa ni malaika na hivyo kudhani kila anayepingana nao ni shetani.Kifupi ni kuwa,Zitto ana mapungufu yake lakini pamoja na mapungufu yake bado Zitto ni bora zaidi kuliko Mbowe/Slaa.
 
Tatizo hawajui siasa zinavyochezwa.

Endapo Zitto atashinda mahakamani,Chadema ya Mbowe/Slaa katu hawataitisha Baraza Kuu ili kusikiliza rufaa ya Zitto kwani ni risk kubwa kwao wakati Zitto atakuwa hana cha kupoteza.Na Zitto akipewa nafasi hiyo ni wazi atatumia hoja nzito zinazonung'unikiwa na wajumbe hao kujenga hoja ya kuwatenganisha na viongozi hawa na wajumbe wa Baraza Kuu na hivyo kuongeza kasi ya kuparaganyika kwa chama.Na kumbuka kumuondoa Zitto kunahitajika theruthi mbili ya kura za siri za wajumbe,what if hazitafika?ni risk kubwa isiyopaswa kujaribiwa na Mbowe/Slaa.

Pili,baada ya Chadema kutoitisha baraza na hivyo kumuachia Zitto uanachama,au kuitisha Baraza na Zitto kuwavuta baadhi ya wajumbe wa Baraza.Hatua ya pili ni kwa Zitto kuanzisha au kujiunga na chama kingine na kushiriki kwenye shughuli zote za kukijenga na kukiimarisha chama hicho ikiwepo vikao na mikutano ya nchi nzima lakini bila kurudisha kadi ya Chadema.Hii itamwezesha pamoja na kukijenga hicho chama lakini pia kuendelee kutumia jukwaa la Bunge kuonyesha uwezo wake wa kuwatetea wananchi Bungeni na kutoa mbadala wa upinzania wa kweli ndani na nje ya Bunge.

Hivi ndivyo walivyofanya Uhuru Kenyatta na William Rutto kwa kuanzisha vyama vyao vya TNA na URP huku wakiendelea na ubunge wao kwa vyama vya ODM na KANU respectively.Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kulitikisa Bunge,hivyo atakuwa na nafasi nzuri kupitia Bunge sio tu kutoa hoja za kutetea wananchi na nchi lakini pia kujijenga mwenyewe na chama chake.

Na kwa kuwa Zitto ana uwezo wa kuwaunganisha wapinzani wengine wote Bungeni,na ana uwezo wa kuwavutia au kuwalazimisha kwa shinikizo la umma Wabunge wa CCM na Chadema kukubaliana na hoja zake,na mwishowe kuonyesha uongozi wake ambao Mbowe hana uwezo wa kuuonyesha Bungeni.Hivyo

Chama cha Zitto kina nafasi nzuri ya kujenga timu kubwa na nzito kuelekea 2015 na ata kuchukua dola kama CCM itagawanyika,maana ikigawanyika wataotoka hawatakwenda kwa chama-kampuni(Chadema) bali kwa chama cha kidemokrasia chenye kukubali mabadiliko(Zitto).Nauona mwisho wa zama ya Chadema na mwanzo wa Zitto aliyekomaa mwaka 2015.

Na hii ndiyo njia ninayodhani anapaswa Zitto aipitie kuelekea 2015.

Nimekusoma kwa utuvu wa hali ya juu sana.
 
kama ana wafuasi wengi na anajiamini kwamba anawanachama wengi..si ni bora akaanzisha chama chake..sasa hivi pale kashaonekana msaliti.hata kama mahakama ikimpatia ushindi haitamsaidia..kama kweli anajiamini aanzishe chama chake na nadhani atapata kuungwa mkono sana na wana ccm..
Zitto sasa hivi amekuwa kama joka la kibisa
 
Mkuu sixgates waambie hao wafuasi wa Zito kuandamana hiyo ni haki yao kisheria. Tena wanatakiwa wawe wengi sana. Ila watambue Zito na CCM sio watu wanaokubaliana na maandamano japo ni haki ya kikatiba. Sasa itakuwa vizuri ili itakapotekea watanzania watakapoamua kuandamaana kuhusiana na kupanda kwa bei ya umeme wasiseme kuna mambo ya kiintelijensia kwani tozo la umeme lina athari ya msingi kwenye maisha ya watanzania kuliko Zito kupata madaraka akiwa chadema.


