Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Duu pole nakumbuka mie nilienda mwishoni mwa 2014 ndani ya wiki 2 tu tayari nikachukua nilifuata njia halali tu bila kona yeyote
mm nmepoteza kitambulisho cha taifa vipi nakipataj ten ili niweze kuchukua paspot mpya hizi
 
naomb kujua mimi kitambulish changu cha taifa kmepotea nawezaj pata kingine msaada tafadhali
Utaratibu unaenda kwa balozi anakupa barua ya serikali ya mtaa, ukifika serikali ya mtaa unaomba barua ya kwenda polisi wanakupa barua ya polisi unaandikiwa Loss Report unaenda mahakama ya mwanzo wanagonga muhuri unapeleka ofisi za Nida unapata ndani ya wiki 1 au 2.
 
Kachukue kitambulisho acha ulalamishi,Vitambulisho vipo na watu wanapata
 
Ndio ,unaweza pata kingine ila utalipia shilingi 20,000 tu
Kupata kipya inachukua muda gani? Je, naweza kutoka NIDA kupata namba ya kitambulisho cha uraia ambacho nimepoteza nikaitumia katika kuomba passport?
 
Mkuu unaweza kueleza kiundani zaidi changamoto ulizokutana Nazi kurenew passport? Mimi nami nilikuwa najianda kwenda kurenew ya kwangu? Ahsante
Nimerenew juzijuzi tu. Kitambulisho Cha taifa mbele Kama Tai. Na kurenew hakuna tofauti na taratibu za kutafuta passport km vile hukuwa nayo. Kila kitu kinaanza upya na within a week niliipata passport yangu bila longolongo.
 
NIDA wanasema kuna mikoa wamecover 100% ukiwemo dsm.source😱fficer wa TCRA aliyehojiwa AZAM 2 last week
Wakati nnafahamu watu kadhaa ambao hawana hivyo vitambulisho
 
Salaam,

Majuzi nilipata fursa fulani ya kwenda nchini Ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda Uhamiaji pale Kurasini kushughulikia passport.

Lahaulaaa...

Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata passport ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.

Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje hicho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport .

Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambiwa vitambulisho vikiwa tayari Mwenyekiti wa Mtaa atawatangazia na mtapata.

Just imagine, eti askari wa Uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-

Cheti cha kuzaliwa,

Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,

Form ya kuomba passport ya Uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na Afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),

Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),

Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao

Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)


Cha ajabu sasa...
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu...

Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?

Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?

Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?

Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?

Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi.

Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema.

Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.

Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote Idara ya Uhamiaji ya nchi hii.

Ahsante
Tupe fursa hiyo tuende mkuu
 
Si kweli.Walikuwa wanatengeneza mazingila ya kukupiga pesa ili ustuke then waseme lakini kuna plan B ambayo ni wewe kukata cash
Hivyo ndivyo walivyotangaza kuwa uwe na kitambulisho cha uraia wa Tz
 
Mkuu nafikiri tunatakiwa tusisafiri nje ya nchi kama wengine.
Mimi nilienda ku renew nimekutana na kikwazo kama hicho.
Paspoti yangu inakoma 27/3/2018, hii inaninyima kupewa visa.
Nani wa kumshauri huyu mkuu wetu?

26 April
 
Nenda NIDA kachukue kitambulisho cha uraia kama hutaki nenda Ikulu.Kuna wanaoweza kupata passport bila kuwa na kitambulisho cha NIDA kama nidharura kama mgonjwa.

Na umekaa miaka yote hiyo bila kuwa hata na passport na usomi wako huo.
 
Hivyo ndivyo walivyotangaza kuwa uwe na kitambulisho cha uraia wa Tz
Nimemuuliza mtu ,kaniambia ni lazima kuwa na kitambulisho cha Taifa. Unaenda NIDA na unapewa bila wasiwasi hapo NIDA
 
Ni roho mbaya, husda, wivu, chuki na visasi visivyovyakawaida. Lakini usihofu hakuna lenye mwanzo likakosa mwisho.
 
Wewe ongea hivyo kwasababu wewe ni mfugaji jijini Chato..,unajua hayawezi kukuta kabisaaa.

Acha wenye mipango ya mbele waseme kwasababu wanazo sababu za kuongea.

Kama kigezo ni kupata kitambulisho cha taifa kwanza kwann wanavichelewesha namna hiyo...???? Hawajui watu wanasafiri kila Siku...??? Au kwakuwa wao hawependi kusafiri wanataka kila mtu asisafiri...????
Kwa taarifa yako huko nchi za nje mi nshachoka hadi kwenda,ila nachokwambia ndo hicho acheni kulalamika kwa kila jambo fateni utaratibu mambo yatakua rahisi tu
 
kwa waliojiandikisha hawajapata si mlipewa vikaratasi vidogo ambavyo vilikatwa kwenye ile fomu na ina namba ya fomu uliyojaza ndipo nida wakamalizana na ww tumieni hizo zinafaa kuthibitisha ni kama dereva akisha renew lesen au kutaka mpya hatua ya mwisho ni kwenda kulipia akikamatwa na trafiki ile risiti ndio huwa inamsaidia
 
Mkuu nakushukuru kwa majibu yaliyo mazuri sana. Naomba nikuulize maswali machache kama hutojali :-
1. Iwapo Passport yangu inaexpire miaka mitatu ijayo kuna ulazima wa kutafuata Electronic Passport
2. Iwapo ni muhimu kubadili sasa, mbali na National ID vitu gani nitatakiwa niviandae?
3. Natoa shukrani kwa muda wako

Ahsante

Nimerenew juzijuzi tu. Kitambulisho Cha taifa mbele Kama Tai. Na kurenew hakuna tofauti na taratibu za kutafuta passport km vile hukuwa nayo. Kila kitu kinaanza upya na within a week niliipata passport yangu bila longolongo.
 
Back
Top Bottom