Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?


rejea "job description"
 
Defensive mechanism ya usimjadili mtu ila hali ime fail.. bandiko limejaa lugha za kinafiki na uoga.

Unajadili ukimya na kumwacha aliekaa kimya? Unazibwa fikira na nakuu!!! Sema wazi yaliyo kukera uwe huru
 
Tuungane na mdau aliye-suggest matembezi ya hisani kila Mkoa kuchangia maafa haya..Mkuu anaonekana na aleji na mikusanyiko..Huenda atajitokeza
 
Kuna hadithi flani inazungumzia maisha ya mzee mbabe na mchawi katika kijiji flani......

"Mzee huyo alikuwa ni mbabe na mpenda sifa na alijiita MTUKUFU jambo ambalo ni kufuru kwa imani ya watu wa kijiji hicho, kwani watu hao waliamini kuwa jina MTUKUFU ni maalumu kwa Mungu wao tu.
Basi wale wanakijiji waliamua kumuomba Mungu wao ashushe adhabu kwa huyu anayemdhihaki.
Siku moja mvua kubwa na radi ya kutisha ilishuka kwenye kijiji hicho. Mvua na radi ile ilikuwa na madhara makubwa kwenye maisha na mali za wanakijiji hao.
Cha kushangaza ni miezi kadha na kadha kupitia bila yule Mzee mbabe na mchawi kuonekana wala sauti yake kusikika.
Siku moja ikaja bainika kuwa mzee huyo mbabe alikuwa amepatwa na Ugonjwa usiofahamika uliomfanya alale tu, kwani viuongo vyote vya mwili vilisimama kufanya kazi.
Kumbe ile mvua na radi zile ilikuwa ni adhabu iliyoshushwa na Mungu wa wale wanakijiji dhidi ya yule mzee mbabe na mchawi."

Mtanisamehe GT wote, kwa kuwapotezea muda kuisoma hadithi hii isiyohusiana na chochote kwenye mada hii.
 
Kwa wale mnaohoji kuhusu ushiriki JPM janga la MAAFA ya KAGERA subirini mshangae jinsi kiongozi huyu mahiri africa atavyowashangaza Watanzania.

Kumbukeni huyu ni mwanasayansi si mwanasiasa. Hapendi uongo na kudanganya watu kwa kujitokeza haraka haraka na kutoa ahadi za uongo. Yeye hufanya kazi zake kwa takwimu na kwa umakini akitanguliza maslahi ya wengi mbele na maslahi yake huyaa acha mbali kabisa.

Wanakagera VUTENI SUBIRA MTAFURAHI sana kipindi kifupi kijacho. Poleni kwa yote mnayopitia kwa sasa. Serikali yetu ni moja na watu wetu ni wa moja. Shida zenu ndio zetu.

Mungu awape uvumilivu muuvuke mtihani huu.

Wenu M2020.
Hapa kazi tu.
 
Ikulu aliyokuwa afikie nayo ilitetemeshwa wako katka ujenzi ikikamilika anaenda
 
Inasikitishana...Tuendelee na maombi tuu..
 
Epushulia mbali..Mkuu hawezi kuwa kaparalaizi bana...Tuendelee kumuombea..
 
Marehemu wote hawana unasaba na vigogo unategemea nini
 
Kimya umekianza wewe kwa kuanza kutosema kimya unachozungumzia ni cha nani.

Mchezo wa vitendawili tega wengine hatuna muda nao kwa sasa.
 
Wakati mwingine nikiona kila ninapotoa kauli zinaleta mkanganyiko na kujadiriwa na international media likitokea linalogusa hisia za watu ni kuwa mpole kwanza ukichota busara na mini hasa la kusema. All in all hata Zambia kulitokeaga ukimya uliokanushwa lakini baadae ikawa public
 
You are not a GT WHY COMMENT?Tuliambiwa Safari imesitishwa ili kwenda kufuatilia hili janga.
 
Jambo hili linafurahisha sana kule Bukoba

Mtoto kala pilipili kwa bahati mbaya akiwa na mama yake jikoni akatoka mbio kwa Muwasho kama yule Usain bolt na kupata hasira akarusha mawe juu ya bati na kutoboa upande vilipo vyumba vya kulala.
Baba yake ni fundi Muashi na mpauaji maarufu pale Bukoba na "inji" nzima lakini jambo la kushangaza na kuteka mioyo ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuomba msaada......

Picha linaendelea mtoto ameanza kutapika mbegu za pilipili wapita njia wanaziokota na kuzibandika nje ya Mikoba yao...tutafika tu.

Nimeiokota sehemu tu hii, c&p
 
Nilichogundua ni kuwa watu wanapenda sana kumsikia kila mara. Akiwa kimya akifanya kazi hawaamini mpaka wamsikie. Hivyo hii inatoa picha kwamba anapendwa sana na wananchi licha ya wanaharakati wa humu kumpigia kelele.
Kwanini aliahirisha safari yake ya Zambia...Press Release ya Ikulu ilisema anaahirisha ili kushiriki na wahanga wa Tetemeko....Mbona sasa hatumuoni..

Well! Kama aliahirisha ili kufanya majukumu mengine na sio la tetemeko, kwanini Ikulu isitishe safari ya Rais kwa kigezo cha Tetemeko..

Tumuombe...
 
Kukaa kimya hakumaanishi kua hatimizi wajibu wake. Au hatua hazikuchukiliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…