Waandamane wasiandamane haina tija mkuu hapo ni sawa na 0 x bilioni moja = 0
 
Nahisi utakua hujamuelewa. Watakaokwenda kuusimamisha Jiji la Dar-essalam leo ni wafuasi wa Mh.Zitto sio walevi wenzio kama unavyo fikiri.
Wewe ndio hujaelewa, kwani hao wafuasi wa Mh. Zitto sio CHADEMA?
 
Haya rudini majumbani kwenu mkaendelee na mapumziko pia shughuli nyingine.
Nilikuwa na Jaji muda si mrefu, ameniambia anaenda kutangaza kuwa Hukumu atawatumia wahusika kwenye Emai zao.
 
Du!a
Watu wengine mna analyse mambo utafikiri ni watoto wa chekechea!!!

Hata baada ya Wassira kusema hadharani kuwa CDM lazima ife kabla ya 2015 bado hamkumwelewa.
You guys planted your own seeds of destruction, na tatizo kubwa mnashindwa kuappreciate the fact that makosa mengi sana yako kwenu.

CCM haikuwatuma kina Mbowe Dubai, wala kula ruzuku, wala kuonana na Mkono kwa mshiko.

imeongezeka tena toka 2013 mpaka 2015!
 
Mimi niwashukuru wato Sixgates na Berenya, tuwe wakweli tu na ukweli utatuweka huru, Mimi baada ya kumfuatilia Dr. Slaa nimegundua ni kiongozi ambaye anapokuwa na hasira ni rahisi sana kuchukua maamuzi yasiyo na busara. Kwa Mh.Mbowe nimeona ni mtu ambaye hataki kuachia madaraka hata kama kuwepo kwake madarakanani kunaleta mpasuko. Kiongozi bora ni yule anayekubali kupisha wengine hata kama bado yeye ni bora. Inawezekana Mh. Mbowe hana washauri wazuri ama wapambe wamemzidi.
Sasa tuje kwa Zito, yeye nilikuwa namuamini tena huku akijinadi ni msomi, lakini nimegundua na yeye hana tofauti sana na hao hapo juu. Wakati wa sakata hili ndio ungekua hasa wakati wa yeye kuonyesha ukomavu wake wa kisiasa na elimu yake ionekane, mama yangu we kwa muda wa hizi siku saba baada ya kufanyiwa kile asichokipenda ndio mapungufu yake yote yameonekana. Ameongea mambo mengi sana ambayo kwa wachambuzi wa mambo atajikuta kwenye wakati mgumu huko mbeleni tuendako hata akifanikiwa kuwa mwenyekiti wa cdm kwani naye anaoenana hana uvumilivu na anachukua maamizi ya jazba.
Mimi naomba tena kuhusu Dr. Kitila, wote ni mashahidi toka kuanza kwa sakata hili, Dr.Kitila ndio ameonyesha kuwa ana msimamo, mvumilivu anakubaliana na hoja tofauti na hana jazba. Hatujamuona akijihushisha na makundi yoyote wala ushabiki usio na tija. Kama ni mtu anayefaa kuwa kiongozi wa cdm basi ni huyu Dr.Kitila kwani wote hata tukiweka pande zote mbili hasimu ndiye pekee anayeweza kukubalika kwa upande wa Zitto ama Slaa +Mbowe. Cdm ijitafakari na wakae meza moja tena kwani naamini wagombanao ndio wapatanao na kuheshimiana pia, japo damage waliyoitengeneza kwa muda huu mfupi ni kubwa.
Mimi sitaki kuamini kwamba milango imefungwa kwa Dr.Kitila kurejea cdm. Dr. Kitila anaweza kuomba kurejea tena cdm japo sijui yeye kama yeye atalichukulia hili vipi. Ama viongozi wa juu wa cdm au watu wote wenye ushawishi katika cdm wanaweza kumshawishi arejee na apendekezwe kugombea nafasi za juu kwani naamini kwa mwenendo wake anaweza kuleta utengamano tena cdm. Kila ajikwezwaye atashushwa na ajishushaye atakwezwa. Dr. Kitila tupende tusipende ana mapungufu yake lakini maamuzi yaliyomkuta ya kuvuliwa uanachama yamechangiwa sana kwa mtazamo wangu na emotions and feelings zilizopo chamani kwa sasa kwa watu kuonyeshana ubavu, matokeo yake imekuwa ni vita vya panzi furaha kwa kunguru.
Nikijaribu kuangalia joto walilokuwa wamelipata CCM kutokana na uwezo na ushawishi wa cdm kwa wananchi mpaka wakawa wanachukua hatua chache japo kwa shingo upande, leo hii serekali inapandisha umeme kwa asilimia 85% huku watatetezi wa wananchi yaani Cdm wanaandama saa 3 asubuhi kwenda mahakamani kufanya ushabiki wa kesi yao wenyewe aibu gani hii. Naomba cdm na wanaoitakia cdm mema muingiapo vitandani kulala jiulizeni tena hili jukumu la kutetea wananchi wanyonge wa taifa hili mmeliweka pembeni mmeamua kucheza mechi ya Madrid na Barcelona mahakamani tena wenyewe kwa wenyewe. Mmeruhusu magazeti yetu kubaki yanaongelea upumbavu wa mahakama na kuacha suala la kupanga gas na umeme ambalo linagusa maisha ya wananchi na uchumi wa watanzania wote mnajadili madaraka!!!!
Naongea kwa uchungu suala hili kwani cdm ndio wangalau ilikuwa inatusaidia kupewa majibu ya matatizo yetu na serekali hata kama ni kwa kubabiababia, lakini haidhuru. Leo tunataka madaraka ili tuje tuwaongoze wananchi maskini wasio na elimu, maji safi, afya bora, gesi na umeme juu. Tunamuacha mshindani wetu Ccm akifanya apendalo wakati uwezo wake wa kuongoza umekwisha na sisi wenye afadhali tunagombea madaraka, aibu gani hii!!

