VERITE-NUE
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 1,481
- 1,450
Kama kuna kitu kigumu maishani, ni kumiliki nyumba nchini Rwanda. Kuanzia ardhi, mpaka vibali, ni mtihani. Jambo hili husababisha walio wengi wajenge tu kutokana na uwezo wao. Mbaya zaidi, kila eneo lina masterplan. Haijalishi ni kijijini, bila kibali, bila ramani, jenga, utajuta.
Imekuwa mtindo sasa, watu wanajenga, mwishoe wanaambiwa wanaishi katika maeneo hatarishi. Katika maeneo hayo, umeme, maji, barabara vinaletwa. Je, serikali inayoleta miundo mbinu hiyo, inakuwa haioni?!
Maeneo ya vijijini, mpaka mtu anaandaa kiwanja, anamwaga mawe na mchanga, msingi unajengwa, nyumba inasimama, inawezekwa na bati zinapigiliwa: je, ni kwamba ngazi zote hazijui!? Maana nyumba haijengwi usiku au siku moja.
Hapa ndipo swala la rushwa linaingia. Viongozi wasioajibishwa, huamua wanayoyataka na kupitia udhaifu wa wananchi.
Hali hii inapelekea wananchi walio wengi kukosa imani na uongozi wa nchi. Japo hawana wa kumlilia, mwishoe inakuwa wanaishi na viongozi, kwa sababu tu ya ulazima,si sababu ya kulidhia.