Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

đź“ŤSerikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

đź“ŤKazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.
Aseee!
 
Kilimo Cha kulima kwenye kioo Cha simu na laptop. Wanalima humuhumu kwenye simu mpaka wanavuna na kuuza. Shambani wanakwambia leta hela tukulimie.
 
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Duuuh!

Kumbe kuna wakati fahamu zako huwa zinarejea unaandika vitu vya maana.

Itakuwa ulipata mshauri mzuri wa saikolojia ya akili, mpaka ukawa sawa.

Ahsante kwa ushauri mzuri.
 
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Kuna ulinzi gani kampuni ikisajiliwa ktk soko la hisa
 
Back
Top Bottom