Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,159
- 2,926
Paschal Mayalla
I. UTANGULIZI
Makala ya Paschal Mayala katika gazeti la Nipashe, toleo la Jumapili, tarehe 23 Februari 2025, imenikumbusha matukio ya kisiasa ya mwaka 2022.
Tarehe 20 Mei 2022 viongozi wa Chadema walikwenda kwenye kikao cha majadiliano ya kuimarisha demokrasia na hali ya kisiasa nchini, ambapo walikutana na Rais Samia Suluhu katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Katika mkutano huo, Chadema walibeba hoja zipatazo 10. Hoja hizo ni (1) Katiba mpya, (2) tume huru ya uchaguzi, (3) zuio haramu la mikutano ya hadhara, (4) tiba ya makovu yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 na 2020, na (5) uharamu wa wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema.
Hoja zingine zilikuwa ni: (6) suala la kutopewa ruzuku, (7) usawa wa vyama vya siasa mbele ya sheria, (8) hatima ya watu walioshitakiwa kwa sababu za kisiasa, (9) usalama wa wanasiasa waliokimbilia nje ya nchi, na (10) Umuhimu na Ulazima wa Mabadiliko ya Kimfumo Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wajumbe wa Chadema walikuwa ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohammed, John Mnyika (Katibu Mkuu), na Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge. Na wajumbe wa CCM walikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka.
Mchakato ulioanza 20 Mei 2022 haukuzaa matunda. Ajenda zilizowasilishwa na Chadema zilipigwa teke na CCM bila wao kuleta hoja mbadala ili kusogeza majadiliano mbele. Hatimaye Chadema wakaibuka na sera ya "No Reform, No Election," yaani, "Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi."
Katika muktadha huu, kada wa CCM ambaye ni mwandishi wa habari aliyejitambulisha kwa picha na kwa jina lake halisi la Paschal Mayala, ameandika makala ya kuwashauri Chadema.
Ni makala yenye kichwa cha maneno “Wapinzani wasaidiwe kuachana na siasa za hadaa," yenye maneno 777, na imeambatanishwa hapa chini katika fomati ya PDF na fomati ya picha pia.
Mayalla aliichapisha makala yake katika gazeti la Nipashe, toleo la Jumapili, tarehe 23 Februari 2025, ukurasa wa saba (7), chini ya safu ya “Fikra Mbadala.”
Andiko hili la sasa ni kwa ajili ya kuhakiki hoja ya Mayalla, kuibomoa kisomi na kuifuta kabisa kutoka kwenye uso wa dunia.
Nimeligawanya kwenye sehemu zifutazo: (1) Utangulizi; (2) Ufupisho wa hoja ya Mayalla; (3) Pingamizi dhidi ya hoja ya mayala; (4) Ufafanuzi wa matamko yaliyomo katika pingamizi; (5) Hitimisho na mapendekezo; (6) Kiambatanisho cha maana za maneno: uwezo, uwezekano na ulazima; na (7) Kiambatanisho cha mbinu 200 za kufanya mageuzi kwa kutumia shinikizo la amani.
II. UFUPISHO WA HOJA YA MAYALLA
Kimsingi, hoja ya Mayala inaweza kufupishwa kwenye matamko matano yafuatayo:
- Lissu anapoulizwa kuhusu maandalizi ya uchaguzi ndani ya chama chake yanaendeleaje, anasema kuwa Chadema haifanyi maandalizi yoyote ya uchaguzi kabla ya mabadiliko ya kimfumo, yaani ‘no reform no election’ na sio vinginevyo.
- Lakini, Tundu Lissu na Chadema yake ni "dhaifu" na hawana “uwezo” wa kuzuia uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu wa 2025, iwe ni kwa kujenga hoja sanaifu au kutumia mabavu.
- Kwa hiyo, sera ya “no reform no election” inayohubiriwa na Tundu Lissu ni “siasa za hadaa,” maana haziendani na uhalisia wa kisiasa uliopo nchini Tanzania.
- Siasa ambazo haziendani na uhalisia wa kisiasa uliopo nchini zinapaswa kupuuzwa na kila mtu makini.
- Kwa hiyo, siasa za hadaa kama vile sera ya “no reform no election” zinazohubiriwa na Tundu Lissu zinapaswa kupuuzwa na kila mtu ikiwemo CCM na serikali yake, mpaka hapo wapinzani watakapokuwa tayari kuendana na uhalisia kwa kufanya “real politics.”