Amini usiamini ni CCM hao hao ndio wametengeneza huu mgogoro na hata kuudhamini,ushahidi mdogo angalia wana CCM wanavyotumia nguvu kubwa kupinga maamuzi ya CHAMA MPINZANI na hata press conference baada ya Zitto kuvuliwa vyeo iliandaliwa na kina nani?. Sikutarajia CCM kuihurumia CHADEMA kiasi hiki kwa kukosea kumtimua ZZK....! Wanasiasa hawana tena uzalendo wa kweli.Hawaumwi tena na matatizo yetu kama akina Nyerere. Wengi wao wako kwa ajili ya kulinda maslahi yao pamoja na vikundi vyao. Hii nchi itakuja kuingia kwenye machafuko makubwa sana. Maana naamini itafika wakati wananchi wataamua kuchukua haki zao kwa nguvu baada ya kukosa watetezi wa kweli,dalili zimeshaanza kuonekana. Kila kukicha wanaharakati na viongozi wa dini wanauawa, wanajeruhiwa kwa kun'golewa meno na kucha,wengine wanapigwa mabomu,nyumba za ibada zinachomwa moto. Jeshi la polisi halijawahi kumtia hatiani hata mhusika mmoja wa hayo matukio.Tunaambiwa uchunguzi bado unaendelea,miaka inazidi kutiririka tu hakuna dalili. Hakika nchi hii inaelekea kwenye umwagaji mkubwa sana wa damu.
 
mie kilichoniuma ni kudanganywa na kiongozi mkuu wa chama mbowe (sio mh!)...............kutuambia 'hata ccm wanajua kuwa hana bei' huku mwisho wa cku anakihujumu chama kwa kuuza majimbo, ukiondoa ushabiki - huu ni usaliti wa hali ya juu kabisa!!

