TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,763
- 4,047
Wananchi wamelimishwa vya kutosha na sasa wanajua vizuri haki zao!Kisa na mkasa?
Wananchi wamelimishwa vya kutosha na sasa wanajua vizuri haki zao!Kisa na mkasa?
Waende pale Mindu,maji ni mengi kama nn...
K .nyembe gani hiyo yenye maji mkuu? Mimi nipo K. nyembe kwa mkorea ,mbona sijawahi kupata maji mwaka wa 7 huu?si kweli,we unaishi maeneo gani?
1.maeneo ya mazimbu maji yanapatikana muda wote
2.maeneo ya kingo-maji yapo
3.maeneo ya mjini-ccm wilaya-ccm mkoa,maji yapo
4.maeneo ya mindu-maji yapo
5.maeneo ya madaganya-maji yapo baadhi ya maeneo
6.maeneo ya chamwino,maji yapo
7,maeneo ya kigurunyembe-yapo maji kibao yakutosha
maeneo ya kihonda-mji mpya-elu hadi kwa chambo ni matatizo tupo,ktk kuishi kwangu kule nimekuwa nikiagiza gari la maji kwa 80,000 kila mwezi.
wewe sema wapi unaishi.acha ubabaishaji
nina uhakika maji yapo,labda unaishi mazingira mapya kabisa,maana ile kihonda kwa chambo hadi mazimbu road,mji mpya,mgudeni ni za kitambo sana waliweka mabomba na mabomba hayo hayatoi maji kazi yao ni kuuza maji kwa malori yao.K .nyembe gani hiyo yenye maji mkuu? Mimi nipo K. nyembe kwa mkorea ,mbona sijawahi kupata maji mwaka wa 7 huu?
Unataka kusema huu ndoo mwanzo wa ukombozi toka kwenye makucha ya CCM au?
Kuna visima 25 tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama katika maeneo yote yenye kero kubwa ya changamoto ya upatikanaji wa maji na kuwa uchimbaji wa visima hivyo umetokana na ukweli kuwa mpaka sasa baadhi ya kata hizo bado hazijapata miumbombinu ya mamlaka ya majisafi na majitaka ndiyo maana nimechimba visima hivyo alisema Abood.abood ndiyo mbuge
Kuna visima 25 tayari wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama katika maeneo yote yenye kero kubwa ya changamoto ya upatikanaji wa maji na kuwa uchimbaji wa visima hivyo umetokana na ukweli kuwa mpaka sasa baadhi ya kata hizo bado hazijapata miumbombinu ya mamlaka ya majisafi na majitaka ndiyo maana nimechimba visima hivyo alisema Abood.
Abood aliyataja maeneo hayo ambayo yana kero kubwa ya upatikanaji wa majisafi na salama katika Manispaa ya Morogoro kuwa ni pamoja na Mzinga, Areasix, Lukobe, Tungi, Mkundi, Kichangani na Areafive na kuwa tayari kiasi cha sh 134 Milioni zimetumika katika awamu mbili ambao awamu ya kwanza vimechimbwa visima 10 na awamu ya pili visima 15 vinaendelea kuchimbwa katika kata hizo.
Baadhi ya maeneo hayo miundombinu ya mamlaka hiyo haijawafikia na kuwa kumekuwa na mgao unaosababisha wakazi wake maeneo hayo kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji kwa muda mrefu.
Hayo maji safi na salama yanatoka kwenye kisima gani? Embu kuwa mkweli kaka/dada, mimi nakaa kihonda azimio na huyo mbunge amechimba kisima ila maji yanayotoka pale hayafai kwa matumizi ya binadamu wala mnyama, maji yana chumvi na magadi hayafai zaidi ya kuflashia chooni tu. Tunanunua maji kila siku, tulisha mwambia bila maji 2015 tusitafutane, aendelee tu na mpango wake wa kuwanunulia wale wapika majungu wa mjini kahawa na kashata maana wao ndio watampigia kura.
wachimbe visima majini mengi sana