Anawataka Chadema "wakumbatie falsafa ya pragmatism," yaani "wawe pragmatic and do what is possible" katika mipaka ya "uwezo" na "udhaifu" walio nao.
Anashauri kuwa Chadema "lazima wajikite kwenye kufanya siasa za ukweli, (real politics) ambazo ni siasa za mikakati ya majadiliano (politics of engagement)" na kujitenga na siasa za makabiliano (politics of confrontation).
Mayalla anatoa wito kwamba, Chadema "wasaidiwe waachane na utopian politics (of confrontation), wafanye real politics (of engagement)."
Hakusema lolote kuhusu ukweli kwamba sera ya "no reform, no election" imezaliwa baada ya Chadema kuweka ajenda ya majadiliano mezani lakini CCM wakaipiga teke na hawakuweka chochote kilicho mbadala katika meza hiyo ya majadiliano hadi leo.
Na hakusema lolote kuhusu ukweli kwamba katika mtazamo wa CCM vyombo vya mabavu ndio BEST ALTERNATIVE TO NEGITIATED AGREEMENT (BATNA) wanayoitegemea pale majadiliano kama haya yanapofeli, wakati Tanzania ni Jamhuri ya Kikatiba na Kidemokrasia.
Wajumbe wa Kikao cha tarehe 20 Mei 2022 kilichofanyika Ikulu ya Chamwino, Ddodoma.
III. PINGAMIZI DHIDI YA HOJA YA MAYALA
Hoja ya Mayala ni potofu kihistoria na kimantiki. Inatosha kuthibitisha hivyo kwa kuonyesha kuwa ama dokezo mojawapo sio kweli au kuonyesha kwamba hitimisho halitokani na madokezo.
Nimechagua kuonyesha kuwa dokezo la pili hapo juu sio kweli, kama nitakavyoeleza hapa chini:
Raia yangu ni kwamba, "uwezekano" wa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025 upo kwa sababu Tundu Lissu na wafuasi wake walioko ndani na nje ya Chadema wanao “uwezo” na "mamlaka" ya kuzuia uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu wa 2025 kwa njia ya kujenga hoja sanifu hata bila kutumia mabavu. Hoja ya Lissu, ambayo inatumia nguvu ya hoja, ni kama ifuatavyo:
- Tangu mwaka 2010 mpaka mwaka 2024 Tanzania tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka tunu za kisiasa zinazojumuisha kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi, katika sehemu kubwa ya vituo vya uchaguzi, na hivyo kuongozwa na serikali haramu kwa sababu ya mchakato haramu wa kiuchaguzi.
- Tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi kwa sababu ya vifungu vibovu vilivyomo kwenye Katiba, sheria, na kanuni za uchaguzi zilizopo.
- Hivyo, bila mageuzi ya Katiba, sheria, na kanuni za uchaguzi hakuna uchaguzi unaoheshimu kanuni za haki, uhuru, ushindani na uwazi unaoweza kufanyika nchini Tanzania.
- Lakini, Watanzania wote wamerithi ahadi ya kuishi katika Taifa ambalo linakuza na kuhami tunu za uhuru, haki, usawa, na uwazi, kwa maana kwamba wanapaswa kupigania tunu hizi kwa hakikisha lwamba kuna chaguzi zinazoheshimu tunu hizi.
- Kwa hiyo, kutokana na nguvu ya hoja inayoambatana na ushahidi usiokanushika, vyombo vinavyotekeleza demokrasia ya uwakilishi, yaani serikali na Bunge, vinapaswa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025 ili kupisha mageuzi ya kimfumo yanayotakiwa na umma wa Watanzania ili umma huo uweze kutekeleza majukumu yake ya kusimika serikali halali kuanzia sasa.
- Umma unayo mamlaka ya kikatiba ya kutumia kanuni za demokrasia ya moja kwa moja, kama inavyotekelezwa kupitia mbinu mbalimbali za shinikizo la amani, kuzuia uovu unaotendwa na serikali kwa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi kupitia mbinu kadhaa inazokubalika na kulindwa kikatiba, yaani "constitutionally protected tools of civil dosobedience."
- Kwa hiyo, kama serikali itapuuzia nguvu ya hoja inayotumika kupendekeza kusogezwa mbele kwa ratiba ya uchaguzi mkuu wa 2025, basi, umma unapaswa kutumia hoja ya nguvu inayotumia njia kadhaa zinazokubalika kikatiba ili kuilazimisha serikali hiyo kukubali kusogeza mbele uchaguzi na kufanya mageuzi husika.
