falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,227
- 9,356
kama YEYE HASAFIRI IWEJE WEWE USAFIRI
Pole sana mkuu!!Salaam!
Majuzi nilipata fursa flani ya kwenda nchini ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda uhamiaji pale kurasini kushughurikia passport.....
Lahaulaaa....
Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata pass ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.
Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje icho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport!
Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambia vitambulisho vikiwa tayari mwenyekiti wa mtaa atawatangazia na mtapata.
Just imagine, eti askari wa uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-
Cheti cha kuzaliwa,
Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,
Form ya kuomba passport ya uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),
Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),
Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao
Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)
Cha ajabu sasa.......
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu.......
Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?
Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?
Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?
Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?
Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa... Wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi. Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema. Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.
Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote idara ya uhamiaji ya nchi hii. Asante
Vipi kwa wale wenye zile za mwanzo ambazo bado hazijamaliza muda wa kutumika? Wanahitaji kubadilisha kabla?
Sijakuelewa mkuu,passport zinatolewa NIDA sikuhizi?Kabisa mkuu unaenda nayo NIDA wanabadilisha wanakupa mpya hii ya kisasa.
Kama mtu anashangaa kwa majaji kwenda likizo Ulaya na yeye mwenyewe asafiri hata kama ni mikutano inayomuhusu ataruhusuje raia wa kawaida kwenda Ulaya hata kama ni fursa za kusoma...?????Mkuu unamaanisha nini hapo kwenye kijani? Mimi masuala ya kisiasa kwenye ishu nyeti kama hizi huwa nashangaa wanaoyaleta. This is very absurd
Wewe ongea hivyo kwasababu wewe ni mfugaji jijini Chato..,unajua hayawezi kukuta kabisaaa.Watanzania tuache kua tunalalamika hovyo kwa kila jambo,tatizo tumezoea kuishi km wanyama bila utaratibu wowote so mkiletewa utaratibu flan mnaanza kulialia tu yn mnapenda kila kitu kiwe mteremko tu.
Hv mnaona ishu ya passport ni kitu kidogo sn yn uende tu asubuhi jione upewe?kigezo hicho cha kupata passport hadi uwe na kitambulisho cha taifa kilitangazwa siku ya kwanza ya uzinduzi wa hyo passport mpya inamana hukusikia?vitambulisho vya taifa wala havisumbui km una vigezo zikizidi sn ni wiki2 ushapata ila mtu kaa nyumbani tu anasuburi apate uhitaji wa hicho kitambulisho ndo aanze kukitafuta sasa kwa mwendokasi utakwama tu.
Ulipata ile passport ya electronic? Ulijazia form online?Mimi nilikua hapo Kurasini wiki iliyopita na ninamshukuru Mungu mambo yalienda faster kuliko nilivyo fikiria mwanzo.
Ni kweli kigezo kimojawapo katika maombi ya Passport ni kua na kitambulisho cha Uraia.
Mimi sikua nacho na nilienda kumuona Commissioner wa Passort au tuseme Supervisor wao alinishauri niende NIDA nikapewe barua itakayothibitisha kua kweli nimeshafanya process zote za kitambulisho ila bado nasubiria kitambulisho. Kweli nilienda NIDA nikawaelezea na siku hiyo hiyo walinipa barua yenye namba yangu ya Kitambulisho cha Uraia na nikarudi kwa kamishina wa Passport (supervisor) akalipitisha ombi langu na ndani ya siku mbili Passport yangu ilikua tayari.
Pia kuna jamaa pia hakua na hicho Kitambulisho lakini alikua kapata safari ya haraka alimuona huyo Msimamizi akapitisha maombi yake na alipata Passport kesho yake.
Hivyo nakushauri nenda kamuone Kamishina wa Passport (Msimamizi mweleze hapo yote atakusaidia ni mtu mzuri sana hana longolongo. Usiishie kwa hawa wa mwanzoni wao wanafuata maelekezo kama Maroboti yaani sasa hv kama una vigezo vyote Passport ni ndani ya siku mbili mpaka tano yaani sio Issue tena.
Tatizo ni lako kutafuta pasi mpaka upate safari,uekua na pasi yako ya zamani yasingekukuta haya,acha kuishi kijimaNini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote idara ya uhamiaji ya nchi hii. Asante
Anamaanisha kwamba kuna upendeleo, watu fulani hawasumbuliwi hivyo!Mkuu unamaanisha nini hapo kwenye kijani? Mimi masuala ya kisiasa kwenye ishu nyeti kama hizi huwa nashangaa wanaoyaleta. This is very absurd
Usiwe na akili ndogo mkuu kitambulisho cha utaifa kina tija kushinda unvyofahamu wewe ndio maana tukaita mfumo wa kielectronic particular zako zote ziko na kila kitu kinacho kuhusuHili la kulazimisha kitambulisho cha uraia kuwa ni hitaji la lazima kupata passport ni takwa lisilo na tija. Kupata kitambulisho cha Taifa inachukua mwezi na ushee, uende Uhamiaji usubiri tena wiki mbili kupata passport na nchi yetu huwezi kupewa passport hadi uwe na safari ya ughaibuni. Hatari!
Vv
Wewe una akili kubwa lkn bado hujaelewa mantiki yangu! Kwa hiyo tusisafiri ughaibuni hadi zoezi la kutoa vitambulisho vya taifa litakapokamilika?Usiwe na akili ndogo mkuu kitambulisho cha utaifa kina tija kushinda unvyofahamu wewe ndio maana tukaita mfumo wa kielectronic particular zako zote ziko na kila kitu kinacho kuhusu
Mi nna skafu ya Arsenal, vp inafaa!Mkuu,nenda ukiwa umevaa shati ya kijani na suruali nyeusi.
Usisahau na skafu kama unayo,utakipata chap