Kimenuka Tarime, Heche asakwa na Polisi

Kimenuka Tarime, Heche asakwa na Polisi

Tujuze mwana nini kinaendelea huko wameisha anza mambo yao kwani ni uongo kuwa viongozi wamekuwa ombaomba
yanamwisho.
 
Kama ni wajanja wamwache! Maana wanampiga chura teke.
 
Kama ni kwa kauli hizo hastahili kuwakimbia polisi, anapaswa kujitokeza na kutozikanusha maana ndio ukweli wenyewe.
 
Afadhali JK anaomba kwa maslahi ya Taifa , zile pesa wanazochangisha CDM wakiwa wavekwiva kwenye suti kwenye mahoteli makubwa hapa nchini kusafisha fedha haramu wanazoletewa na wazungu hao hao zinafanya nini?

Acha uzuzu wewe!! fedha chafu zinapitia wapi wakati hapa Tz serikali yenu ina kitengo cha kuzuia fedha chafu? au unataka kusema kuwa serirkali yenu ni dhaifu hadi kwenye kuzuia fedha chafu zisiingie nchini?. Hizo suti unazozitaja ni zipi, au unaongelea zile suti alizoongwa Mr. dhaifu kule USA?
 
Kwani kamkashifu au kasema ukweli?kweli anaenaenda kuleta neti wenzake wanabeba madini.hilo jeshi la nyinyiemu police wanaendelea na kazi za kutengeneza movie zao.

Police wamepewa maagizo hayo na dogo Nape kwa hofu mbinyo wa M4C
 
Mhhhh! Sijui kashfa dhidi ya Kikwete iko wapi katika hayo yaliyozungumzwa na Heche. Yote aliyoongea ni ukweli mtupu. Naona kuna kila dalili ya polisi magamba kuanza kubambikia kesi Viongozi mbali mbali wa CHADEMA, lakini hakuna kurudi nyuma mapambano yataendelea.

😛eace:😛eace:😛eace:

Alutta continua! continua

Hali ya kisiasa wilayani Tarime inazidi kuwa tete baada ya jana mwenyekiti wa Chadema wilayani humo kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti wa BAVICHA John Heche. Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kamanda John Heche anasakwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya kwa tuhuma za kumkashifu raisi Kikwete.

Katika mkutano wake wa juzi alioufanya katika mji mdogo wa Sirari, Heche aliwaeleza wananchi kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ombaomba wakati ina rasilimali nyingi sana za kuiwezesha kujitegemea. Akawaeleza wananchi hao kuwa raisi Kikwete ndiye anaongoza zoezi hilo la kuwa ombaomba, kwa kwenda ulaya na marekani kila mara kutembeza bakuli.

Heche alielezea masikitiko yake kwa raisi Kikwete kupishana angani na ndege zilizojaza madini yetu kupeleka ulaya na marekani huku yeye akiwa amefungashiwa vyandarua na hao wazungu wanaopora rasilimali zetu. Bado nafuatilia kujua hatma ya sakata hili na nitaendelea kuwa update kadri inavyowezekana.
 
Afadhali JK anaomba kwa maslahi ya Taifa , zile pesa wanazochangisha CDM wakiwa wavekwiva kwenye suti kwenye mahoteli makubwa hapa nchini kusafisha fedha haramu wanazoletewa na wazungu hao hao zinafanya nini?
No research no right to speak, usitekwe na mpropaganda wa nyinyiemu wenu, kama CDM wanatoa hela ya haramu nje hilo ni kosa kisheria, so km wana uthibitisho swala hilo limefanyika wakashtaki, vinginevyo waache kutuzuga na brainless propaganda maana km wanajua kuna jinai inafanyika na wanainyamaza kitendo hicho ni jinai pia wanakuwa accessories after the fact.
 
UPDATES:
Nimezungumza na kamanda Heche muda mfupi uliopita, amenifahamisha kwamba amepigiwa simu na kaimu kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime Rorya ili afike kituoni kwa mahojiano.
Sasahivi ndio anaelekea kituo cha polisi Tarime mjini kwa ajili ya mahojiano hayo.

Taarifa za ndani kabisa toka polisi Tarime ni kwamba kuna shinikizo/maelekezo toka juu kwamba Heche akamatwe ama akijisalimisha azuiliwe mahabusu ya polisi hadi kesho atakapopandishwa kizimbani.

Nadhani wale mliopo Tarime mnaweza kufuatilia kwa karibu na kutujuza kinachojiri huko.
Hivi kwa nini serikali inazidisha juhudi za kuwafanya wananchi wakichukie CCM?
 
View attachment 61696
Hivi huwa anaenda kuomba omba au kupiga picha na mastaa wa huko naomba kuwekwa sawa hapa.. Pata picha za matukio mbalimbali ya Kikwete akiwa majuu
Malengo ya safari ni mawili. La kwanza ni picha na watu maarufu duniani bila kujali ni umaarufu wa nini na pili ni kutembeza bakuli. Tunashukuru kwa kuwa na kiongozi wa karba hii maana kwetu sisi watanzania ndiyo rekodi pekee tunayojivunia kwa sasa kwa kuwa na RAHISI aliyetembelea nchi nyingi duniani ndani ya kipindi kisichopungua miaka saba.
 
Hali ya kisiasa wilayani Tarime inazidi kuwa tete baada ya jana mwenyekiti wa Chadema wilayani humo kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti wa BAVICHA John Heche. Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kamanda John Heche anasakwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya kwa tuhuma za kumkashifu raisi Kikwete.

Katika mkutano wake wa juzi alioufanya katika mji mdogo wa Sirari, Heche aliwaeleza wananchi kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ombaomba wakati ina rasilimali nyingi sana za kuiwezesha kujitegemea. Akawaeleza wananchi hao kuwa raisi Kikwete ndiye anaongoza zoezi hilo la kuwa ombaomba, kwa kwenda ulaya na marekani kila mara kutembeza bakuli.

Heche alielezea masikitiko yake kwa raisi Kikwete kupishana angani na ndege zilizojaza madini yetu kupeleka ulaya na marekani huku yeye akiwa amefungashiwa vyandarua na hao wazungu wanaopora rasilimali zetu. Bado nafuatilia kujua hatma ya sakata hili na nitaendelea kuwa update kadri inavyowezekana.

Sasa hapo kuna uongo gani?? au askari walitaka aseme Jk huwa anapeleka misaaada USA!!!
 
Kimenuka nini sasa hapo mbona Heche ameeleza facts tupu?
 
Tunataka tujue kuhusu huyo MWENYEKITI WA CHADEMA TARIME ALIESITISHA MKUTANO kwa sababu hata jana kuikuwa na tuhuma zinazohusu huyo mwenyekiti wa CDM tarime kutumiwa na magamba, msimumunye maneno sisi tunataka ukweli kuhusu hilo gamba jipya ndani ya chama chetu.
 
Tatizo la polisi hawajui kashfa na pale mtu anaposema ukweli!!! upeo wao ni kufanya mauaji tuu basi..
 
Heche ni mtu ambaye hana upeo wowote zaidi ya kuongea kwa jazba tu anasema Rais anaomba sana mbona yeye Heche mwenyewe bado anakaa kwa kaka yake Sinza.
 
sijaona alichomtukania rasi bali kaeleza ukweli mtupu
ni ajabu nchi kuomba omba huku tukachia madini yakibebwa usiku kucha
kwnai uongo? hakuna airports katikc amchimbo ya madini? hawatuibii? rais haombi? ukweli mtupu
hawatathubutu kumweka ndani nguvu ya umma ni kubwa kuliko hiyo nguvu ya polisi
muraaaaa,walyancholi,wanzali, walyanchaki wote mko wapi? amkeni teteeni haki yenu.
 
Hali ya kisiasa wilayani Tarime inazidi kuwa tete baada ya jana mwenyekiti wa Chadema wilayani humo kuandika barua polisi kusitisha mikutano ya mwenyekiti wa BAVICHA John Heche. Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba kamanda John Heche anasakwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime Rorya kwa tuhuma za kumkashifu raisi Kikwete.

Katika mkutano wake wa juzi alioufanya katika mji mdogo wa Sirari, Heche aliwaeleza wananchi kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ombaomba wakati ina rasilimali nyingi sana za kuiwezesha kujitegemea. Akawaeleza wananchi hao kuwa raisi Kikwete ndiye anaongoza zoezi hilo la kuwa ombaomba, kwa kwenda ulaya na marekani kila mara kutembeza bakuli.

Heche alielezea masikitiko yake kwa raisi Kikwete kupishana angani na ndege zilizojaza madini yetu kupeleka ulaya na marekani huku yeye akiwa amefungashiwa vyandarua na hao wazungu wanaopora rasilimali zetu. Bado nafuatilia kujua hatma ya sakata hili na nitaendelea kuwa update kadri inavyowezekana.

Police bhana...wanamtafutia wapi?
 
Back
Top Bottom