Wajumbe wa Chadema wakiingia kwenye mkutano wa tarehe 20 Mei 2022
IV. UTETEZI WA MATAMKO YALIYOMO KATIKA PINGAMIZI
Utetezi wa tamko la kwanza
Tamko kwamba tangu mwaka 2010 mpaka mwaka 2024 Tanzania tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka tunu za kisiasa linathibitishwa kama ifuatavyo.
Kulingana na taarifa zilizoko kwenye hotuba za Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema, mawazo yafuatayo yanawakilisha msimamo rasmi wa Chadema kuhusu sababu za kaulimbiu ya “Bila Mabadiliko, Hakauna Uchaguzi”
1. Takwimu za uchaguzi wa serikali za mitaa kati ya mwaka 2014 na 2019, kwa mujibu wa Lissu, zinathibitisha kwamba kwa mujibu wa utaratibu wa sasa wa kisheria, kikanuni, kikatiba na wa kiserikali, uchaguzi salama usioambatana na mauaji, ulio huru, wenye uwazi na unaofanyika kwa haki hauwezekani tena kufanyika ktk nchi hii. Takwimu ziko hivi:
(a) Katika uchaguzi wa mitaa na vijiji wa 2014: Jumla ya vijiji vilikuwa 11,748; CCM ilishinda vijiji 9,378 (80%); na CHADEMA vijiji 1,754 (15%). Jumla ya mitaa yote ilikuwa 3,875; CCM ilishinda mitaa 2,583 (67%); na CHADEMA ilishinda mitaa 980 (25.29%).
(b) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa 2019: Jumla ya vijiji ilikuwa 12,262; CCM ikashinda 12,260 (99.99%); na CHADEMA haikutajwa kabisa. Jumla ya mitaa nchini 4,263; CCM ikashinda mitaa 4,263 (100%); na CHADEMA haikutajwa kabisa.
(c) Katika uchaguzi wa vijiji na mitaa mwaka 2024: Jumla ya vijiji ni 12,271; CCM ikashinda vijiji 12,150 (99%); na CHADEMA ikashinda vijiji 97 (0.79%). Jumla ya mitaa ni 4,264; CCM ikashinda mitaa 4,213 (99%); na CHADEMA ikashinda mitaa 36 (0.84%).
2. Takwimu hizi maana yake ni kuwa, mfumo wetu wa uchaguzi wa sasa unayo matatizo mengi, kiasi kwamba, bila kufanyika kwa mabadiliko ya kisheria, kikanuni na kikatiba, kwanza, basi chaguzi za kiinimacho zenye kuwaumiza wapinzani na kuipendelea CCM zitaendelea milele kwa sababu zilizo wazi.
(a) Mosi, chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 zimeweka rekodi za kuenguliwa kwa wagombea wengi wa vyama vya upinzani kwa vigezo visivyo vya kikatiba, mfano kukosea jina, na kukosea kuandika jina la chama. Lakini wagombea wote wa CCM wanabakizwa kwa madai kuwa wao hawana dosari yoyote.
(b) Mfumo wa sasa wa uchaguzi ni mfumo wenye sura ya siasa za chama kimoja. Ulitengenezwa na CCM, kwa ajili ya CCM, unaifaidisha CCM na kwa sababu hiyo si mfumo wa kidemokrasia na unawaumiza wananchi na nchi yote.
(c) Ni mfumo wa CCM kwa kuwa, uchaguzi mkuu unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ambayo ni ya CCM ambayo huteuliwa na kupewa maelekezo na Mwenyekiti wa CCM ambaye mara zote huwa ndiye Rais wa nchi.
(d) Aidha, Mwenyekiti wa CCM ambaye naye mara zote huwa ni mshiriki na mshindani ktk uchaguzi ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume, wajumbe wote wa Tume na mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume. Ndiye mwajiri na mteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo (wakurugenzi wa halmashauri za miji, wilaya, manispaa na majiji), watendaji wa kata na wa vijiji. Katika mazingira haya, hawa kamwe hawawezi kutenda haki Bpbali watampendelea aliyewateua.
