Salaam!
Majuzi nilipata fursa flani ya kwenda nchini ujerumani kimasomo (Summer Schools), nikaenda uhamiaji pale kurasini kushughurikia passport.....
Lahaulaaa....
Naambiwa mkulu kasema kigezo cha kupata pass ya kusafiria ni kuwa na kitambulisho cha taifa. Nikashangaa sana.
Nikiangalia mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia namna unavyoendeshwa kwa kusuasua nikajiuliza maswali kwamba inawezekanaje icho kikawa ndio kigezo pekee cha kupata passport!
Nikijiangalia nina miezi kama miwili tangu nijiandikishe kupata kitambulisho cha uraia na mpaka leo sijakipata. Tuliambia vitambulisho vikiwa tayari mwenyekiti wa mtaa atawatangazia na mtapata.
Just imagine, eti askari wa uhamiaji ananiambia kwa confidence kabisa kwamba siwezi kupata hati ya kusafiria bila hicho kitambulisho licha ya kumuonyesha documents zote za muhimu ambazo ni:-
Cheti cha kuzaliwa,
Barua ya mualiko wa hiyo Summer School Scholarship,
Form ya kuomba passport ya uhamiaji yenye kukidhi vigezo na wadhamini wasiotia shaka (hii nilijazia mkoani kabla ya kushauriwa na afisa uhamiaji wa mkoani kwamba niende dar makao makuu),
Kopi za vitambulisho vingine muhimu vinavyoleta tija kwenye kuomba hati ya kusafiria (government issued),
Kopi za vyeti vya elimu yangu tangu sekondary mpaka shahada yangu ya pili,
Picha za passport size wanazozitaka wao
Kopi ya nakala niliyojiandikisha ili kupata kitambulisho cha uraia huku mkoani kwetu. (Ambacho bado nasubiri)
Cha ajabu sasa.......
Majibu niliyopewa ni kwamba tamko kutoka juu limetoka na kigezo ni kitambulisho cha uraia kwanza otherwise nenda ofisi ya rais akuandikie barua ya kuturuhusu sisi kuprocess hiyo hati unayoitaka. Nilijiuliza maswali mengi bila majibu.......
Je watawala wetu wanatambua namna mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia ulivyo slow huku uraiani?
Je watawala wetu na wafanyakazi wa uhamiaji hawana mbinu zingine za kung'amua eligibility ya kumpa mtu hati ya kusafiria?
Je watawala wetu wanatambua kwamba asilimia kubwa ya watanzania wengi kwasasa hawana vitambulisho vya uraia lakini isiwe kigezo cha kuwakosesha fursa zingine wanazozipigania kwa nguvu na jasho lao?
Je watawala wanatambua kwamba wao pia wanaweza kwa namna moja ama nyingine wakawa wanazuia maendeleo ya raia wao kwa kuweka vigezo visivyo na mashiko wala mamtiki kwenye masuala nyeti na yenye kuhitaji uharaka?
Mwisho ningependa kutoa rai kwa watawala hawa... Wasichanganye siasa na mambo ya kitaalamu au ya kisayansi. Nimekosa fursa hii adimu kwa kuchelewa kuscan pasi yangu ya kusafiria kwa wakati. Fursa imepeperuka kwakuwa kwasasa sina kitambulisho cha uraia ambacho nimeshajiandikisha kitambo tu ila hawataki kuvitoa mapema. Ama kwa hakika kuna baadhi ya mambo ya nchi hii yananisikitisha sana.
Nini maoni yako kama mwananchi wa kawaida. Washauri kitu chochote idara ya uhamiaji ya nchi hii. Asante