Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Boss wako tu hajasafiri wewe unaenda wapi?
Bado tunajenga viwanda vya madiwani na kununua wapinzani kwanza tukimaliza ndo mtaanza kusafiri
 
PESA HAKUNA KILA KONA NA PIA HUU NI MUDA WA KUCHAPA KAZI NA SI KUZURURA HOVYOHOVYO MAANA MKIFIKA HUKO AKILI ZENU ZINAKUWA KAMA ZA KINA MANGE NA CHAHALI.OVA
 
Labda NIDA wangekusaidia na kukuandika hata barua kuwa wewe ni mtanzania na una hati zote na unahitaji kusafiri kiasi kitambulisho kinatengenezwa.
 
Mkuu nafikiri tunatakiwa tusisafiri nje ya nchi kama wengine.
Mimi nilienda ku renew nimekutana na kikwazo kama hicho.
Paspoti yangu inakoma 27/3/2018, hii inaninyima kupewa visa.
Nani wa kumshauri huyu mkuu wetu?
Mkuu hata kurenew inahitajika kitambulisho cha uraia?
 
Mkuu nafikiri tunatakiwa tusisafiri nje ya nchi kama wengine.
Mimi nilienda ku renew nimekutana na kikwazo kama hicho.
Paspoti yangu inakoma 27/3/2018, hii inaninyima kupewa visa.
Nani wa kumshauri huyu mkuu wetu?
Mkuu unaweza kueleza kiundani zaidi changamoto ulizokutana Nazi kurenew passport? Mimi nami nilikuwa najianda kwenda kurenew ya kwangu? Ahsante
 
Mimi nilikua hapo Kurasini wiki iliyopita na ninamshukuru Mungu mambo yalienda faster kuliko nilivyo fikiria mwanzo.
Ni kweli kigezo kimojawapo katika maombi ya Passport ni kua na kitambulisho cha Uraia.
Mimi sikua nacho na nilienda kumuona Commissioner wa Passort au tuseme Supervisor wao alinishauri niende NIDA nikapewe barua itakayothibitisha kua kweli nimeshafanya process zote za kitambulisho ila bado nasubiria kitambulisho. Kweli nilienda NIDA nikawaelezea na siku hiyo hiyo walinipa barua yenye namba yangu ya Kitambulisho cha Uraia na nikarudi kwa kamishina wa Passport (supervisor) akalipitisha ombi langu na ndani ya siku mbili Passport yangu ilikua tayari.
Pia kuna jamaa pia hakua na hicho Kitambulisho lakini alikua kapata safari ya haraka alimuona huyo Msimamizi akapitisha maombi yake na alipata Passport kesho yake.

Hivyo nakushauri nenda kamuone Kamishina wa Passport (Msimamizi mweleze hapo yote atakusaidia ni mtu mzuri sana hana longolongo. Usiishie kwa hawa wa mwanzoni wao wanafuata maelekezo kama Maroboti yaani sasa hv kama una vigezo vyote Passport ni ndani ya siku mbili mpaka tano yaani sio Issue tena.
 
Mimi niliandikisha kitambulisho changu cha uraia mwaka jana
Mwezi wa tisa pale Shaurimoyo zilipo ofisi ya TRA,
Ilikua ni katika kampeni za kurasimisha wafanyabiashara wadogo kariakoo.
Mpaka sasa sielewi ni wapi naweza kwenda kufwata kitambulisho changu cha uraia.
 
Nenda ofisi za NIDA utapata msaada wa kupata kitambulisho cha Taifa faster. Usikate tamaa
Vipi kwa wale wenye zile za mwanzo ambazo bado hazijamaliza muda wa kutumika? Wanahitaji kubadilisha kabla?
 
Nida wanasuasua sana kwenye mchakato wa vitambulisho vya uraia. Mchakato hauko intergrated enough kuweza kung'amua raia wa kweli na kuwapa vitambulisho right away. Kwanini wanatupiga picha na wanaondoka miezi miwili nila kupatia vitambulisho? Something fishy fishy kinanukia
Nadhani ningeona wamefikiri vyema kama hizo hati kwa sasa zisitolewe kwanza mpaka NIDA wawe wamemaliza kazi yao 99% kwa hilo gap tutumie hizi za kawaida kwa maana ziendelee kuzalishwa.
Maana hii nchi sio kisiwa kwamba hamna kutoka wala kuingia.

Maana kiujalisia NIDA lazima wachelewe kutokana na nature ya nchi yetu hasa kimuingiliano mikoa ya pembezoni nida haiwezi kutoa IDs kama njugu lazima kujiridhisha nk
 
Mimi niliandikisha kitambulisho changu cha uraia mwaka jana
Mwezi wa tisa pale Shaurimoyo zilipo ofisi ya TRA,
Ilikua ni katika kampeni za kurasimisha wafanyabiashara wadogo kariakoo.
Mpaka sasa sielewi ni wapi naweza kwenda kufwata kitambulisho changu cha uraia.
Bora yako wengine toka 2013[emoji30][emoji30][emoji30]
 
Nazani passport zimeisha sasa wanatafuta vijisababu.
 
Mkuu unamaanisha nini hapo kwenye kijani? Mimi masuala ya kisiasa kwenye ishu nyeti kama hizi huwa nashangaa wanaoyaleta. This is very absurd
Wewe ni nani kwenye hii nchi mpaka useme huo mchakato ni wa kisiasa? Wewe ni mbunge wa upinzani? Kiongozi wa chama cha upinzani? Au activist dhidi ya Serikali?

Ulienda ukiwa umevaa mavazi ya chama pinzani?
Hivyo videgree vyako viwili ndio vimeleta siasa? Kama "msomi" argument building inakua ya kipumbavu hivi bora hata usingeenda shule.
 
Nadhani ningeona wamefikiri vyema kama hizo hati kwa sasa zisitolewe kwanza mpaka NIDA wawe wamemaliza kazi yao 99% kwa hilo gap tutumie hizi za kawaida kwa maana ziendelee kuzalishwa.
Maana hii nchi sio kisiwa kwamba hamna kutoka wala kuingia.

Maana kiujalisia NIDA lazima wachelewe kutokana na nature ya nchi yetu hasa kimuingiliano mikoa ya pembezoni nida haiwezi kutoa IDs kama njugu lazima kujiridhisha nk
Kwani nani alikuambia passport za zamani hazitumiki?
 
ulikua hauko serious... goli la mkono lilikushinda....mimi siku mbili tu napata kila kitu ndanibya ofisi moja tu ya uhamiaji...mzee ulikua umafuata utaratibu...pole mkuu wakati mwingine unatakiwa uangalie kama viatu vya wale maofisa kama vina vumbi unavuta kiwi fasta wanasafisha viatu wanatoka kukutafutia kila kitu..
 
Pole kwa yalokukuta nilikuwa pale wiki mbili zilizopita.kurenew kitabu kilichokwisha na yule anaye tafuta kipya usumbufu na process ni kama ile ile tu.

Ushauri, kulalamika hakutasaidia hii ndio afrika mzee,cha kufanya komaa upate hicho kitambulisho,ukipambana ndani ya wiki mbili unakipata.kama utakuwa umechelewa safari yako pole sana.
 
Back
Top Bottom