(e) Mfumo wa ugawaji majimbo ya uchaguzi sio wa haki kwa kuwa hauzingatii idadi ya watu ambao ni wakazi. Maeneo ambayo CCM ina uhakika wa kushinda imeyagawa katika vijimbo vingivingi Ili mradi iingize wabunge wengi bungeni. Mfano Dar Es Salaam yenye wapiga kura wengi 3,427,000, ambazo ni takwimu za Tume ya Uchaguzi za mwaka 2020, iko sawa na wapiga kura wa mikoa ya Rukwa, Pwani, Songwe, Iringa, Katavi na Njombe kwa pamoja. Lakini DSM ina majimbo 10 tu, sawa na na wastani wa wapiga kura 327,000 kila jimbo la Dar. Lakini, katika mikoa hiyo sita (6) kwa ujumla ikiwa na majimbo 37, kuna wastani wa wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo. Wapiga kura 91,000 katika kila Jimbo kwenye mikoa hiyo ni mara 3.5 ya wapiga kura 327,000 katika jimbo la Dar. Hakuna usawa hapo.
(f) Lissu anaongeza kwamba, kwa upande wa Zanzibar, majimbo ya uchaguzi yana wastani wa wapiga kura 10,000. Hii maana yake ni kwamba mbunge kutoka Zanzibar anaweza kuchaguliwa na watu wasiozidi 2,500 akaja Dodoma na akawa na haki sawa na mbunge anayehudumia wapiga kura 327,000 mkoani Dar Es Salaam. Hakuna usawa hapo.
3. Kwa hiyo, Lissu anasema, hitimisho la ikimantiki ni kwamba, Watanzania tunapaswa kuzuia chaguzi za kiinimacho zisifanyike kwa kujenga hoja kwa wananchi, wanachama wetu, taasisi za kiraia na za kidini, viongozi wa dini, nchi wahisani wa Tanzania, taasisi za haki za kibinadamu za kitaifa na kimataifa hadi waelewe na kutuunga mkono. Hii ndio maana ya msemo kwamba “Mabadiliko Kwanza, Uchaguzi baadaye,” yaani “No Reforms, No Election.
4. Kwa Mujibu wa Lissu, kutokana na hitimisho hapo juu, mapendekezo ya msingi kuhusu mabadiliko yanayotakiwa kufanyika kwa sasa yanapatikana kwenye Ripoti za Tume mbalimbali. Kuna Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991) iliyoundwa na Rais Hayati Ally Hassan Mwinyi; Tume ya Jaji Robert Kissanga (1998) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; Tume ya Jaji Mark Bomani (2003) iliyoundwa na Rais Hayati Benjamin Mkapa; na Tume ya mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Sinde Warioba (2014/2015) iliyoundwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Tume hizi zote zilipendekeza mabadiliko yafuatayo:
(a) Lazima tuwe na Tume Huru ya uchaguzi yenye Mwenyekiti na wajumbe wake wanaoteuliwa na mtu baki badala ya Rais; yenye bajeti inayojitegemea kutoka Bungeni kwa ajili ya kuendesha shughuli zake; yenye wafanyakazi wake wa kudumu na wa mikataba ya muda mfupi/maalumu inayowajiri yenyewe wakiwajibika kwa Tume pekee; na yenye wasimamizi wa vituo vya kupigia kura hadi kwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na wakurugenzi wa Tume wasiowajibika kwa Rais.
(b) Ugawaji wa majimbo lazima ufanyike upya kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu kama ilivyokuwa katika sheria za uchaguzi na katiba kuanzia mwaka 1961 hadi 1991. Kigezo cha miumdombinu na jiografia ya eneo hakifai.
(c) Daftari la wapiga kura litengenezwe upya kwa kuandikisha wapiga kura wote upya kwa kuondoa wapiga kura hewa wote. Aidha, daftari la wapiga kura lisiwe Siri Bali lazima liwe wazi (accessible) kwa yeyote anayetaka kuliangalia Ili mradi kuweka utaratibu rahisi na wa wazi kufanya hivyo.
(d) Utaratibu wa kuengua wagombea wote iwe wa CCM, CHADEMA au chama chochote kwa sababu ambazo si za kikatiba ukomeshwe na kupigwa marufuku na sheria tutakazotunga.
(e) Utaratibu wa vyombo vya dola kuwafanyia vurugu wagombea wa vyama pinzani na CCM upigwe marufuku na sheria na sheria iweke utaratibu wa kuwashitaki, kuwalipisha fidia na kufukuzwa kazi mwenye mamlaka yeyote atakayetumia mamlaka yake vibaya kwenye eneo hili.
