Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Kimya Hiki, Is Not Right!, There Must Be Something Wrong Somewhere! Or Am, I Wrong!?

Wakati mwingine ni bora akae kimya tu maana nae hakawii "kuharibu" yule! Hata hili la watanzania kutekwa huko Congo sio dogo kivile.
 
Uso umeumbwa na aibu kina Ruge mzee wa Escrow ndio wenye uwezo wa kuiponya Bukoba ndani ya dakika tu lakini umeshatangaza unataka waishi kama mashetani.

Mabalozi waliambiwa wasiingilie mambo ya ndani wanashangaa wameitwa jumba jeupe kuombwa msaada baba mwenye nyumba haonekani, na mkumbuke wenzetu wazungu ni watu wa kukeep record, bado wana kumbukumbu na walimsikia Baba mtukufu akitamba Tanzania hatutaki misaada, je hata wewe Pasco utaanza vipi kuwaface watu kama hao uliowatambia?

Maskini hana kiapo na Shabaan Robert alituhasa tuweke akiba ya maneno.

Yale mapesa ya MCC zaidi ya dollar millioni 800 tuliyapiga teke leo kumfuata mzungu kumuomba msaada inaweza kusababisha waanzishe research center ya kuzifanyia research akili zetu.

Cha msingi tuendelee kumuombea tu.
Mkuu umemaliza kila kitu hapa.
 
..ukimya huu ulionekana hata siku ya kuchangisha misaada ikulu....btw..kama ilivyokuwa walipoitwa mabalozi ikulu....swali juu ya ukimya huu anatakiwa alijibu Gerson Msigwa....anayetangaza watu kupewa ajira kila leo(teuzi)..huku watumishi walio wengi taifa zima wakiachwa....
 
Naamini kwa dhati kabisa kuna mtu sasa hivi anapitia katika wakati mgumu sana kuliko tunavyoweza kufikiri.Mtu anaweza kujiona mwenye nguvu na mamlaka ya kumpatiliza kila anayemuhisi kuingilia maslahi yake,anaweza kuanzisha vita na kila mtu,lakini kadili anavyozikanyaga haki za wenzake ndivyo naye anavyojiingiza katika vita yake binafsi na nafsi yake.

Ni afadhari mtu ukateswa na maumivu ya mwili kuliko kuteswa na "KARMA", ukiyaruhusu matendo yako yakufikishe hatua ya kuuondoa utulivu wako wa ndani,unakuwa " umejiangika mwenyewe msarabani" na kuiruhusu KARMA isimame kinyume na matendo yako ya kidharimu uliyoyafanya dhidi ya wanyonge na wasio na nguvu ya kujitetea.

KARMA ipo kazini,imesimama badala yetu,inajibu mapigo ya haki kutokana na maneno na matendo ya muhusika.Hili ndilo linaloweza kuwa sababu ya hisia zetu,ngoja tusubiri hatima ya vita hii kuu ya kidhamiri ifanyikayo ndani ya mtu,naamini mpambanaji wetu"KARMA"atatuwakilisha vizuri katika mpambano huu usioonekana.
Much respect Mkuu,karma inajibu malipizi now.
 
Tijifunze kuwa na akiba ya maneno. Ukubwa sio ufahari ni jukumu!
 
Tijifunze kuwa na akiba ya maneno. Ukubwa sio ufahari ni jukumu!
..hili janga la bukoba limetoa funzo kubwa sana kwa mkulu....kelele hazilipi...leo unawabeza watu...alafu kesho unapata janga unawatafuta wakupe misaada....huyu ni Mungu anawaonyesha watu mapito....
 
Waziri mkuu si alishawakilisha Kagera? ikumbukwe Tanzania ina majanga kila siku tena ni mengi mno. sasa huo ukimya mnao question mngependa mtu ajigawanye mara ngapi? jipe mfano wewe na familia yako, ni mara ngapi mmeweza kuwepo kwenye tukio wote kwa pamoja iwe msiba, sherehe, kuona mgonjwa N.K? mimi nahisi Pasco unalo unalolitafuta au unalo unalojua na kama unalo unalojua basi kufwa free ku share nasi. After all sharing is caring. Sambaza upendo mkuu.
Sio lazima kuonekana, hata kutumia runinga kuzungumzia??? ..Yan hata tusimuone mkuu wetu akizungumzia jambo hili .???

Kuna kitu..
 
Tushukuru kwa huu ukimya,
Kwani imesaidia kupungua kwa matamko yasiyo na kichwa wala miguu

ni kweli maana hata mtaani walau amani imerudi mambo ya kurushiana vijembe na mipasho yamepungua sana kwa hii wiki ya ukimya wake
 
Back
Top Bottom