Kilio cha Walimu nchini (mwaka 2021)

Hao walimu,hawaoni miradi inayotekelezwa?
Walimu wangekua hawajui wapi pesa imeelekezwa,wangezidi kumsifu mzee.
SGR na Nyerere dam ni mifano iliyodhahiri.
 
Angalia huyu askofu asikufanye kama mtoto wa Zari, maana kila siku unaleta upuuzi wake JF
 
Aisee Mimi sio mwalimu Ila ni mtumishi idara ya mifugo niliajiriwaga mwaka mwezi may 2014 .

Aisee yaani miaka ya nyuma ilikuepo mtumishi wa ajira mpya atastahili kuthibitishwa kazini mwaka mmoja( probation) then baada ya mwaka wa probation anaka miaka mitatu then anapanda daraja baada ya hapo after every three years mtumishi atastahili kupata promotion Ila alipoingia Mheshimiwa huyu Sheiria ikabadilishwa ajira mpya ni ikapelekwa miaka mitano na wengine mpaka miaka minne ipite.

Lakini hata hivyo hiyo sheria mpya haifanyi kazi kwani mpaka sasa watu tuna miaka 7bila kupanda daraja Kwa yote hayo Mheshimiwa huyu akaongeza makato y bodi kutoka 8% to 15 % yaani ni awamu ngumu kwa watumishi wa low levels
 
Ninyi matichya sindiyo mlituletea hawa watu kwa kishindo!! Unless hamjui kusoma na picha hamuoni... Sasahivi kipaumbele ni kujenga miundombinu kwaiyo suala la promotion na nyongeza lisubiri wakati wanaondoka msitupigie makelele!!
 
Kinachofahamika hivi sasa ni kuwa hakuna chama cha wafanyakazi chanye maana tena, taifani kama mengine mengi na yasiyosemwa yalivyopoteza maana.
 
Ni seme kweli hakuna watu wanafiki Kama walimu wa nchi hii ...Kuna msemo unasema KARMA IS A BITCH..
 
KILIO CHA WAALIMU NCHINI TANZANIA!

Nimepokea waraka kutoka kwa mmoja wa waalimu akiwawakilisha waalimu wenzake. Kwa sababu za unyeti wa maudhui ya waraka huo, kiapo changu cha Uaskofu kinaniruhusu kutokutaja jina la mtu aliyeniletea! Nimeamua kuuchapa waraka huo katika ukurasa wangu ili kusaidia kilio cha waalimu kuwafikia wahusika na jamii kwa ujumla!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki

"Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Heri ya Mwaka Mpya 2021. Nataka nikueleze kuhusu kilio cha walimu wa Tanzania kwa sasa.
Kilio kikubwa cha walimu ni madaraja. Kama unavyofahamu, mishahara katika Utumishi wa Umma haijaongezwa kwa miaka 5 iliyopita, hivyo tegemeo kubwa la walimu ni kupanda madaraja lakini nako ni kugumu.

Mathalani, wako walimu wa ajira mpya wa mwaka 2014, hawa ilikuwa wapande madaraja mwaka 2019 (mwaka 1 probabation +miaka 4 ya kutumikia cheo). Wapo walimu waliopanda madaraja 2015, hawa walipaswa kupanda 2019 baada ya kutumikia cheo kipya kwa miaka 4 lakini hawajapanda na hakuna dalili za kuwapandisha.

Chama cha Walimu (CWT) kipo kimya, hakuna wa kuwasemea Walimu wa Tanzania. Walimu nao wapo kimya, wanaogopa. Utumishi wa Umma umekuwa mzigo mzito ndani ya awamu hii ya uongozi. Naomba Baba Askofu, lizungumzie hili jambo pengine wenye mamlaka watasikia na kutendea kazi!

Ni mimi Mwalimu."
Na vipi kuhusu wadogo zetu waliohitimu vyuo tangu mwaka 2015 hawajaajiriwa mpaka wanaanza kuzeeka?
 
Wa

walimu wanatia aibu wao muda wote ni kulia lia tu, hivi walilazimishwa kusomea ualimu kama walikua hawaupendi.
 
Back
Top Bottom