Kimenuka Tarime, Heche asakwa na Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kimenuka Tarime, Heche asakwa na Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Aug 13, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hali ya kisiasa wilayani Tarime inazidi kuwa tete baada ya jana mwenyekiti wa Chadema wilayani humo kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti wa BAVICHA John Heche. Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kamanda John Heche anasakwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya kwa tuhuma za kumkashifu raisi Kikwete.

  Katika mkutano wake wa juzi alioufanya katika mji mdogo wa Sirari, Heche aliwaeleza wananchi kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ombaomba wakati ina rasilimali nyingi sana za kuiwezesha kujitegemea. Akawaeleza wananchi hao kuwa raisi Kikwete ndiye anaongoza zoezi hilo la kuwa ombaomba, kwa kwenda ulaya na marekani kila mara kutembeza bakuli.

  Heche alielezea masikitiko yake kwa raisi Kikwete kupishana angani na ndege zilizojaza madini yetu kupeleka ulaya na marekani huku yeye akiwa amefungashiwa vyandarua na hao wazungu wanaopora rasilimali zetu. Bado nafuatilia kujua hatma ya sakata hili na nitaendelea kuwa update kadri inavyowezekana.

  UPDATES 2:
  Taarifa rasmi kutoka Tarime ni kwamba Kamanda Heche amefika kituo cha polisi Tarime kama alivyoitwa na kaimu kamanda wa Tarime Rorya lakini amegoma kuhojiwa hadi atakapokuwa na wakili wake. Kufuatia hali hiyo uongozi wa jeshi la polisi umekubaliana nae na kumpa muda hadi kesho saa tisa afike na wakili wake kwa ajili ya mahojiano.

  Kwa upande mwingine Heche anaendelea na mikutano ya hadhara kjama kawaida na muda huu anaelekea eneo la Muriba kuzungumza na wananchi. Zengwe lililokuwa limewekwa na mwenyekiti wa wilaya limeshindwa na sasahivi mwenyekiti huyo anahaha huku na kule asijue hatma yake itakuwa ni nini.
   
 2. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Liwalo na Liwe !
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  haya sasa,aende tu akatoe maelezo,maana kutafutwa sio kufungwa
   
 4. m

  mamajack JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwani kamkashifu au kasema ukweli?kweli anaenaenda kuleta neti wenzake wanabeba madini.hilo jeshi la nyinyiemu police wanaendelea na kazi za kutengeneza movie zao.
   
 5. Deus F Mallya

  Deus F Mallya Verified User

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 707
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwani lipi la Uongo hapo?
  Nchi ambayo kila siku inaomba misaada tu wanataka iitweje?
  Nchi ambayo ndege inatua na kubeba Twiga na Tembo wanataka iitweje?
  Nchi ambayo Ndege inatua na kubeba madini bila kuhakikiwa Wanataka iitweje?
  Rais anayeenda kuomba omba Misaada kila kukicha mnataka aitweje?
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Tarime napaaminia hakuna mbaya itakayotokea kwani ni uwongo kuwa sisi ni ombaomba duniani? asilimia ngapi ya budget yetu inategemea bakuli? madini na michanga yote si inapelekwa ulaya? mara ngapi jk anaenda kuomba na akirudi hapa anajigamba wafadhili wametusaidia??
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwa nini amejificha?
   
 8. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ukweli mtupu...sioni kashfa hapo! Labda tu kwa ule usemi kuwa 'Truth Hurts'!
   
 9. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,476
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  WAO WANA PESA NA DOLA, SISI TUNA PEOPLES POWER NA MUNGU. KAMWE HAWATAEZA KUZUIA M4C, NA HARAKATI ZOTE ZA KUMKOMBOA MTANZANIA KUTOKA MIKONONI MWA MKOLONI MWEUSI (chama cha mabwepande).
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Afadhali JK anaomba kwa maslahi ya Taifa , zile pesa wanazochangisha CDM wakiwa wavekwiva kwenye suti kwenye mahoteli makubwa hapa nchini kusafisha fedha haramu wanazoletewa na wazungu hao hao zinafanya nini?
   
 12. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwita Maranya hilo la kuongea ukweli unaoitwa kashfa na kutafutwa na polisi ni la kawaida sana!Concern yangu ipo hapo ulipoandika kuwa mwenyekiti wa chadema wilaya Tarime aliandika barua polisi kusitisha mikutano ya Heche.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  UPDATES:
  Nimezungumza na kamanda Heche muda mfupi uliopita, amenifahamisha kwamba amepigiwa simu na kaimu kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime Rorya ili afike kituoni kwa mahojiano.
  Sasahivi ndio anaelekea kituo cha polisi Tarime mjini kwa ajili ya mahojiano hayo.

  Taarifa za ndani kabisa toka polisi Tarime ni kwamba kuna shinikizo/maelekezo toka juu kwamba Heche akamatwe ama akijisalimisha azuiliwe mahabusu ya polisi hadi kesho atakapopandishwa kizimbani.

  Nadhani wale mliopo Tarime mnaweza kufuatilia kwa karibu na kutujuza kinachojiri huko.
   
 14. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Suala la nchi kuwa omba omba dunia nzima inafahamu na rasilimali zetu kuchukuliwa inafahamika pia. Ila sababu za mwenyekiti wa wilaya wa Cdm kuzuia mikutano ya BAVICHA ni nini?
   
 15. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  fafanua hapo mwanzoni. Mwenyekiti wilaya chadema kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti BAVICHA... hii kama haijakaa sawa.!
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa maslahi yapi uliyoyaona kwa awamu hii ya kikwete...unajua deni la taifa kwa sasa ni kiasi gani? unakumbuka wakati anaachiwa nchi hazina kulikuwa na kiasi gani? je deni likuwa kiasi gani?...vipi bei ya vyakula nikupe mfano kikwete anachukua nchi bei ya mchele ilikuwa TZS 650 sasa hivi mpaka TZS 3000, kiberiti 25 sasa hivi 100...ngoja nikomee hapo
   
 17. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  "CHADEMA lazima tuisambaratishe ndani ya mwaka mmoja kwa njia yeyote tuiwezayo" Wasirra
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  "Nisipoenda kuhemea watanzania mtakufa na njaa!" - J. M. Kikwete (Tabora 2010)
   
 19. k

  kanewi JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  yote haya ni kama yanajirudia na isitoshe kwa taifa kama letu lililojaa uzalimu na vimbwanga vya kila aina,ktk harakati za kusaka ukombozi misukosuko ndo mahara pake,.IF YOU DO NOT STAND FOR IT THEN PUT THE WORD FREEDOM OUT OF YOUR vocabulary,.HECHE USITISHIKE NDO MUENDELEZO HUO SIO MAPYA HAPA KWETU
   
 20. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Crashwise acha kupoteza mda wako kumuelimisha thatha kama una mda wa kuchezea si umfundishe paka wako kusoma na kuandika?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...