Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kimbembe! Kupata passport mpya ya kusafiria

Kupata kitambulisho sio kazi ndogo...mtaani kwetu hata dalili bado za kuanza kuna jamaa yangu toka mwezi wa sita mwaka jana mpaka leo kitambulisho hakija toka
 
Kwani nchi ni ya ccm mpk uichukie? Unaweza ukaipenda nchi na bado ukaichukia ccm, uzalendo hauhusishi chama cha siasa.
Babako akiwa mshari na asiyeleka hali ya kupenda inapungua
 
Kupata kitambulisho sio kazi ndogo...mtaani kwetu hata dalili bado za kuanza kuna jamaa yangu toka mwezi wa sita mwaka jana mpaka leo kitambulisho hakija toka
Mimi ni mmoja kati ya watz wa mwanzo kabisa kujiandikisha kupata kitambulisho cha taifa na ilinichukua miaka mitatu hadi kukitia mkononi. Kwa kuwa mwelekeo ni kuwa na kitambulisho cha taifa kwa kila raia, kutazuka foleni kubwa na misukumano ya hapa na pale mpaka lengo litakapotimia. Subira yavuta heri walisema wahenga.
 
Tatizo uhamiaji nao hawakupi passport hadi uwe na safari
Umeshaambiwa pasi ni haki yako,mtu atakaeniambia kuwa lazima niwe na safari hapo hapo naenda kwa kamishna mkuu kumshitaki kwa sababu pasi hiyo nailipia mimi huyo afisa kinamuuma nini
 
Salaam,

Majuzi nilipata fursa fulani ya kwenda nchini Ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda Uhamiaji pale Kurasini kushughulikia passport.

Lahaulaaa...

Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata passport ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.

Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje hicho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport .

Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambiwa vitambulisho vikiwa tayari Mwenyekiti wa Mtaa atawatangazia na mtapata.

Just imagine, eti askari wa Uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-

Cheti cha kuzaliwa,

Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,

Form ya kuomba passport ya Uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na Afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),

Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),

Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao

Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)


Cha ajabu sasa...
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu...

Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?

Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?

Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?

Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?

Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi.

Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema.

Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.

Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote Idara ya Uhamiaji ya nchi hii.

Ahsante
Sisi huku tabgu tuandikishe ni mwez wa 3 sasa na havijatoka na cjui vinatoka lini? tanzania ni shida everything goes slowly
 
I wish i could speak![emoji53][emoji53][emoji53]
d4bc15f73cb35b860ca2fd5e449d5b70.jpg
Siku yake ya kuzaliwa Leo. Happy Birth Day
 
Hivi na ukitaka kuonana na mkuu wa pale uhamiaji unafanyaje maana mim niliomba pass tangu mwaka jana mwezi wa sita hadi leo bado wananipa kalenda tu sijui nifanyaje?!
 
Hivi na ukitaka kuonana na mkuu wa pale uhamiaji unafanyaje maana mim niliomba pass tangu mwaka jana mwezi wa sita hadi leo bado wananipa kalenda tu sijui nifanyaje?!
Mwaka jana mkuu? Wakati siku hizo ilikuwa ni wiki2 unaenda kuchukua duu pole!
 
Watanzania tuache kua tunalalamika hovyo kwa kila jambo,tatizo tumezoea kuishi km wanyama bila utaratibu wowote so mkiletewa utaratibu flan mnaanza kulialia tu yn mnapenda kila kitu kiwe mteremko tu.
Hv mnaona ishu ya passport ni kitu kidogo sn yn uende tu asubuhi jione upewe?kigezo hicho cha kupata passport hadi uwe na kitambulisho cha taifa kilitangazwa siku ya kwanza ya uzinduzi wa hyo passport mpya inamana hukusikia?vitambulisho vya taifa wala havisumbui km una vigezo zikizidi sn ni wiki2 ushapata ila mtu kaa nyumbani tu anasuburi apate uhitaji wa hicho kitambulisho ndo aanze kukitafuta sasa kwa mwendokasi utakwama tu.
mkuuu kama mimi nimepoteza kitambulisho cha taifa na nahitaji nipate pasport mpya hii je nifanyeje nipate kitambulisho hiko cha taifa msaada jamaan na itachukua mida gani?
 
Mwaka jana mkuu? Wakati siku hizo ilikuwa ni wiki2 unaenda kuchukua duu pole!
We acha tu ndugu hadi kelo kila ukienda sound pata picha tangu mwezi wa sita hadi sasa ni mwezi wa tatu bado tu
 
Mazingira kama hayo yanafanya raia waichukie serikali yao halali bila sababu, sina hakika lakini watendaji serikalini pia wanaweza kuwa wanachangia hali hii mbaya.
Mimi biafsi nilifanya process zote za passport ya mtoto na nikalipia mwaka jana mapema December na nikaahidiwa kuipata February 2018 lakini cha ajabu nimeambiwa nianze maombi upya.
Mtoto ndio hivyo tena kachelewa kujiunga na chuo SA kwa sababu ya urasimu wa watendaji waliopo uhamiaji pamoja na kupeleka viambatanisho vyote muhimu.
 
We acha tu ndugu hadi kelo kila ukienda sound pata picha tangu mwezi wa sita hadi sasa ni mwezi wa tatu bado tu
Duu pole nakumbuka mie nilienda mwishoni mwa 2014 ndani ya wiki 2 tu tayari nikachukua nilifuata njia halali tu bila kona yeyote
 
Back
Top Bottom