Zitto na Mbowe wote wanafanana mkuu...... ila zitto ni hatari zaidi maana harakati zake zimejaa unafiki mwingi sana
 
Mjinga ni mbowe ambaye katangaza na kukiri kuchukua fedha yoyote hata iwe haramu au ya mpinzani wake wakati wa kampeni za uchaguzi-mtendaji mkuu too local(waraka)

huo ni ujinga au hakuwa na njia nyingine?
 
Weeeewe!! Chunga hiyo maneno yako wewe.
Hapana fananisha Uhuru/Ruto na hii ghasia yenu Zitto.
Hii mtu Uhuru iko kwa system tangu tumboni ya mama yake na vilevile iko na chapaa mob hata Ruto iko namna ile chapaa mob.
Halafu Kenya tunaenda tafuta mtu kwa kabila yake, Kikuyu iko kabila kubwa na iko na chapaa mingi.
Sasa hiyo maneno vile wewe unasema kwamba eti zitto atajenga hoja ya kukubalika bungeni akiwa na Chama yake mpya halafu CCM imuangalie tu wakati kule CCM iko mafisi maji mingi inayotaka Urais, weeee.
Labda CCM imchukue na imfanyie kampeni kitu ambacho wakongwe wa chama wanaotaka urais watakataa au walikubali ujue lazima wahujumu chama. Zitto alitakiwa aanze hizo harakati muda mrefu na awe amejitoa CDM muda ili atengeneze nrtwork yake vizuri lkn hii ya kupitia mgongoni kwa CDM(Ubunge, umaarufu bungeni) na CCM(kupata chapaa) ili awe na chama chake sidhani kama itafanya kazi

Kwa kuweka record sahihi,William Rutto ni mtoto wa mkulima,aliyekuwa hana nguzo ya kisiasa ya kumbeba lakini alijijenga kisiasa mwenyewe from no-where kama alivyo Zitto mpaka kufikia kuwa mzizi wa Bonde la Ufa tena kinyume na matakwa ya mkongwe wa huko,Mzee Moi.

Na pamoja na yote,siasa ni mchezo na wanaoujua ndio wanaodumu.Nikirudi hukohuko Kenya,Kuna waliodhani Raila Odinga anajiua kisiasa kwa kwenda Kanu lakini kinyume chake akatoka akiwa nyota zaidi.Aliingia peke yake lakini akatoka na karibu wanasiasa wote wenye ushawishi katika KANU na kunda NARC iliyoiondoa KANU madarakani.Na Tanzania kuiondoa CCM tunahitaji function ileile japo siyo copy and paste.Tunahitaji CCM igawanyike.

Tanzania bado haina chama cha upinzani kinachoweza kuitoa CCM so far,na kwa ukubwa wa CCM huwezi kuitoa madarakani bila kuigawanya kwanza.Na hii ndio catalyst tunayoihitaji Tanzania,Raila wetu,itakayoweza kuwavuta sio wapinzani tu bali pia mpaka wanaCCM wenye ushawishi hasa ukizingatia kama ilivyokuwa KANU mwaka 2002,CCM sasa ina wengi wanaotaka wachukue urais 2015.Na imejaa kutoaminiana ndani yake kuliko wakati wowote wa uhai wake.

Na bahati mbaya Chadema ilivyo sasa haiwezi kutake advantage ya hili.Hakuna mwanasiasa yeyote makini atakayekuwa tayari kwenda kwenye chama chenye "wenyewe" kama Chadema, Chadema inahitaji mabadiliko makubwa kuweza kuwa kweli chama cha wananchi wote na cha kidemokrasia kama jina lake lilivyo.Zitto alikuwa asset kwao lakini kwa kutojua wamebaki kuridhika na mafanikio kidogo waliyonayo.
 
chadema ina wanachama, haina wafuasi mtu, acheni kuwahadaa watanzania, tangulini Zitto akawa na wafuasi Chadema, au unafikili Chadema ni sawa na maccm, umepotea.
 
Nahisi utakua hujamuelewa. Watakaokwenda kuusimamisha Jiji la Dar-essalam leo ni wafuasi wa Mh.Zitto sio walevi wenzio kama unavyo fikiri.

