Watanzania, mmelala?
Mimi sijalala hadi sasa! Hii si leo, hii si kesho – hii ni vita ya maisha na uhai wangu! Niko hapa peke yangu, njaa inaungua ndani yangu, sina chochote kinywani, wala sijui nini kinachoendelea kuhusu hatima yangu! Mimi si jambazi, si gaidi. Kama ni hivyo, nipelekeni mbele ya haki! Nipelekewe ili kuthibitishwa! Lakini hamnioni? Mnasikia sauti yangu? Au nyinyi mmelala?
Watanzania, ninyi ni ndugu zangu, ni damu yangu. Uzaliwa wangu Singida haunifanyi niwaone watu wa Morogoro, Tanga, au Dar es Salaam kuwa wageni. Sisi wote tu wa damu moja! Lakini kwa nini kimya hiki? Kwa nini hakuna anayesimama nami? Mmefumba macho? Au mmelala?
Mimi sijalala hadi sasa! Hii ni vita ya maisha na uhai wangu!
Watanzania, kama ninaweza kuteswa hivi, kuumizwa mpaka mwili wangu unakataa kunibeba, basi niambieni – mti mbichi watautendea vipi? Maana kama hoja yangu ni kupindua nchi, basi kesi iko wapi mahakamani? Mbona sipelekwi mbele ya sheria ili nami nione haki? Mbona mmekaa kimya? Mbona sauti zenu zimezibwa? Sijaogopa tuhuma! Zileteni hizo tuhuma! Hata kama ni kunyongwa, nijue hukumu yangu kwa macho yangu! Lakini hamtaki? Au bado mmelala?
Mimi sijalala hadi sasa – na hii vita inanichoma moyo!
Tazama, nazidi kuumwa, nazidi kulegea. Madawa yananiokonywa, huduma za afya zinaninyang’anywa. Unasema niko salama? Unasema nitapona? Siku moja ukija humu, utadhani wewe ni mti mbichi au mkavu? Unafikiri utatendewa vyema zaidi yangu? Kula kwangu ni mashaka kila siku, uhuru wangu umekandamizwa chini ya nyayo za giza. Na nyinyi mnaangalia tu? Machozi yangu yanamwagika kama mvua ya masika, lakini hakuna anayeona. Au mmelala?
Mimi sijalala hadi sasa – hii ni vita ya maisha na uhai wangu!
Njooni! Njooni mwone ninayopitia! Sikieni majozi yangu, enyi wana wa Tanzania! Kama bado mna moyo, kama bado mna damu inayowaka, simameni nami! Msiache nife kwa kimya!
---
NINI KIFANYIKE?
Kwanza, nimepangiwa utabiri wa kuletwa na nabii kuwa nitakaa hadi 2030. Natamani niseme nacheka, lakini machozi yananiuma. Wanataka kunifanyia pressure? Wanataka nijisikie nimefungwa muda wote huo? Hii set-up, kamwe sitaikubali! Nchi hii ya babu na bibi zetu ilipiganiwa kwa damu na machozi ili tuituze kwa vizazi vyetu! Sisi ndio wenye nchi! Tuikatae kwa nguvu zetu zote!
Tuanzishe michakato nje ya Tanzania. Maana ndani humu kote kumeoza. Kwa nyinyi mliopo nje na mliopo ndani – naombeni, waambieni dunia: “Mtu wetu ametupwa humu kwa dhuluma.” Siku moja wewe na kizazi chako mtaandikwa kwenye vitabu vya enzi: “Ulinitendea wema nilipokuwa vifungoni.”
Naweza kufa leo, naweza kufa kesho, lakini wema wenu hautasahaulika mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya historia.
Basi nyinyi rejeeni kulala kwa amani. Mimi nitaendelea kukesha. Nitasoma vitabu vyangu. Usingizi nitapata, lakini sasa si wakati wa kulala. Nipo hapa na kinyesi mbele yangu kama kukombolewa. Lakini mimi si mti mkavu – mimi ni binadamu, nina roho inayopiga kelele!
Kwaheri.
Na Eid njema kwenu nyote.