Kilio cha Walimu nchini (mwaka 2021)

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,138
2,000
KILIO CHA WAALIMU NCHINI TANZANIA!

Nimepokea waraka kutoka kwa mmoja wa waalimu akiwawakilisha waalimu wenzake. Kwa sababu za unyeti wa maudhui ya waraka huo, kiapo changu cha Uaskofu kinaniruhusu kutokutaja jina la mtu aliyeniletea! Nimeamua kuuchapa waraka huo katika ukurasa wangu ili kusaidia kilio cha waalimu kuwafikia wahusika na jamii kwa ujumla!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

"Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Heri ya Mwaka Mpya 2021. Nataka nikueleze kuhusu kilio cha walimu wa Tanzania kwa sasa.
Kilio kikubwa cha walimu ni madaraja. Kama unavyofahamu, mishahara katika Utumishi wa Umma haijaongezwa kwa miaka 5 iliyopita, hivyo tegemeo kubwa la walimu ni kupanda madaraja lakini nako ni kugumu.

Mathalani, wako walimu wa ajira mpya wa mwaka 2014, hawa ilikuwa wapande madaraja mwaka 2019 (mwaka 1 probabation +miaka 4 ya kutumikia cheo). Wapo walimu waliopanda madaraja 2015, hawa walipaswa kupanda 2019 baada ya kutumikia cheo kipya kwa miaka 4 lakini hawajapanda na hakuna dalili za kuwapandisha.

Chama cha Walimu (CWT) kipo kimya, hakuna wa kuwasemea Walimu wa Tanzania. Walimu nao wapo kimya, wanaogopa. Utumishi wa Umma umekuwa mzigo mzito ndani ya awamu hii ya uongozi. Naomba Baba Askofu, lizungumzie hili jambo pengine wenye mamlaka watasikia na kutendea kazi!

Ni mimi Mwalimu."
 

katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
837
1,000
Mwalimu mwaka jana tarehe 28/10 ulitangaza matokeo ya wananchi au ya polepole na Sirro?
Kama ni namba mbili basi tuondokee hapa.
Hivi baada ya mwaka moja wa probation unakaa tena minne ndipo upande daraja na si mitatu?Walimu mnatia huruma lkn Hali hiyo si kwa Walimu tu ni kea watumishi wote.kuna mmoja alinidokeza lkn siyo mwl yy tangu 2004 hajawahipanda sababu walikuwa kwenye special scale na Sasa wamerudishwa kwenye pgss na bado hajapanda
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,736
2,000
Hawa ni mawakala wa CCM wa wizi wa kura wacha wakome..mshahara wa laki tatu na nusu ataishije mjini huku una mke na watoto 3 dadadeq.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom