Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Sasa wewe umetoka huko mkoani mpaka hapa kwa mkulu kutafuta passport ya kusafilia bila kuomba ushairi humu JF, afu Leo unakuja kulia lia apa ili iweje?
Jf humu ni kila kitu hata ukitaka Dada mtu aoelewe anaolewa tu hamna shida, Jf engine kubwa kuzidi hata hao serikali.
Siku nyingine usiende kichwa kichwa
 
Kupata kipya inachukua muda gani? Je, naweza kutoka NIDA kupata namba ya kitambulisho cha uraia ambacho nimepoteza nikaitumia katika kuomba passport?

Mimi nilipata ndani ya wiki tatu
 
Salaam,

Majuzi nilipata fursa fulani ya kwenda nchini Ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda Uhamiaji pale Kurasini kushughulikia passport.

Lahaulaaa...

Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata passport ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.

Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje hicho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport .

Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambiwa vitambulisho vikiwa tayari Mwenyekiti wa Mtaa atawatangazia na mtapata.

Just imagine, eti askari wa Uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-

Cheti cha kuzaliwa,

Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,

Form ya kuomba passport ya Uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na Afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),

Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),

Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao

Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)


Cha ajabu sasa...
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu...

Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?

Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?

Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?

Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?

Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi.

Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema.

Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.

Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote Idara ya Uhamiaji ya nchi hii.

Ahsante

Yaani haya mambo yanachanganya sana. Process vitambulisho vya Taifa inatumia system ile ile ya kuandikishia wapiga kura. kwenye zoezi la kuandikisha wapiga kura it was a matter of minutes unatoka na kitambulisho cha mpiga kura and it is apparent the same process would be applied for National ID. Ilikuwa ni suala la ku- evolve viongozi wa kata kuandaa neccessary documentations za watu wote ili the moment mtu anapokuwa registered aweze kuondoka na kitambulisho chake.
 
Kwa taarifa yako huko nchi za nje mi nshachoka hadi kwenda,ila nachokwambia ndo hicho acheni kulalamika kwa kila jambo fateni utaratibu mambo yatakua rahisi tu
Hivi wewe uwezo wako wa kufikiri umeenda likizo ee...????

Umemsoma mtoa mada ukamuelewa...????

Wewe unafikiri intake inakusubiri baada ya kupata scholarship...???

Alafu unasema nchi za nje umekaa mpaka ukachoka..!!acha kujikweza mkulima wewe..!!!!
 
Wewe ni nani kwenye hii nchi mpaka useme huo mchakato ni wa kisiasa? Wewe ni mbunge wa upinzani? Kiongozi wa chama cha upinzani? Au activist dhidi ya Serikali?

Ulienda ukiwa umevaa mavazi ya chama pinzani?
Hivyo videgree vyako viwili ndio vimeleta siasa? Kama "msomi" argument building inakua ya kipumbavu hivi bora hata usingeenda shule.
Mkuu umetoa povu jingi bila hata kuelewa comment yangu! Pole sana. Soma tena utanielewa. Nilikuwa namjibu aliyesema niende na kofia ya kijani kuomba passport kwa kumuambia kwanini anachanganya siasa kwenye suala langu
 
Mkuu unamaanisha nini hapo kwenye kijani? Mimi masuala ya kisiasa kwenye ishu nyeti kama hizi huwa nashangaa wanaoyaleta. This is very absurd

Tena uwe na kadi ya Kijani iliyolipiwa miaka 3 mbele yaani up to 2019. Kama hutaki, ngojea utaratibu wetu pendwa upate kitambulisho cha Taifa 2020 December. Ati masuala ya kisiasa unawashangaa wanaoyaleta. Hayo ndo maagizo unataka au hutaki hayatuhusu
 
Watanzania tuache kua tunalalamika hovyo kwa kila jambo,tatizo tumezoea kuishi km wanyama bila utaratibu wowote so mkiletewa utaratibu flan mnaanza kulialia tu yn mnapenda kila kitu kiwe mteremko tu.
Hv mnaona ishu ya passport ni kitu kidogo sn yn uende tu asubuhi jione upewe?kigezo hicho cha kupata passport hadi uwe na kitambulisho cha taifa kilitangazwa siku ya kwanza ya uzinduzi wa hyo passport mpya inamana hukusikia?vitambulisho vya taifa wala havisumbui km una vigezo zikizidi sn ni wiki2 ushapata ila mtu kaa nyumbani tu anasuburi apate uhitaji wa hicho kitambulisho ndo aanze kukitafuta sasa kwa mwendokasi utakwama tu.
Mkuu alitangaza hilo agizo wakati huo nimejiandikisha kitambulisho cha uraia kitambo tu. Hujataka kuliona hili jambo kwa upana wake.
 
Wakuu hili swala limekuwa shida sana, kwa mfano hapa Mbeya wanasema hawatoi hizi electronic passport mpaka dar maana hapa hawana vifaa. Hivi siku si nyingi ntakuwa naenda dar kufatilia maana nimeshajaza fimu tayari online na nisha print
 
Mkuu nakushukuru kwa majibu yaliyo mazuri sana. Naomba nikuulize maswali machache kama hutojali :-
1. Iwapo Passport yangu inaexpire miaka mitatu ijayo kuna ulazima wa kutafuata Electronic Passport
2. Iwapo ni muhimu kubadili sasa, mbali na National ID vitu gani nitatakiwa niviandae?
3. Natoa shukrani kwa muda wako

Ahsante
Hakuna umuhimu wa kukimbilia ku-apply hizi pass mpya! Wametoa mpaka mwaka 2020 ndio mwisho. Hivyo bado hizi za sasa zitaendelea kutumika mpaka mwaka huo!
 
Hakuna umuhimu wa kukimbilia ku-apply hizi pass mpya! Wametoa mpaka mwaka 2020 ndio mwisho. Hivyo bado hizi za sasa zitaendelea kutumika mpaka mwaka huo!
Sasa kama ipo ya zamani kwanini watu wanahangaika, watu tunaendelea na hizo kukuu
 
Nashukuru kuna namna umeelewa kidogo kuhusu sisi Watanzania. Hata hivyo nakuelewesha tena kidogo. Mtoto anapozaliwa hospitalini mzazi hupewa cheti na nakala hubaki hapo hospitali na kitabu cha vyeti kikijaa hupelekwa Ofisi ya DC na mzazi huenda na hicho cheti Ofisi ya Usajili (kwa DC) ili mtoto apewe cheti cha kuzaliwa. Wao kwa DC huwa wana-match taarifa zao na cheti chako maana kitabu cha nakala wanakuwa nacho na wanakupa wiki chache uende kuchukua cheti. Sasa jiulize, watoto wote huzaliwa hospitali? Je, wazazi wote hata wale wanaojifungua hospitali wanaona umuhimu wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa? Je, kwa wale wanaotoka Upangwa milimani na kwenda kujifungulia hospitali na kupata cheti cha awali, baada ya kurudi nyumbani wangapi wanaona umuhimu hasa wa kusafiri kilometa 50-100 wilayani kwa ajili ya kupeleka tu taarifa za mtoto na kisha arudi tena huko baada ya mwezi kwenda kuchukua cheti?

Ndugu yangu mwenye akili nyingi, hiyo ndio hali halisi ya Mtanzania na mazingira yake. FYI wewe ulipata passport ukiwa F4, mimi watoto wangu wote hata aliye Class 4 anayo passport na vyeti vyote vya kuzaliwa anavyo. Lkn napenda tu ufahamu, ni sehemu ndogo tu ya raia ndio wana hizo documents. Kukupa taarifa zaidi ni kuwa kati ya Watanzania wote wapatao milioni 44, ni Watanzania laki 4 tu ndio wenye passport! Hiyo document imefanywa kuwa ya gharama sana hadi kuipata wakati ni haki ya kila Mtanzania mwenye cheti cha kuthibitisha uraia wake na uwezo wa kuilipa kuipata pale anapoihitaji.

