SoC02 Kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

O M R

New Member
Sep 13, 2022
1
0
Kilimo-ni shughuli inayofanywa na binadamu kujipatia chakula cha kujikimu kupitia mazao ya chakula na biashara mfano: mahindi,viazi, mihogo, mtama,ulezi,pamba,katani,mikonge nakadhalika na kilimo cha wanyama mfano: ng'ombe,mbuzi,kondoo, nakadhalika na uvuvi wa samaki.kilimo hupaswa kuwa njia ya uzalishaji chakula endelevu na biashara ya maendeleo kwa ujumla.

Zifuatazo ni faida za kilimo kwa vijana na taifa kwa ujumla zitokanazo na kilimo cha chakula na biashara.

Kuuza uchumi-
Katika kilimo tunaweza kukuza uchumi katika familia na jamii kwa ujumla mfano: kwenye mazao ya pamba, katani, mikonge na mfano kwa wanyama, ngozi za wanyama kwa ajili ya kutengenezea bidhaa zitokanazo na ngozi,na vitoweo pia,hii husaidia ongezeko la uchumi kupitia kodi na tozo.

Kuongeza kipato kwa wakulima-kilimo husaidia watu katika vipato vyao binafsi na kuweza kujikimu kimaisha pamoja na familia zao, husaidia kupunguza umaskini katika jamii.

Kutoa ajira kwa mtu/watu-kilimo husaidia katika hutoaji fursa ya ajira kwa watu wasio kuwa na ajira mfano: katika ufugaji mtu anamifugo (mbuzi) takribani 3000 hatoweza kumudu katika kuhudumia mifugo wote hao bali huajiri mtu/watu katika kusaidia kuhudumia mifugo na, mfano katika mazao mtu anashamba (mahindi)heka 10 hatoweza kumudu kuhudumia peke yake shamba lote bali huajiri watu wa kupalilia,kumwagilia,kuvuna.mpaka hapo kilimo kimewapa watu kadhaa kuwa na ajira na kupunguza umaskini uliokithiri kwa watu wengi wao

Kupunguza baa la njaa-baa la njaa ni changamoto sana inapotokea katika jamii hufanya mili kudhoofu, kupungua kwa nguvu kazi,vifo holela holela.hivyo kilimo husaidia kutokomeza baa la njaa katika jamii na taifa kwa ujumla kupitia kilimo cha chakula na biashara.
-vijana wengi wao wakihitimu vyuo vikuu wanakosa ajira wanashindwa kujishughulisha wakisubiri kuajiriwa,faida ya kilimo kwa vijana.

Kupunguza wimbi la ukosefu wa ajiri kwa vijana-hasa katika nchi yetu ya tanzania vijana wengi wamekaa wakisubiri kuajiriwa sio kutumia fursa ya kujiari binafsi mfano:watumishi wa umma ni laki nane na wanaomaliza vyuo kwa mwaka ni laki nane iwapo vijana wakijihusisha na kilimo watapunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana na kukaa tu mitaani bila shughuli za kujipatia kipato na kujikimu kimaisha.

Kujiepusha kuwa katika makundi mabaya na uharifu-vijana wengi wanaokosa ajira huishia kujiingiza katika makundi mabaya yasiyo faa katika jamii na uharifu,hivyo akiwa na kazi ya kujishughulisha na kilimo humsaidia kutokuwa na wakati/muda wa kujiingiza katika makundi mabaya na kuingia kwenye utumiaji mfano:madawa ya kulevya,bangi, uharifu nakadhalika.

Kukuza uchumi binafsi na taifa-faida ya kilimo kwa vijana kujipatia kipato cha kujikimu wao binafsi na familia zao na ongezeko la uchumi wa taifa kupitia kilimo biashara.

Kulisaidia taifa-katika taifa vijana ni chachu katika jamii na asilimia kubwa wanauwezo wa kuleta maendeleo makubwa katika jamii iwapo wakithubutu,hivyo vijana wakijitoa katika kilimo huweza kusaidia taifa katika nyanja ya biashara na kiuchumi pia.

Kuongeza ubunifu na kijiamini-raha ya kilimo huongeza ubunifu kwa mtu na kujiamini katika shughuli anayofanya ya kilimo na kumuongezea maarifa na ustadi katika kilimo iwe katika mazao, mifugo,uvuvi.

Mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na kufanywa na serikali kuboresha kilimo

Maendeleo katika sekta ya kilimo katika mazao, ufugaji na uvuvi ni muhimu katika kukuza uchumi wa taifa na kuleta uamsho kwenye ukuaji wa kilimo.

Sayansi na teknolojia-hii itarahisisha katika kukuza kilimo mfano mashambani, matumizi ya vifaa vya kisasa kama vile trekta, mbolea nakadhalika ili kuleta mavuno na mazao bora hivyo kupatikana kwa vifaa vya sayansi na teknolojia itaboresha kilimo kwa kiasi kikubwa.

Kuajiri wataalam watakao shughulikia kilimo na kutoa mazao bora-serikali ikiajiri wataalam wengi na kuwapa vitendea kazi mfano: mabwana shamba na maafisa ugavi watakao tembelea wakulima na kushauri juu ya namna ya kufanya ili kupata mazao mengi na bora na faida, hivyo itaboresha hali ya wakulima kiuchumi na kuinua sekta ya kilimo na kuipatia pia serikali manufaa kwa kupitia kilimo.

Kuanzisha shule, taasisi na vyuo vinavyofundisha kilimo mfano: sokoine university of agriculture-serikali inapaswa kuanzisha shule na vyuo vya kutosha vinavyofundisha kilimo kwa vitendo zaidi pia masomo yawekwe katika mitaala ya elimu na kupewa pia kipaumbele ili wajifunze na waweze kujiari kupitia kilimo hicho.

Kutoa vifaa vya kisasa vya kilimo kwa wakulima-serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mfano mabenk ili kuboresha kilimo kwa kugawa vifaa kama vile matrekta, mbolea pamoja na wataalam wa dawa za mazao,hii itakuza kwa ukubwa sekta nzima ya kilimo

Kutunga sera zinazohamasisha kilimo-mfano wa sera zinazohamasisha kilimo ni kama "tokomeza baa la njaa", "kilimo kwanza", "kilimo ni uti wa mgongo" inapaswa kuwepo na kauli mbiu nyingi za kuamasisha hali ya morali kwa wakulima hasa vijana kutambua na kuelewa jinsi kilimo kilivyo na fursa kwa nchi na wananchi kwa ujumla,hii itawezesha kuboresha na kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

Kupunguza kodi zisizo za lazima kwa wakulima-kupitia serikali k umekuwa na kodi mbalimbali ambazo nyingi huwaumiza wakulima ambao ni maskini hivyo ili serikali iweze kuinua kilimo inatakiwa kupunguza kodi na tozo ili kuwawezesha wakulima kufanya kazi kwa wingi na ustadi wa hali ya juu.

Bei nafuu za pembejeo-katika kuboresha kilimo pembejeo hutakiwa kuwa bei nafuu ili kuwawezesha wakulima wa aina zote kuweza kumudu kununa vitu hivyo mfano: mbolea,dawa hii itapelekea pia kupata matunda mazuri na bora katika kilimo.

Ushindani katika kilimo-serikali inapaswa kuweka mikakati ya kuwepo kwa ushindani katika sekta ya kilimo itasaidia kuinuka na kukua kwa sekta ya kilimo mfano: serikali kutoa zawadi na tuzo kwa mkoa utakao ongoza kwa uzalishaji kilimo kwa wingi hii itawapa chachu wakulima kuwa na bidii na jamii kwa ujumla katika kilimo.

Kilimo ni muhimu sana katika jamii na taifa hutupa chakula na biashara pia itokanayo na kilimo hivyo husaidia katika kutokomeza baa la njaa, kupunguza umaskini uliokithiri,fursa na kuongeza ustadi na kujiamini pia huboresha mahusiano katika familia, kilimo kipewe kipaumbe maana maisha ya binadamu yanaendeshwa na kilimo ambacho hutoa chakula kwa ajili ya binadamu,kilimo haibagui maskini wala tajiri,jinsia,elimu bali hufanywa na mtu/watu waliotayari kujihusisha na kilimo cha aina yoyote ile.
 
Back
Top Bottom