(f) Barua rasmi tu ya chama cha siasa ambako wakala anatoka ili kusimamia kura za mgombea wake inatosha kumfanya wakala atambuliwe na msimamizi wa kituo cha uchaguzi. Hivyo, utaratibu wa Sasa wa mawakala wa wagombea wa vyama vya siasa kuapishwa kiapo cha kutunza siri ni batili na hauna sababu na unaleta urasimu usio na maana yoyote kwa sababu kwenye kituo cha kupigia kura hakuna Siri ya kutunzwa hapo kwa sababu kila kitu kinatakiwa kufanyika kwa uwazi huku kila mtu akiona.
(g) Utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kwa nafasi zote kuanzia kwenye kituo cha kupigia kura ufanyike tu pale ambapo mawakala wa wagombea wote wameridhika na kusaini fomu za matokeo. Kwenye kituo cha majumuisho matokeo yatangazwe pale tu ambapo wagombea wote wameridhika na kusaini fomu ya matokeo. Kama mgombea au wakala wa mgombea hajaridhika kwa sababu yoyote sheria iseme ni marufuku kwa msimamizi wa kituo kutangaza matokeo hayo. Na ikitokea hivyo, basi mgogoro wa namna hiyo uende mahakamani kuamuliwa.
Utetezi wa tamko la pili
Tamko kwamba tumekuwa tunafanya uchaguzi unaokiuka tunu za kisiasa linahusu vifungu vya kikanuni, kisheria na kikatiba vifuatazo vinavyopaswa kurekebishwa kwa kuwa vinafunguliaa matapeli wa kisiasa milango ya uhalifu wa kiuchaguzi:
- Kifungu cha 6 cha Sheria ya kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinachomruhusu DED kusimamia uchaguzi kwa njia ya mzunguko;
- Kifungu cha 9 cha sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2024 kinachomruhusu Rais kuteua wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa njia ya mzunguko;
- Vifungu vyote vya Katiba ya nchi (1977) vinavyomruhusu mgombea Urais yeyote kufanya kazi za Rais wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa nchi, na Mwenyekiti wa chama kimojawapo cha siasa wakati wa kampeni za uchaguzi.
- Vifungu vyote vya Kanuni za Uchaguzi vinavyowazuia wapiga kura halali kwa mujibu wa ibara ya 5(2) ya Katiba ya nchi (1977) kupiga kura kwa sababu za makosa ya kiuandishi yanayotibika kwa njia ya kiapo au kwa kujaza fomu upya.
Tamko kwamba Watanzania wote wamerithi ahadi ya kuishi katika Taifa ambalo linakuza na kuhami tunu za uhuru, haki, usawa, na uwazi, kwa maana kwamba wanapaswa kupigania tunu hizi kwa hakikisha lwamba kuna chaguzi zinazoheshimu tunu hizi linatokana na ahadi ya waasisi wa Taifa hili kwa kila raia wa TanzTanzaniaa tunavyosoma kwenye Katiba ya nchi (1977), kwenye ibara ya Ibara ya 1, 3(1), 5(1), 5(2), 8(1), 9(a), 9(g), 9(h), 9(k), na 132(5)(f), kati ya zingine nyingi, kwamba:
1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
3(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
5(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi.
5(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo: (a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;(b) kuwa na ugonjwa wa akili; (c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai; (d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama mpiga kura. Mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.
8(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo: (a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii; (b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi; (c) Serikali itawajibika kwa wananchi; (d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
9(a) Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa.
9(g) Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;
9(h) Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;
9(k) Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha: kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia
132(5)(f) Misingi ya Maadili ya Viongozi wa Umma: itaweka masharti mengine yoyote yanayofaa au ambayo ni muhimu kwa madhumuni ya kukuza na kudumisha uaminifu, uwazi, kutopendelea na uadilifu katika shughuli za umma na kwa ajili ya kulinda fedha na mali nyinginezo za umma.
Utetezi wa tamko la sita
Tamko kwamba umma unayo mamlaka ya kikatiba ya kuzuia uovu unaotendwa na serikali kwa kusogeza mbele ratiba ya uchaguzi kupitia mbinu kadhaa za shinikizo la amani zinazokubalika kikatiba, linatokana na kifungu cha 28(1) cha Katiba ya nchi (1972) kisemacho kuwa:
28(1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.
Kuna mbinu zipatazo 200 za kutekeleza jukumu tajwa bila kuvunja sheria za nchi, baadhi zikiwa zimejadiliwa kwa kina katika kitabu cha Gene Sharp(1973) kiitwacho "The Politics of Nonviolent Action, Volume 1-3, (Boston: Peter Sargent). Mbinu hizo ni pamoja na hizi zilizotajwa kwenye "Kiambatanisho B," kutoka kwenye kitabu chenye fomati ya PDF kilichoambatanishwa pia.
