Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kama ulishamaliza taratibu za NIDA kuna namba watakupa ambayo jamaa wa uhamiaji wataitumia kupata details zako za kitambulisho cha taifa
 
Mkuu umetoa povu jingi bila hata kuelewa comment yangu! Pole sana. Soma tena utanielewa. Nilikuwa namjibu aliyesema niende na kofia ya kijani kuomba passport kwa kumuambia kwanini anachanganya siasa kwenye suala langu
Naona hata ulichokiandika umeshakisahau,

Hii ni nani kaandika? ..... " Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala
hawa wasichanganye siasa na mambo ya
kitaalamu au ya kisayansi."
 
Je ulipata Passport Rafiki.

Wale ambao mlitumia utaratibu wa kuchukua barua kutoka NIDA je ilifanya Kazi.?????
 
Hiyo kitambulisho cha uraia ni upuuzi mkubwa.
Sina kitambulisho chochote
 
Salaam,

Majuzi nilipata fursa fulani ya kwenda nchini Ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda Uhamiaji pale Kurasini kushughulikia passport.

Lahaulaaa...

Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata passport ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.

Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje hicho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport .

Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambiwa vitambulisho vikiwa tayari Mwenyekiti wa Mtaa atawatangazia na mtapata.

Just imagine, eti askari wa Uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-

Cheti cha kuzaliwa,

Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,

Form ya kuomba passport ya Uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na Afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),

Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),

Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao

Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)


Cha ajabu sasa...
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu...

Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?

Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?

Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?

Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?

Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi.

Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema.

Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.

Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote Idara ya Uhamiaji ya nchi hii.

Ahsante
Mkuu kama tayari ulishapigwa picha kwenye kitambulisho cha uraia nenda ofisi ya nida, hsda makao makuu, watakupa barua tu utaipeleka uhamiaji utapata passport, mi kuna jamaa yangu nimemfanyia hivyo tayari ameshaipata passport yake. Ni kitu kidogo sana hicho mkuu
 
Mkuu kama tayari ulishapigwa picha kwenye kitambulisho cha uraia nenda ofisi ya nida, hsda makao makuu, watakupa barua tu utaipeleka uhamiaji utapata passport, mi kuna jamaa yangu nimemfanyia hivyo tayari ameshaipata passport yake. Ni kitu kidogo sana hicho mkuu
Passport zinachukua muda gani kutoka??????
 
Kwakweli sijui nani wa kumshauri mkuu wetu. Watanzania tunanyimana fursa wenyewe kwa wenyewe. Nimesikitika sana. Pole mkuu
Embu pitia hiyo attachment mkuu wakati mwingine hizi idara za serikali ni kwenda nazo kidigitali maana wengine huwa wanatoa jibu wanavyojisikia
 

Attachments

Back
Top Bottom