Vv
Unapoteza bure muda kumuelimisha mtu ambae upeo wake umeishia mtaa wa pili anaoishi! Watu kama hawa bado pengine ni watoto wadogo na hawajatembelea sehemu nyingi za Tanzania wajue changamoto zake.
 
Sasa kama ipo ya zamani kwanini watu wanahangaika, watu tunaendelea na hizo kukuu
Watu wengi wanaohangaika kwa sasa ni wale ambao walizonazo zime-expire na wanataka mpya! Obviously ni lazima watapewa mpya. Halfu kuna ambao walikuwa hawana kabisa na wamepata safari! Na vile vile kuna wengine wamekuja kwa likizo na wanatarajia wakiondoka hawatarudi muda wa karibuni kabla hizo za zamani hazijaondolewa. Na mwisho kuna wengine ni kimuhe muhe tu cha kumiliki hizo mpya!
 
Kwa serikali hii, hati ya kusafiria ni ANASA. Kama Mkuu hasafiri, wewe Unaenda wapi?? (In Bashii voice)
 
Watu wengi wanaohangaika kwa sasa ni wale ambao walizonazo zime-expire na wanataka mpya! Obviously ni lazima watapewa mpya. Halfu kuna ambao walikuwa hawana kabisa na wamepata safari! Na vile vile kuna wengine wamekuja kwa likizo na wanatarajia wakiondoka hawatarudi muda wa karibuni kabla hizo za zamani hazijaondolewa. Na mwisho kuna wengine ni kimuhe muhe tu cha kumiliki hizo mpya!
Hapo sawa ila wanaojazana ni wale wenye kimuhe muhe, siye wenyewe tulienda na kuuliza kuhusu kutumia 2yrs tukaambiwa poa haina shida
 
Imagine kwa sisi ambao tumerenew passport mwaka Jana , zinatakiwa ziishe after 10 years lakini Kabla ya hiyo miaka 10 unaambiwa ulipe tena pesa kwa ajili ya kubadilishiwa passport uchukue zile wanazozitaka sasa niliyolipa kwa hii niliyo nayo ambayo haina hata miezi wananisaidiaje na ni pesa nimetoa, wangeweka utaribu kwamba passport ikiisha muda ukienda kubadilisha ndio ulipe charges mpya hii si sawa
 
Mkuu fikiria Mtoto hatakiwi kupewa doc za nida, je akitaka pass aende na wazazi wake ughaibuni atafnyaje... Na yeye ni mtanzania...

Kwanini watu wasi lala mikie utaratib mbovu


Atlist basi waweke mtoto atumie details za wazazi zikiwa zimeambatanishwa na Cheti cha kuzaliwa Yaani kitambulisho cha utaifa cha wazazi ili watoto na wenyewe waweze kupata passport Mwigulu Nchemba
 
Hilo swala la passport ni pasua kichwa nikiangalia yangu kurasa zimebaki chache na hicho kitambulisho nishajaza ila sidhani kama tutapata mapema na safari zipo kuna siku niliumiza kichwa itakuaje lakini ngoja kwanza iishe ntapata akili ila ni mtihani huo...
 
Atlist basi waweke mtoto atumie details za wazazi zikiwa zimeambatanishwa na Cheti cha kuzaliwa Yaani kitambulisho cha utaifa cha wazazi ili watoto na wenyewe waweze kupata passport Mwigulu Nchemba
Kitu ambacho ni muhimu sana sana na Tanzania inatakiwa ikifanye kwa haraka ni kuwa na database ya raia wote na possibly kila mmoja apewe social security number. Ni kazi ngumu, inayohitaji umakini, resources na time lakini it worth doing! Ukishakuwa na database na kuwatambua raia wako wote vitu vingine ni kama kusukuma mlevi tu. Kitu kama kitambulisho au passport una uwezo wa ku-apply online na sana sana ukienda ofisini kwao ni kuwapa finger prints tu! Vilevile kutambua wageni, wahalifu na rekodi zao inakuwa rahisi zaidi.
 
Back
Top Bottom