Gene Sharp(1973), The Politics of Nonviolent Action, Volume 1-3, (Boston: Peter Sargent)
V. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
Hoja ya Tundu Lissu inakubalika kwa wapiga kura wote wenye akili timamu wakiwemo mapadre, mashehe, wanafunzo wa vyuo vikuu, watu wengi wenye elimu ya msingi, watu wengi wenye elimu ya sekondari, wakulima wengi, wafanyakazi wengi, wafanyabiashara wengi.
Watu hawa ni "wananchi wa Tanzania" wenye sifa zifuatazo:
- Wanajua tofauti kati ya wema na ubaya.
- Wanafahamu kuwa kuiba kura ni uovu.
- Wanajua kuwa Tanzania ni dola ya Kikatiba.
- Wanajua kuwa Tanzania ni dola ya Kidemokrasia.
- Wanajua kuwa demokrasia maana yake wengi wape na sio kinyume chake.
- Wanafahamu kuwa Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri.
- Wanajua tofauti kati ya dola ya Jamhuri na dola ya Kifalme.
- Wamefundishwa na viongozi wao wa dini kwamba "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu"
- Wamefundishwa na viongozi wao wa dini kwamba "Mungu wetu ni Mungu wa haki."
- Wanajua kuwa uchaguzi unaoheshimu tunu za kisiasa kama vile haki, uhuru, ushindani na uwazi ni bora kuliko uchaguzi unaokiuka kanuni hizi.
Hivyo, Paschal Mayala aachane na siasa za hadaa, akubali ukweli mchungu kwamba Tanzania ni dola ambayo ni Jamhuri ya KIkatiba na Kidemokrasia isiyopaswa kunajisiwa na wanasiasa matapeli.
Hawa wanaiba uchaguzi mchana kweupe.
Na jambo baya zaidi ni kwamba mataoeli hawa ni sehemu ya vyombo vya dola inayojumuisha ma-WEO, ma-DED, ma-DC, ma-RC, ma-RAS, ma-OCD, ma-DSO, ma-RSO, ma-ZSO, na watu baki kama hao.
Pia aache dharau kwa Lissu Jembe la Kimataifa na aepuke utapeli wa kucheza na maneno dhidi ya Watanzania.
Kama akijifunza kutofautisha maana za maneno "uwezo," "uwezekano," na "ulazima," ataweza kugundua kwamba, kisheria na kikatiba, tamko lisemalo kwamba "Bila mabadiliko hakuna uchgauzi" ni tamko ambalo linaongelea mambo yfuatayo:
- Linaongelea "uwezekano" wa kusogeza ratiba ya uchaguzi kwa kuwa hakuna sheria inazuia ratiba ya uchaguzi kusogezwa mbele, hata kama ingekuwepo bado sheria sio msahafu wa kidini.
- Linaongelea "ulazima" wa kusogeza ratiba ya uchaguzi kwa maana kwamba kadiri uhalifu wa kiuchaguzi unavyohusika, uvumilivu wa umma wenye kiu ya haki umefika kwenye ukomo wa juu kabisa, yaani "enough is enough."
- Na linaongelea "uwezo" wa kusogeza ratiba ya uchaguzi kwa maana ya mamlaka yaliyo mikononi mwa umma kuamua kwa pamoja juu ya mustakabali wa Taifa lao, ama kupitia demokrasia ya uwakilishi ay demokrasia ya moja kwa moja.
Lakini, Mayalla alazima ajue kuwa "katika kujinufaisha na haki yake ya ukosoaji wenye kuzingatia haki na kanuni za kimantiki," yaani “the right of fair and reasoned criticism,” haki hiyo inayo mipaka yake, na mpaka mmojawapo ni kutofautisha kati ya hoja na mleta hoja, wakati mpaka wa pili ni ukuta unatenganisha ukweli mkavu (brute facts) na uwongo unaoambatana na maoni binafsi.
Nawasilisha.
KIAMBATANISHO A: MAANA TOFAUTI ZA NENO "UWEZEKANO"
Kuna "uwezekano" wa kimantiki, kifizikia, kimetafizikia. Pia kuna "ulazima" wa kimantiki, kifizikia, kimetafizikia. Ufafanuzi unafuata.
- Logically possible: Something is considered logically possible if it does not contradict the laws of logic, meaning it can be conceived of without creating a contradiction, even if it might not be physically achievable in reality; like a flying car.
- Physically possible: Something is physically possible if it can occur within the constraints of the known laws of physics, meaning it could actually happen in the real world; like a person jumping on the moon is logically possible but not physically possible.
- Metaphysically possible: This refers to a broader concept of possibility, often considered in terms of "possible worlds," where something is metaphysically possible if it could exist in some conceivable reality, even if we don't fully understand the laws governing that reality.
- Legal possibility: This refers to whether an action or event is permissible under the law, meaning it is not prohibited by legal statutes.
- Social possibility: Something is socially possible if it is considered acceptable or feasible within the norms and practices of a particular society.
- Logically necessary: A proposition is logically necessary if it is true by definition and cannot be false according to the rules of logic, like "a square has four sides".
- Physically necessary: Something is physically necessary if it must happen according to the laws of physics, like gravity pulling objects towards the Earth.
- Metaphysically necessary: A proposition is metaphysically necessary if it is true in all possible worlds, meaning it cannot be conceived of as being otherwise.
- Key takeaway: "Logical possibility" is the broadest category, encompassing anything that can be conceived without contradiction, while "physical possibility" is a subset that considers only what is possible based on the physical laws of our universe. "Metaphysical possibility" is a more philosophical concept, referring to what could exist in any conceivable reality.
VI. KIAMBATANISHO B: MBINU 200 ZA SHINIKIZO LA AMANI DHIDI YA SERIKALI KATILI
Kwa mujibu wa kitabu cha Gene Sharp(1973) kiitwacho "The Politics of Nonviolent Action, Volume 1-3, (Boston: Peter Sargent), ambacho kimeambatanishwa hapa mwishoni mwa makala, mbinu za shinikizo la amani ni pamoja na hizi hapa:
Formal Statements
1. Public Speeches
2. Letters of opposition or support
3. Declarations by organizations and institutions
4. Signed public statements
5. Declarations of indictment and intention
6. Group or mass petitions
Communications with a Wider Audience
7. Slogans, caricatures, and symbols
8. Banners, posters, and displayed communications
9. Leaflets, pamphlets, and books
10. Newspapers and journals
11. Records, radio, and television
12. Skywriting and earthwriting
Group Representations
13. Deputations
14. Mock awards
15. Group lobbying
16. Picketing
17. Mock elections
Symbolic Public Acts
18. Displays of flags and symbolic colors
19. Wearing of symbols
20. Prayer and worship
21. Delivering symbolic objects
22. Protest disrobings
23. Destruction of own property
24. Symbolic lights
25. Displays of portraits
26. Paint as protest
27. New signs and names
28. Symbolic sounds
29. Symbolic reclamations
30. Rude gestures
Pressures on Individuals
31. “Haunting” officials
32. Taunting officials
33. Fraternization
34. Vigils
Drama and Music
35. Humorous skits and pranks
36. Performances of plays and music
37. Singing
Processions
38. Marches
39. Parades
40. Religious processions
41. Pilgrimages
42. Motorcades
Honoring the Dead
43. Political mourning
44. Mock funerals
45. Demonstrative funerals
46. Homage at burial places
Public Assemblies
47. Assemblies of protest or support
48. Protest meetings
49. Camouflaged meetings of protest
50. Teach-ins
Withdrawal and Renunciation
51. Walk-outs
52. Silence
53. Renouncing honors
54. Turning one’s back
The Methods of Social Noncooperation
Ostracism of Persons
55. Social boycott
56. Selective social boycott
57. Lysistratic nonaction
58. Excommunication
59. Interdict
Noncooperation with Social Events, Customs, and Institutions
60. Suspension of social and sports activities
61. Boycott of social affairs
62. Student strike
63. Social disobedience
64. Withdrawal from social institutions
Withdrawal from the Social System
65. Stay-at-home
66. Total personal noncooperation
67. “Flight” of workers
68. Sanctuary
69. Collective disappearance
70. Protest emigration (hijrat)
The Methods of Economic Noncooperation: Economic Boycotts
Actions by Consumers
71. Consumers’ boycott
72. Nonconsumption of boycotted goods
73. Policy of austerity
74. Rent withholding
75. Refusal to rent
76. National consumers’ boycott
77. International consumers’ boycott
Action by Workers and Producers
78. Workmen’s boycott
79. Producers’ boycott
Action by Middlemen
80. Suppliers’ and handlers’ boycott
Action by Owners and Management
81. Traders’ boycott
82. Refusal to let or sell property
83. Lockout
84. Refusal of industrial assistance
85. Merchants’ “general strike”
Action by Holders of Financial Resources
86. Withdrawal of bank deposits
87. Refusal to pay fees, dues, and assessments
88. Refusal to pay debts or interest
89. Severance of funds and credit
90. Revenue refusal
91. Refusal of a government’s money
Action by Governments
92. Domestic embargo
93. Blacklisting of traders
94. International sellers’ embargo
95. International buyers’ embargo
96. International trade embargo
The Methods of Economic Noncooperation: The Strike
Symbolic Strikes
97. Protest strike
98. Quickie walkout (lightning strike)
Agricultural Strikes
99. Peasant strike
100. Farm Workers’ strike
Strikes by Special Groups
101. Refusal of impressed labor
102. Prisoners’ strike
103. Craft strike
104. Professional strike
Ordinary Industrial Strikes
105. Establishment strike
106. Industry strike
107. Sympathetic strike
Restricted Strikes
108. Detailed strike
109. Bumper strike
110. Slowdown strike
111. Working-to-rule strike
112. Reporting “sick” (sick-in)
113. Strike by resignation
114. Limited strike
115. Selective strike
Multi-Industry Strikes
116. Generalized strike
117. General strike
Combination of Strikes and Economic Closures
118. Hartal
119. Economic shutdown
The Methods of Political Noncooperation: Rejection of Authority
120. Withholding or withdrawal of allegiance
121. Refusal of public support
122. Literature and speeches advocating resistance
Citizens’ Noncooperation with Government
123. Boycott of legislative bodies
124. Boycott of elections
125. Boycott of government employment and positions
126. Boycott of government depts., agencies, and other bodies
127. Withdrawal from government educational institutions
128. Boycott of government-supported organizations
129. Refusal of assistance to enforcement agents
130. Removal of own signs and placemarks
131. Refusal to accept appointed officials
132. Refusal to dissolve existing institutions
Citizens’ Alternatives to Obedience
133. Reluctant and slow compliance
134. Nonobedience in absence of direct supervision
135. Popular nonobedience
136. Disguised disobedience
137. Refusal of an assemblage or meeting to disperse
138. Sitdown
139. Noncooperation with conscription and deportation
140. Hiding, escape, and false identities
141. Civil disobedience of “illegitimate” laws
Action by Government Personnel
142. Selective refusal of assistance by government aides
143. Blocking of lines of command and information
144. Stalling and obstruction
145. General administrative noncooperation
146. Judicial noncooperation
147. Deliberate inefficiency and selective noncooperation by enforcement agents
148. Mutiny
Domestic Governmental Action
149. Quasi-legal evasions and delays
150. Noncooperation by constituent governmental units
International Governmental Action
151. Changes in diplomatic and other representations
152. Delay and cancellation of diplomatic events
153. Withholding of diplomatic recognition
154. Severance of diplomatic relations
155. Withdrawal from international organizations
156. Refusal of membership in international bodies
157. Expulsion from international organizations
The Methods of Nonviolent Intervention: Psychological Intervention
158. Self-exposure to the elements
159. The fast
a) Fast of moral pressure
b) Hunger strike
c) Satyagrahic fast
160. Reverse trial
161. Nonviolent harassment
Physical Intervention
162. Sit-in
163. Stand-in
164. Ride-in
165. Wade-in
166. Mill-in
167. Pray-in
168. Nonviolent raids
169. Nonviolent air raids
170. Nonviolent invasion
171. Nonviolent interjection
172. Nonviolent obstruction
173. Nonviolent occupation
Social Intervention
174. Establishing new social patterns
175. Overloading of facilities
176. Stall-in
177. Speak-in
178. Guerrilla theater
179. Alternative social institutions
180. Alternative communication system
Economic Intervention
181. Reverse strike
182. Stay-in strike
183. Nonviolent land seizure
184. Defiance of blockades
185. Politically motivated counterfeiting
186. Preclusive purchasing
187. Seizure of assets
188. Dumping
189. Selective patronage
190. Alternative markets
191. Alternative transportation systems
192. Alternative economic institutions
Political Intervention
193. Overloading of administrative systems
194. Disclosing identities of secret agents
195. Seeking imprisonment
196. Civil disobedience of “neutral” laws
197. Work-on without collaboration
198. Dual sovereignty and parallel government