Wafuasi wa Zitto si wanachama wa CHADEMA? Zitto si CHADEMA?
 
UMEONA MBALI
Mbona kama ww ndio unawakusanya na kuwaswaga hao vijana?
Ccm mmejiingiza kwa nguvu cdm.
Alafu wataalamu wa picha watatuambia nani ww maana unaonekana kwenye kioo cha ndani cha gari.

MBONA WANAENDELEA KUFANYA MAKOSA MENGI SANA HAWANA HATA TECHNICALITY EBU ONA MATUMIZI HAYA YA MANENO.
Baada ya hukumu ....................
Picha

Nitaendelea kuwaleteeni taarifa

attachment.php


--------------------------
....................................................................................................
TAAHADHARI
Wapo kundi la vijana ambao ni wakutengenezwa nasikia wanasubiri tukifika HC waje kuanzisha fujo wajidai wanadai hela kutoka kwetu, eti tumewanunua n hatujawlipa..ninachosema hakuna anaetudai.

Ukitizama kwenye Red lugha hiyo inaenda mbali sana kama anavyotafsiri Babalao.Na hiyo kwenye kioo pia anaonekana ni mtoto wa kike mbona wanaratibu mambo yao kitoto pasipo ugumu wowote ambao utampa kazi mwelevu kubutua kinachoendelea.Kwa mwenendo huuu da HURUMA.
 
jobless tz wapo wengi, vinajana wengi wana tumiwa vibaya, Zitto ana watumia vijana kwa maslai yake binafsi.....Zitto ni zaidi ya mchumia tumbo.
 
Hivi sixgates unajipatia riziki kwa shughuri ipi hasa hapa mjini? I mean unafanyakazi saa ngapi?
 
Last edited by a moderator:
Tangu lini ukawa upande wa Zitto? huo ndio unafiki mbaya kuliko wote, huko ni kuchochea migogoro ili mfaidike na mpate cha kusema, eti uko upande wa Zito? CCM uwe upande wa Zito leo? You arent serious Mpwa. Na nimesema kama Mbowe ni fisadi si tuna vikao na si muda utafika pia? sasa hayo ya Mbowe si yamesemwa jana ulitak leo hii tayari vikao vikae na iamuliwe unavyotaka wewe? kumbuka huyo unaesema uko upande wake ishu zake zilianza ever since sio kwamba leo ndio zimechipua ghafla kama uyoga, mind you

Ha ha ha mpwa wangu Elli usikasirike bwana. Mimi nipo upande wa oppressed zinapokuwapo pande mbili (oppresser and oppressed). Sasa kumbe mnavikao vyenu vya ndani mmeshindwaje kuyamaliza mambo ya zitto bila sisi tulioko nje ya chama/saccoss tusijue? Kumbe mkuki mtamu kwa nguruwe sio? Mpwa naipenda nchi yangu na ninawachukia wahujumu nchi wakiwemo mafisadi. Lakini sipo tayari kuiweka rehani mchi yangu kwakuwaruhusu wahuni na wapiga dili waje waigeuze nchi ni mali ya familia yao. Tunaitaki upinzani imara tena wenye sura ya kitaifa lakini sio huu wakichaga na wenye sura ya ubaguzi. Hili ni taifa la watanzania wenye dini tofauti, makabila tofauti, wanaokaa maenen tofauti. Haipaswi kuendekeza siasa za kibaguzi hata kidogo. Wembe unaotumika kumnyolea zito huohuo ndio utatumika kumnyolea fisadi/mlarushwa/mdini/mkanda/namkabila Mbowe. Huohuo ndio utakaotumika kumnyolea mshirikina Slaa(najua utashangaa mpwa) ila ndio hivyo. By the way hujui moyoni mwangu kuna nini dhidi ya siasa ya nchi yangu. Haujui ni kwanini mimi ninaungamkono CCM Pamoja na madudu ya miaka na miaka. Kwahiyo ukiniona nipo upande wa mtu flani jua ni kutokana na mahaba na nchi hii.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom